Kauli ya Rais imevunja Katiba; kwa kuingilia uhuru wa Mahakama

Mahakama ina taratibu zake yeye kusema vile nikama kuishinikiza mahakama itoe maamuzi kuwa favour wao while mahakama ni impartial abiter lazima isikilize pande zote mbili ili wa comply na principal of natural justice, hata kama mtu wamemkamata na kidhibiti once aka plea not guilty court should enter to the full trial.
 
Napenda kusema wazi kabisa kua Rais wetu alishauriwa vibaya, na waliomshauri wamemweka katika kikaango na wadau wa sekta ya sheria.

Hii ni kutokana na kauli aliyoitoa jana katika maadhimisho ya siku ya sheria duniani au " Law day" pale aliposema kwamba kuna kesi zaidi ya 400 zilizopo mahakamani ambazo kama zikiendeshwa ipasavyo basi serikali inaweza kujipatia kiasi cha shilingi trilioni moja kama fidia toka wa wadaawa, ambazo ameahidi kuwapatia mahakama kiasi cha shilingi bilioni mbili.

Kuna mambo machache ya kuangalia hapa ;

1. Ni hakimu gani au jaji atakayekua tayari kutoa hukumu dhidi ya serikali.

2. Ni wakili gani anapoteza muda wake kwenda mahakamani wakati anajua kua mteja wake anakwenda kushindwa.

3. Vipi kuhusiana na uhuru wa mahakama kufanya kazi yake bila kuingiliwa.

4. Vipi kuhusiana na haki ya mtuhumiwa kuwa hana hatia mpaka pale mahakama itakapomtia hatiani.

5. Ina maana serikali itashinda kesi zote 400??

Napenda nikumbushe kwamba mashauri yakishafikishwa mahakamani mambo hua yanaendeshwa kwa taratibu, kanuni na sheria ambazo tayari zipo, hayaendeshwi kwa kauli za kisiasa, huko ni kuingilia uhuru wa mahakama.

Kauli ya Rais ukiitazama kwa kina utaona kwamba imevunja ibara ywa 13 (6) (a) na 107B ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , 1977, nanukuu;

Equality before the law 13.-(1) All persons are equal before the law and are entitled, without any discrimination, to protection and equality before the law.

(6) To ensure equality before the law, the state authority shall make procedures which are appropriate or which take into account the following principles, namely: (a) when the rights and duties of any person are being determined by the court or any other agency, that person shall be entitled to a fair hearing and to the right of appeal or other legal remedy against the decision of the court or of the other agency concerned;

Independence of the Judiciary 107B. In exercising the powers of dispensing justice, all courts shall have freedom and shall be required only to observe the provisions of the Constitution and those of the laws of the land.

Ukipitia ibara zote mbili, utaona kwamba kwa kauli ya Rais, majaji na mahakimu hawatakua katika hali ya uhuru wa kufanya kazi zao kwani hawatataka kwenda kinyume na maagizo ya rais ambayo yanaelekeza makusanyo ya trilioni moja.

Vile vile haki ya wadaiwa itakua imevunjwa maana mpaka sasa wanachukuliwa kua tayari ni wakosaji wakati mashauri bado hayajamalizika na mahakama kufikia maamuzi yake.

Jambo la msingi kabisa la kufanyika hapa ni kwa Rais, kuiondoa kauli ile kwani kwa kiasi kikubwa italeta usumbufu mkubwa katika mashauri yanayoendelea mahakamani.

Wanasheria wanaweza kutuhumu majaji kua wamefikia maamuzi yao kutokana kua waliahidiwa bilioni miambili na rais , kwahiyo wanafanya hivyo kutimiza malengo yao.

Kama mwananchi wa kawaida na mdau wa sheria, kwakweli kauli ile haikua sahihi. Na inahitajika uamuzi wa busara kabisa ufanyike ili hili jambo liishe vyema kwani kuna kila dalili ya maombi kupelekwa mahakamani ili mashauri yasimamishwe mpaka kauli hiyo itakapofutwa.

Nawasilisha.
Kwenye hili watz tuache porojo, hao vigogo waliopewa dhamana ya kuongoza mashurina tahasisi za umma na kufanya ufisadi kama NIDA,TRA na TPA hawajavunja sheria!
Je mnataka JPM magufuli awachekee chekee kama JK alivyowachekea na kuongea kwa lugha nzuri na wezi wa EPA! ?
Watanzania tubadilike, hata huko wanakoheshimu utawala wa sheria na haki za binadamu hawana mzaha na wahujumu uchumi waliwashughulijia ndiyo maana sahz kuna kuheshimu sheria!
Mwacheni Mhe. anyooshe hii nchi na hapa lazima udikteta kidogo uwepo!?
 
Kuingilia uhuru wa mahakama nafikiri unavunjwa pale ambapo kuna kesi ipo mahakamani inaendelea na serikali kutoa shinikizo nini kifanyike. Pili, sidhani kama Rais amezungumzia kitu chochote ambacho kipo mahakamani zaidi ya kuwataka Mahakama, Polisi na DPP kumaliza mashauri haraka iwezekanavyo!
Kuna kesi tayari zinazoendelea, kumbuka hilo, na malengo hapa ni kukusanya fedha, na mahakama imeahidiwa bilioni 200, na nyingine kununulia ndege, ukiacha ushabiki, ambao hata mimi pia kama mwana ccm natakiwa kutetea kauli ya rais, na kufikiri kwa kutumia milango yote ya fahamu utaona ninalolisema, pale Rais kashauriwa vibaya, hakutkiwa kuongea vile.
 
kazi sana kumridhisha mtanzania

Umeona dada yangu? Yaani sisi binadamu wa Tanzania ni shughuli pevu.....JK tulikuwa tunamuona dhaifu! Kaja huyu tunalilia rule of law! To be honest sometimes you understand why watawala behave the way they do. The good thing is that hata kwenye hotuba yake Magufuli alilitegemea hili na alilisema. Kiukweli ile hotuba ya Magufuli ukiisikiliza you can feel it..... Ilinivuta hisia sana (especially issue ya vitambulisho na ufisadi kwenye nchi masikini kama ya kwetu)....
 
Kweli wabongo tuna gubu, katika yote aliyoongea umeona umkosoe tu? msifie basi hata kwa mazuri aliyozungumza. Binafsi sijaona kama amewapangia maamuzi majaji naona kama amewapa mkakati wa kazi tu bado maamuzi yatatolewa na majaji na kwa kufata sheria za nchi.Tatizo wapiga dili wengi walizoea ikulu kama kimbilio lao.
Watanzania tunasifia performance ya Kenya-Kweny miundombinu na Rwanda &Kagame tunadhani walishushiwa hayo mafanikio, nop waliyafanyia kazi kwa jasho la damu!
 
Ni swala gumu kulijadili hili na mimi naweza kusema umeliangalia kwa macho mepesi sana.

kumbuka raisi alikuwa amevaa kofia nyingi hivyo kila alilolizungumza ni lazima ujiulize aliliongea kwa kutumia kofia ipi.

zipo tetesi mitaani kuwa serikali huwa haishindi kesi hata moja ya madai bali yenyewe huwa inashindwa tu iwe imepelekwa kama mdaiwa au inadai. yasemekana hili hutokana na rushwa iliyojikita katika mifumo ya kutoa haki na kwa upande wa serikali huwa haitoi rushwa hivyo maamuzi huwa sekita binafsi wanashinda ama kutoa kitu kidogo ili kuepuka kulipa faini kubwa serikalini au kutoa kitu kidogo ili mahakama zetu zihalalishe malipo makubwa kwao kutoka serikalini.

sasa bila kupepesa utaona kuna jipu katika mfumo wa utoaji haki linalohitaji kutumbuliwa. lakini hilo haliko chini ya mamlaka ya mtumbua majibu hivyo alikuwa anajaribu kufanya linalowezekana katika uwezo wake kutumbua jipu lililo katika mfumo wa mahakama. Hapa aliongea kuwaonyesha walioko katika mhimili huo mambo ambayo yanawakwamisha wao kama wadai katika kesi walizowalisilisha na kwa kutambua wajibu wa serikali kufacilitate kifedha mhimili huo ili uendeshe shughuli akatoa ahadi.

kwangu mimi naona hotuba ya raisi ikitoa changamoto kwa wanasheria kumaliza kesi ndani ya mda na kutoa maamuzi ya haki kwa anayestahili na sote tujaribu kuielekeza hotuba yake kutoa msukumo huo.

Napenda kusema wazi kabisa kua Rais wetu alishauriwa vibaya, na waliomshauri wamemweka katika kikaango na wadau wa sekta ya sheria.

Hii ni kutokana na kauli aliyoitoa jana katika maadhimisho ya siku ya sheria duniani au " Law day" pale aliposema kwamba kuna kesi zaidi ya 400 zilizopo mahakamani ambazo kama zikiendeshwa ipasavyo basi serikali inaweza kujipatia kiasi cha shilingi trilioni moja kama fidia toka wa wadaawa, ambazo ameahidi kuwapatia mahakama kiasi cha shilingi bilioni mbili.

Kuna mambo machache ya kuangalia hapa ;

1. Ni hakimu gani au jaji atakayekua tayari kutoa hukumu dhidi ya serikali.

2. Ni wakili gani anapoteza muda wake kwenda mahakamani wakati anajua kua mteja wake anakwenda kushindwa.

3. Vipi kuhusiana na uhuru wa mahakama kufanya kazi yake bila kuingiliwa.

4. Vipi kuhusiana na haki ya mtuhumiwa kuwa hana hatia mpaka pale mahakama itakapomtia hatiani.

5. Ina maana serikali itashinda kesi zote 400??

Napenda nikumbushe kwamba mashauri yakishafikishwa mahakamani mambo hua yanaendeshwa kwa taratibu, kanuni na sheria ambazo tayari zipo, hayaendeshwi kwa kauli za kisiasa, huko ni kuingilia uhuru wa mahakama.

Kauli ya Rais ukiitazama kwa kina utaona kwamba imevunja ibara ywa 13 (6) (a) na 107B ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , 1977, nanukuu;

Equality before the law 13.-(1) All persons are equal before the law and are entitled, without any discrimination, to protection and equality before the law.

(6) To ensure equality before the law, the state authority shall make procedures which are appropriate or which take into account the following principles, namely: (a) when the rights and duties of any person are being determined by the court or any other agency, that person shall be entitled to a fair hearing and to the right of appeal or other legal remedy against the decision of the court or of the other agency concerned;

Independence of the Judiciary 107B. In exercising the powers of dispensing justice, all courts shall have freedom and shall be required only to observe the provisions of the Constitution and those of the laws of the land.

Ukipitia ibara zote mbili, utaona kwamba kwa kauli ya Rais, majaji na mahakimu hawatakua katika hali ya uhuru wa kufanya kazi zao kwani hawatataka kwenda kinyume na maagizo ya rais ambayo yanaelekeza makusanyo ya trilioni moja.

Vile vile haki ya wadaiwa itakua imevunjwa maana mpaka sasa wanachukuliwa kua tayari ni wakosaji wakati mashauri bado hayajamalizika na mahakama kufikia maamuzi yake.

Jambo la msingi kabisa la kufanyika hapa ni kwa Rais, kuiondoa kauli ile kwani kwa kiasi kikubwa italeta usumbufu mkubwa katika mashauri yanayoendelea mahakamani.

Wanasheria wanaweza kutuhumu majaji kua wamefikia maamuzi yao kutokana kua waliahidiwa bilioni miambili na rais , kwahiyo wanafanya hivyo kutimiza malengo yao.

Kama mwananchi wa kawaida na mdau wa sheria, kwakweli kauli ile haikua sahihi. Na inahitajika uamuzi wa busara kabisa ufanyike ili hili jambo liishe vyema kwani kuna kila dalili ya maombi kupelekwa mahakamani ili mashauri yasimamishwe mpaka kauli hiyo itakapofutwa.

Nawasilisha.
 
Kwenye hili watz tuache porojo, hao vigogo waliopewa dhamana ya kuongoza mashurina tahasisi za umma na kufanya ufisadi kama NIDA,TRA na TPA hawajavunja sheria!
Je mnataka JPM magufuli awachekee chekee kama JK alivyowachekea na kuongea kwa lugha nzuri na wezi wa EPA! ?
Watanzania tubadilike, hata huko wanakoheshimu utawala wa sheria na haki za binadamu hawana mzaha na wahujumu uchumi waliwashughulijia ndiyo maana sahz kuna kuheshimu sheria!
Mwacheni Mhe. anyooshe hii nchi na hapa lazima udikteta kidogo uwepo!?
Kama ndio hivyo hakuna umuhimu basi wa kua na mhimili wa mahakama na katiba, utawala wa sheria unaheshimiwa kwa kuheshimu mamlaka za mihimili yote, yaani bunge, mahakama na serikali(executive)
 
Kuna kesi tayari zinazoendelea, kumbuka hilo, na malengo hapa ni kukusanya fedha, na mahakama imeahidiwa bilioni 200, na nyingine kununulia ndege, ukiacha ushabiki, ambao hata mimi pia kama mwana ccm natakiwa kutetea kauli ya rais, na kufikiri kwa kutumia milango yote ya fahamu utaona ninalolisema, pale Rais kashauriwa vibaya, hakutkiwa kuongea vile.
Ulitaka aongee namna gani????? Kitu gani kipya alikisema pale? Tatizo wengi wetu tumezoea kuishi kinafiki (kusifia watawala) na ndo maana umasikini utatuandamaa milele.
 
Kweli wabongo tuna gubu, katika yote aliyoongea umeona umkosoe tu? msifie basi hata kwa mazuri aliyozungumza. Binafsi sijaona kama amewapangia maamuzi majaji naona kama amewapa mkakati wa kazi tu bado maamuzi yatatolewa na majaji na kwa kufata sheria za nchi.Tatizo wapiga dili wengi walizoea ikulu kama kimbilio lao.
Pombe mkurupukaji hajui nini cha kuongea wapi.
Wewe tetea mahaba yako kwake ila ndo ivyo mfalme ana masikio marefu kama ya punda wewe unaogopa kumwambia.
 
Ni swala gumu kulijadili hili na mimi naweza kusema umeliangalia kwa macho mepesi sana.

kumbuka raisi alikuwa amevaa kofia nyingi hivyo kila alilolizungumza ni lazima ujiulize aliliongea kwa kutumia kofia ipi.

zipo tetesi mitaani kuwa serikali huwa haishindi kesi hata moja ya madai bali yenyewe huwa inashindwa tu iwe imepelekwa kama mdaiwa au inadai. yasemekana hili hutokana na rushwa iliyojikita katika mifumo ya kutoa haki na kwa upande wa serikali huwa haitoi rushwa hivyo maamuzi huwa sekita binafsi wanashinda ama kutoa kitu kidogo ili kuepuka kulipa faini kubwa serikalini au kutoa kitu kidogo ili mahakama zetu zihalalishe malipo makubwa kwao kutoka serikalini.

sasa bila kupepesa utaona kuna jipu katika mfumo wa utoaji haki linalohitaji kutumbuliwa. lakini hilo haliko chini ya mamlaka ya mtumbua majibu hivyo alikuwa anajaribu kufanya linalowezekana katika uwezo wake kutumbua jipu lililo katika mfumo wa mahakama. Hapa aliongea kuwaonyesha walioko katika mhimili huo mambo ambayo yanawakwamisha wao kama wadai katika kesi walizowalisilisha na kwa kutambua wajibu wa serikali kufacilitate kifedha mhimili huo ili uendeshe shughuli akatoa ahadi.

kwangu mimi naona hotuba ya raisi ikitoa changamoto kwa wanasheria kumaliza kesi ndani ya mda na kutoa maamuzi ya haki kwa anayestahili na sote tujaribu kuielekeza hotuba yake kutoa msukumo huo.
Well, kama nia ilikua ni kutumbua majipu nadhani hilo angelisema wazi pale kwamba kuna rushwa kwenye judicial system na angewatahadharisha wapenda rushwa kua atadeal nao lakini hili la kutoa ahadi ya bilioni 200 ili trilioni ikusanywe wewe unalionaje mkuu, hiyo imekaaje?
 
Napenda kusema wazi kabisa kua Rais wetu alishauriwa vibaya, na waliomshauri wamemweka katika kikaango na wadau wa sekta ya sheria.

Hii ni kutokana na kauli aliyoitoa jana katika maadhimisho ya siku ya sheria duniani au " Law day" pale aliposema kwamba kuna kesi zaidi ya 400 zilizopo mahakamani ambazo kama zikiendeshwa ipasavyo basi serikali inaweza kujipatia kiasi cha shilingi trilioni moja kama fidia toka wa wadaawa, ambazo ameahidi kuwapatia mahakama kiasi cha shilingi bilioni mbili.
.

Hujaandika kama mwanasheria.Alichosema Raisi ni kuilalamikia mahakama sio kuingilia uhuru wa mahakama.Hata mimi nina malalamiko na mahakama kuna mtu namdai kodi ya nyumba amekaa miaka mitatu bila kulipa kama mahakama ingeiendesha hiyo kesi ipasavyo ningekuwa na hela za kutosha kumlipa wakili wangu ambaye ananidai.

Bunge huwa pia linalalamikia mahakama,serikali kulalamikia mahakama kuna ajabu gani? Hata mimi nina malalamiko kwa mahakama
 
Ni kweli ninao na unatakiwa ujifunze kwangu. soma nilichoandika nidarasa zuri kwako na kwa wengine wasioelewa kama wewe.

Kulingana na hizo sheria unazozielewa ni nani ana mamlaka ya kumhimiza jaji mkuu kama mambo hayaendi sawa kwenye mahakama? or ni untouchable sector? na kwann rais amteu jaji mkuu kama hawezi kumkemea.
 
Kuna kesi tayari zinazoendelea, kumbuka hilo, na malengo hapa ni kukusanya fedha, na mahakama imeahidiwa bilioni 200, na nyingine kununulia ndege, ukiacha ushabiki, ambao hata mimi pia kama mwana ccm natakiwa kutetea kauli ya rais, na kufikiri kwa kutumia milango yote ya fahamu utaona ninalolisema, pale Rais kashauriwa vibaya, hakutkiwa kuongea vile.
Ameingilia uhuru wa mahakama kivipi? Yeye ni Rais wa nchi hawezi kutoa ushauri kweli kwa mihimili mingine? Kama hawezi kutoa ushauri kwa mihimili mingine kama Bunge na Mahakama nini maana yakuwa Rais! Hiyo miimili mingine ijifanyie mambo kivyake kwasababu wana uhuru wa kutoingiliwa? Hii itakuwa nchi au janga!
 
Napenda kusema wazi kabisa kua Rais wetu alishauriwa vibaya, na waliomshauri wamemweka katika kikaango na wadau wa sekta ya sheria.

Hii ni kutokana na kauli aliyoitoa jana katika maadhimisho ya siku ya sheria duniani au " Law day" pale aliposema kwamba kuna kesi zaidi ya 400 zilizopo mahakamani ambazo kama zikiendeshwa ipasavyo basi serikali inaweza kujipatia kiasi cha shilingi trilioni moja kama fidia toka wa wadaawa, ambazo ameahidi kuwapatia mahakama kiasi cha shilingi bilioni mbili.

Kuna mambo machache ya kuangalia hapa ;

1. Ni hakimu gani au jaji atakayekua tayari kutoa hukumu dhidi ya serikali.

2. Ni wakili gani anapoteza muda wake kwenda mahakamani wakati anajua kua mteja wake anakwenda kushindwa.

3. Vipi kuhusiana na uhuru wa mahakama kufanya kazi yake bila kuingiliwa.

4. Vipi kuhusiana na haki ya mtuhumiwa kuwa hana hatia mpaka pale mahakama itakapomtia hatiani.

5. Ina maana serikali itashinda kesi zote 400??

Napenda nikumbushe kwamba mashauri yakishafikishwa mahakamani mambo hua yanaendeshwa kwa taratibu, kanuni na sheria ambazo tayari zipo, hayaendeshwi kwa kauli za kisiasa, huko ni kuingilia uhuru wa mahakama.

Kauli ya Rais ukiitazama kwa kina utaona kwamba imevunja ibara ywa 13 (6) (a) na 107B ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , 1977, nanukuu;

Equality before the law 13.-(1) All persons are equal before the law and are entitled, without any discrimination, to protection and equality before the law.

(6) To ensure equality before the law, the state authority shall make procedures which are appropriate or which take into account the following principles, namely: (a) when the rights and duties of any person are being determined by the court or any other agency, that person shall be entitled to a fair hearing and to the right of appeal or other legal remedy against the decision of the court or of the other agency concerned;

Independence of the Judiciary 107B. In exercising the powers of dispensing justice, all courts shall have freedom and shall be required only to observe the provisions of the Constitution and those of the laws of the land.

Ukipitia ibara zote mbili, utaona kwamba kwa kauli ya Rais, majaji na mahakimu hawatakua katika hali ya uhuru wa kufanya kazi zao kwani hawatataka kwenda kinyume na maagizo ya rais ambayo yanaelekeza makusanyo ya trilioni moja.

Vile vile haki ya wadaiwa itakua imevunjwa maana mpaka sasa wanachukuliwa kua tayari ni wakosaji wakati mashauri bado hayajamalizika na mahakama kufikia maamuzi yake.

Jambo la msingi kabisa la kufanyika hapa ni kwa Rais, kuiondoa kauli ile kwani kwa kiasi kikubwa italeta usumbufu mkubwa katika mashauri yanayoendelea mahakamani.

Wanasheria wanaweza kutuhumu majaji kua wamefikia maamuzi yao kutokana kua waliahidiwa bilioni miambili na rais , kwahiyo wanafanya hivyo kutimiza malengo yao.

Kama mwananchi wa kawaida na mdau wa sheria, kwakweli kauli ile haikua sahihi. Na inahitajika uamuzi wa busara kabisa ufanyike ili hili jambo liishe vyema kwani kuna kila dalili ya maombi kupelekwa mahakamani ili mashauri yasimamishwe mpaka kauli hiyo itakapofutwa.

Nawasilisha.
mkuu si kuna kitu kinaitwaga check and balance au
 
Kama ndio hivyo hakuna umuhimu basi wa kua na mhimili wa mahakama na katiba, utawala wa sheria unaheshimiwa kwa kuheshimu mamlaka za mihimili yote, yaani bunge, mahakama na serikali(executive)
Na kama ulimsikiliza kwa makini alikuwa anamuomba sana Mhe.Jaji mkuu amsaidie kwy eneo la kuamua kesi zinazokwenda mahakamani,yupo sahihi hata kama hukupenda uchaguzi wake wa maneno aliyoyatumka kuwasilisha ujumbe kwa CJ&DPP.
tumuunge mkono, tutafika tu nchi ya ahadi!
 
Back
Top Bottom