Slim5
JF-Expert Member
- Jan 7, 2014
- 28,163
- 37,801
Huo msafara nimekutana nao maeneo kabla ya UBENA. Tumesimamishwa kama dk 40!Ni kawaida kwa viongozi wetu kuwa na misafara mikubwa na yenye mbwembwe kibao, lakini kwa mtukufu rais wangu wa awamu hii umekuwa kero na mateso kwa watumiaji wa barabara kwa kuzingatia kwamba mara nyingi anasafiri kwa barabara, hali imekuwa mbaya na mateso ya hali ya juu.
Leo wakati naelekea Mpwapwa tumekwamishwa kwa zaidi ya saa moja kwenye kituo cha mafuta jirani na kituo kikuu cha mabasi Morogoro, kwa kweli nashauri wahusika wabuni njia mbadala ya kumsafirisha rais wangu.