Emmamkolomi
JF-Expert Member
- Sep 21, 2013
- 628
- 209
Kwa bahati nzuri nilipata bahati kuisikiliza hotuba nzima ya Rais siku ya sheria. Si baada ya hotuba ile tu ambapo Rais amekuwa akilaumiwa. MImi sioni ajabu kwanza ningeshangaa sana kama Rais angepongezwa na watu wote kutokana na jinsi anavyotekeleza majukumu yake. Tatizo ni hii OTM (oparesheni tumbua majipu). Kuna watu wengi sana walikuwa wakinufaika na wizi na ufisadi mkubwa uliokuwa ukiendelea nchini kwetu.
Hawa watu wana ndugu zao ambao wote wameathirika, mtu angefanya kosa kubwa kufikiria kwamba wale wote kwa uwingi wao ambao kwa namna moja au nyingine wameguswa na OTM watashangilia, Na bado kilio kitaendelea kwa sababu Rais anaonekana bado anaendelea na oparesheni yake. Mpaka sasa kwa sehemu kubwa amegusa sehemu ndogo sana ya nchi hii yaani TRA na Bandari. Ukiangalia unaona wazi kabisa kwamba nchii hii ilifika mahali pabaya na kwamba yaelekea hakuna taasisi iliyo salama, na Magufuli kote huko atakuja just a matter of time kwa hiyo kilio cha wezi wa fedha za serikali, mafisadi na wala rushwa kitaendelea na wajiandae popote walipo kwani hakika atawafikia. Kibaya zaidi ataunda mahakama yao. Na wale wanaosema Rais anaingilia mhimili mwingine waendelee tu kupiga kelele. lakini habari ndo hiyo OPARESHENI TUMBUA MAJIPU INAENDELEA na kila aliye sehemu ya jipu hakika itamfikia.