Kero: Msafara wa Rais umekuwa mateso kwa watumiaji wa barabara

namraroh

Senior Member
Sep 9, 2010
114
124
Ni kawaida kwa viongozi wetu kuwa na misafara mikubwa na yenye mbwembwe kibao, lakini kwa mtukufu rais wangu wa awamu hii umekuwa kero na mateso kwa watumiaji wa barabara kwa kuzingatia kwamba mara nyingi anasafiri kwa barabara, hali imekuwa mbaya na mateso ya hali ya juu.

Leo wakati naelekea Mpwapwa tumekwamishwa kwa zaidi ya saa moja kwenye kituo cha mafuta jirani na kituo kikuu cha mabasi Morogoro, kwa kweli nashauri wahusika wabuni njia mbadala ya kumsafirisha rais wangu.
 
kumbe mzee wa msoga Alitukanwa bure wakati alipokuwa anatumia usafiri wa Anga afanyapo ziara mikoani?
 
Na Mimi pia yamenikuta hayo oil com kihonda Nimekaa zaidi ya saa moja Kimsubr mtukufu apite nimekereka sana
 
Reactions: PNC
Eti kwa sababu ya kutaka sifa kuwa anatumia usafiri wa barabara ndio atese Watanzania wengine ambao pia wanahitaji barabara kwa kufanya shughuli zao!!! Hii haikubaliki kabisa!

Halafu sio kweli kwamba kutumia magari anaokoa pesa....Usikute ndio anazidisha gharama kuliko angetumia usafiri wa anga.
 
Huo msafara huwa ni kero sana Kwa abiria Wa daladala
 
Safi, na nyie mikoani msafe kidogo maana huku dar ni kero.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…