Getrude Mollel
JF-Expert Member
- Apr 26, 2022
- 270
- 362
Katika Qatar Economic Forum, moja kati ya wazungumzaji alikuwepo Mo Dewji, tajiri namba moja Tanzania na mbali ya hayo, ni moja kati ya hayo ni mtu ambaye amewekeza sana Tanzania na kutoa maelfu ya ajira kwa watanzania. Katika mazungumzo yake, alitoa kauli nzito sana na nzuri ambayo kama ni mtu wa kutazama kwa jicho la mbali, utaona kali hii ni mtaji mkubwa kwa Tanzania hasa katika kuleta uwekezaji zaidi Tanzania. Nanukuu.
"Now we have a new President, she a woman, a very very vibrant, she's doing a fantastic job, she's moving around the whole world. So-called the 'Royal Tour', we can already see the impact in terms of a huge influx of tourists bringing foreign revenues and a lot of investments coming into the country I think she's doing a fantastic job and Tanzania is ready to fly."
Kauli hii ukiisikiliza vizuri utajua tu hapa Mo amefanya jambo kubwa sana kwa Taifa lake. Sasa basi kwa nini narejelea kusema kwamba kauli ya Mo ni mtaji mkubwa sana kwa Taifa la Tanzania?
Kauli ya Mo itarejesha imani ya wawekezaji wenye mitaji mikubwa. Miaka kadha nyuma wakati wa JPM, kutokana na aina ya uongozi wake, imani ya wawekezaji ilishuka sana.
Hata kama wawekezaji walifika nchini, lakini waliwekeza fedha zao kwa woga sana kutokana na kutoeleweka kwa Serikali ya JPM aliyokuwa na maamuzi ya kushutukiza ambayo wawekezaji waliohofia pengine wangeteketeza mitaji yao. Kwa kauli ya Mo, kutokana na nafasi yake nchini Tanzania na fedha alizowekeza, ni wazi kwamba wawekezaji wa aina yake ambao Tanzania inawahitaji sana, wanaweza kuja Tanzania, kuwekeza na kuleta ajira zaidi kwa Watanzania.
Tujiulize, wakati wa Magufuli ambao Mo mwenyewe alitekwa kwa wiki kadhaa hata tusijue alikuwa wapi, mbona hakuwahi kusema popote pale kama eti, Magufuli ni Rais mzuri sana na kumpa sifa kedekede? Mnadhani Mo na ukubwa wake huko nje, na jopo la watu mashuhuri wanaojuana naye, mnadhani walifurahi yeye kupotezwa? Acha hiyo, vipi kuhusu imani zao juu ya kuja kuwekeza Tanzania, nchi ambayo mtu aina ya Mo, a million dollars rich anapotea tu kama Kuku.
Matajiri aina ya Mo wanalindwa Duniani kote. Mo ni mtu muhimu sana. Ameajiri zaidi ya watu 40,000 hapa Tanzania. Imagine afunge viwanda vyake vyote hao watu 40K Serikali itawabeba kwa mbeleko gani, kama sio kuongezeka tu kwa uhalifu. Tuseme tu Mo kwa sasa ana amani na furaha kuliko wakati wowote ule. Hiyo tu, inatosha sana kuonesha Dunia sasa Tanzania ni nchi ya aina gani, na hii ni faida kwetu kwani italeta wawekezaji zaidi na kutanua fursa za kibiashara Tanzania.
Ni wazi, hii isingewekezana bila uongozi thabiti na wenye maarifa wa Rais Samia Suluhu Hassan.