Desprospero
JF-Expert Member
- Feb 1, 2023
- 1,009
- 2,470
Tunadhani hii case closed!
Wengi ndani na nje ya CCM mmekuwa mkihoji kwa nini Mwenezi wa CCM Paul Makonda amekuwa akifanya ziara na misafara mirefu kuliko hata PM na Naibu PM.
Katika ziara zake amekuwa akisikiliza kero za wananchi na kuwapigia simu papo kwa papo Waziri au Mkurugenzi na kutoa maagizo mazito. Wengi wamehoji mipaka yake ya kazi kama Katibu wa H/K Itikadi na Uenezi.
Akiwaapisha Wakuu wa Mikoa leo Rais Samia Suluhu Hassan amesema, "utakuta mambo yanaharibika, haki za watu zinadhulumiwa, pesa zinatumika hovyo, yani mpaka Paul Makonda apite ayagundue ndipo yatatuliwe. Makonda ameyabaini mengi sana. Sasa msisubiri mpaka Makonda apite ndipo muwajibike".
Kwa kauli hii kila mtendaji wa Serikali na viongozi wote wa chama mtambue kuwa sauti ya Makonda ni ya Rais Samia Suluhu Hassan. Kwa maneno mengine Paul Makonda ni Bosi wenu wote na ndio maana alimwagiza hata Waziri Mkuu na Makamu wa Rais.
Case closed!