Kauli ya Lissu ya Rais Mzanzibar ni matokeo ya kufumba masikio Tanganyika kuwa na Serikali yake na viongozi wake watakaoamua mambo yao, asilaumiwe!

Synthesizer

Platinum Member
Feb 15, 2010
12,147
21,165
Kwanza niombe moderators muiache hii thread ijitegemee, inaenda mbali zaidi ya kauli ya Lissu.

Kama una akili timamu na za kutosha, utakuwa umegundua kwamba suala la kusema kero za muungano zinatatuliwa limekuwa ni suala la kuzidi kuipa Zanzibar mamlaka yake kama nchi kamili na kuiondoa kwenye mambo yanayohusu muungano. Hii inatia ndani kuwapa zaidi nafasi waZanzibar kufanya kazi upande wa bara, si katika taasisi za muungano tu, bali hata maeneo ambayo sio ya muungano. Na tunajua ukweli suala hili limekua kubwa sana kipindi hiki cha Raisi Samia.

Sasa nyie watu mnaojiita viongozi wetu mkidhani kwamba watu wa bara hawaoni hili, basi mnajidanganya. In fact viongozi wa bara mnaoshupalia kumlaumu Lissu kwa kauli yake mnaonekana kama wasaliti wa Tanganyika, traitors. Kila mtu wa bara kwa sasa anaona ukweli kwamba katika suala la Muungano, Zanzibar ina mamlaka kamili kama nchi japo kuna kidanganyio cha muungano, wakati rasirimali za bara zinazidi kuibeba Zanzibar kila siku kwa kisingizio cha muungano. Zanzibar walipohisi kuna mafuta visiwani waliamua mafuta yaondolewe kwenye muungano. Mnafikiri watu wa bara hawaoni haya?

Angalia suala la umeme. Kimsingi, Zanzibar hawataki kulipia umeme. Wanakopa umeme wa Tanesco, deni linafikia mabilioni, wakiambiwa walipe wanakuja juu. Tanesco wanakatazwa kuwakatia umeme au hata kuwadai, wanaambiwa ni suala linashughulikiwa huko juu. Matokeo ni kwamba watumiaji wa umeme bara inabidi watozwe bei kubwa ya umeme ili kufidia umeme ambao Zanzibar wanatumia lakini kama serikali hawataki kuulipia! Hata wewe msomaji wa bara unalipia bili yako ya umeme kwa kuchangia kuwapa Zanzibar umeme wa bure! Sasa wao kulipia umeme hiyo nayo ni kero ya muungano?

Mfano mwingine. Zanzibar wanaruhusiwa kumiliki ardhi bara, lakini watu wa bara hawawezi kumiliki ardhi Zanzibar kwa kisingizio Zanzibar ni kisiwa kidogo. Sasa kama ni kisiwa kidogo, si ndio maana Wa Zanzibar wanaruhusiwa kuhamia bara? Ingekuwa sawa kusema ni kisiwa kidogo kama Wazanzibar wasingeruhusiwa kumiliki ardhi upande wa bara. Sasa unaruhusu waje bara kupunguza pressure ya population kule, lakini unasema watu wa bara msinunue ardhi Zanzibar. Unawahadaa nani kwa kisingizio hiki, watu wa bara? Kwa sababu tunajua sababu ya kuwanyima watu wa bara kununua ardhi Zanzibar sio upungufu wa ardhi. Kama ardhi ya kununua haipo basi haitawezekana kununua, na watu watajipatia ardhi bara. Sio rahisi kununua ardhi Moshi kwa sababu hakuna ardhi ya kununua, sasa leo utasema Wasukuma wasinunue ardhi Moshi kwa sababu Moshi kuna upungufu wa ardhi kwa ajili ya Wachaga, una akili sawasawa wewe?

Zanzibar sasa imekuwa ikifanya kitu kinaitwa "cherry picking" kuamua nini kiwe katika muungano, na inaonyesha wazi kwamba katika suala la wao kufanya hivyo, watu wa bara hawatakiwi kupinga lolote. Na tunajua kwamba kwa sasa Zanzibar wanatumia nafasi ya uwepo wa Rais Samia kwenye kiti cha Uraisi kama nafasi pekee ya kuvutia mambo mengi upande wao. Hilo sio siri.

Zanzibar wamejisahau sana katika kuvutia upande wao hadi imefikia watu wachache wameanza kudokeza kwamba suala la watu wa bara kwenda Zanzibar kwa passport lirudishwe! Ni wazi mapendekezo kama hayo ya kipumbavu yasingetokea katika kipindi cha raisi mwingine, bali kunakuwa na ujasiri wa kuyatoa chini ya Raisi Samia.

Sasa kumlaumu Tundu Lissu kwa kauli aliyotoa juu ya Raisi wa Zanzibar kufukuza Wamasai ni kumwonea. Tundu Lissu alichofanya ni kueleza hisia za Watanzania bara wenye akili timamu karibu wote. Ni wale tu ambao hawana uwezo wa kufikiri ulio sawa watapingana na Lissu, na sio kwa sababu kuna tatizo katika kauli ya Lissu, bali kwa sababu nafasi walizonazo katika uongozi wa serikali zinawataka wamkosoe Lissu. Ndani ya mioyo ya hawa watu wanajua Tundu Lissu anaongea ukweli.

Sasa, onyo langu kwa serikali ni kwamba inabidi iwe makini sana na suala hili la muungano. Hata Raisi Samia mwenyewe, japo ni raisi wa Tanzania, hapaswi kujisahau kwamba yeye ni Mzanzibar, na yapo mambo ambayo ni afadhali asiyafanyie uamuzi kwa sababu yana "political sensitivity" katika context ya kwamba yeye ni Mzanzibar. Hii ni pamoja na uamuzi ambao binafsi naona haukuwa wa busara wa mkataba wa bandari za bara, ajira za Wazanzibar upande wa bara, teuzi zake nk. Raisi Samia aliamua kupambana na watu wa bara katika hili, akijua yeye na Waziri wa Miundombinu, wenye maamuzi makubwa juu ya huu mkataba, walikuwa Wazanzibar. Hilo lilikuwa kosa (political blunder) hata kama mkataba unaweza uwe na manufaa.

Kuna maamuzi ambayo Raisi Samia anapaswa kutumia busara ya kuyaacha hadi raisi kutoka bara aje awe madarakani na ayashughulikie, pamoja na mikataba yenye impact kubwa upande wa bara. Raisi Samia, kama atatumia busara, atakuwa mwangalifu sana katika kufanya maamuzi ambayo yanaathiri watu wa bara na sio watu wa Zanzibar, japo yanafanyika katika kivuli cha muungano. Kama hatafanya hivyo, basi aelewe wazi kwamba vyama kama Chadema watatumia maamuzi hayo ili kujaribu kumwondoa madarakani, na watanzania bara wote wenye akili wanapaswa kuwaunga mkono. Raisi Samia asisahau kwamba ni Watanzania bara wanaomuweka raisi madarakani kwa sababu ya wingi wao. Lissu anajua hilo, na Chadema watakuwa hawajaiva kisiasa kama hawatalitumia hilo katika njia yenye akili kujaribu kuiondoa CCM madarakani.

Pia soma
 
Kwanza niombe moderators muiache hii thread ijitegemee, inaenda mbali zaidi ya kauli ya Lissu.

Kama una akili timamu na za kutosha, utakuwa umegundua kwamba suala la kusema kero za muungano zinatatuliwa limekuwa ni suala la kuzidi kuipa Zanzibar mamlaka yake kama nchi kamili na kuiondoa kwenye mambo yanayohusu muungano. Hii inatia ndani kuwapa zaidi nafasi zaidi waZanzibar kufanya kazi upande wa bara, si katika taasisi za muungano tu, bali hata maeneo ambayo sio ya muungano. Na tunajua ukweli suala hili limekua kubwa sana kipindi hiki cha Raisi Samia.

Sasa nyie watu mnaojiita viongozi wetu mkidhani kwamba watu wa bara hawaoni hili, basi mnajidanganya. In fact viongozi wa bara mnaoshupalia kumlaumu Lissu kwa kauli yake mnaonekana kama wasaliti wa Tanganyika, traitors. Kila mtu wa bara kwa sasa anaona ukweli kwamba katika suala la Muungano, Zanzibar ina mamlaka kamili kama nchi japo kuna kidanganyio cha muungano, wakati rasirimali za bara zinazidi kuibeba Zanzibar kila siku kwa kisingizio cha muungano. Zanzibar walipohisi kuna mafuta visiwani waliamua mafuta yaondolewe kwenye muungano. Mnafikiri watu wa bara hawaoni haya?

Kwa mfano, Zanzibar wanaruhusiwa kumiliki ardhi bara, lakini watu wa bara hawawezi kumiliki ardhi Zanzibar kwa kisingizio Zanzibar ni kisiwa kidogo. Sasa kama ni kisiwa kidogo, si ndio maana Wa Zanzibar wanaruhusiwa kuhamia bara? Ingekuwa sawa kusema ni kisiwa kidogo kama Wazanzibar wasingeruhusiwa kumiliki ardhi upande wa bara. Sasa unaruhusu waje bara kupunguza pressure ya population kule, lakini unasema watu wa bara msinunue ardhi Zanzibar. Unawahadaa nani kwa kisingizio hiki, watu wa bara? Kwa sababu tunajua sababu ya kuwanyima watu wa bara kununua ardhi Zanzibar sio upungufu wa ardhi. Kama ardhi ya kununua haipo basi haitawezekana kununua, na watu watajipatia ardhi bara. Sio rahisi kununua ardhi Moshi kwa sababu hakuna ardhi ya kununua, sasa leo utasema Wasukuma wasinunue ardhi Moshi kwa sababu Moshi kuna upungufu wa ardhi kwa ajili ya Wachaga, una akili sawasawa wewe?

Zanzibar sasa imekuwa ikifanya kitu kinaitwa "cherry picking" kuamua nini kiwe katika muungano, na inaonyesha wazi kwamba katika suala la wao kufanya hivyo, watu wa bara hawatakiwi kupinga lolote. Na tunajua kwamba kwa sasa Zanzibar wanatumia nafasi ya uwepo wa Rais Samia kwenye kiti cha Uraisi kama nafasi pekee ya kuvutia mambo mengi upande wao. Hilo sio siri.

Zanzibar wamejisahau sana katika kuvutia upande wao hadi imefikia watu wachache wameanza kudokeza kwamba suala la watu wa bara kwenda Zanzibar kwa passport lirudishwe! Ni wazi mapendekezo kama hayo ya kipumbavu yasingetokea katika kipindi cha raisi mwingine, bali kunakuwa na ujasiri wa kuyatoa chini ya Raisi Samia.

Sasa kumlaumu Tundu Lissu kwa kauli aliyotoa juu ya Raisi wa Zanzibar kufukuza Wamasai ni kumwonea. Tundu Lissu alichofanya ni kueleza hisia za Watanzania bara wenye akii timamu karibu wote. Ni wale tu ambao hawana uwezo wa kufikiri ulio sawa watapingana na Lissu, na sio kwa sababu kuna tatizo katika kauli ya Lissu, bali kwa sababu nafasi walizonazo katika uongozi wa serikali zinawataka wamkosoe Lissu. Ndani ya mioyo ya hawa watu wanajua Tundu Lissu anaongea ukweli.

Sasa, onyo langu kwa serikali ni kwamba inabidi iwe makini sana na suala hili la muungano. Hata Raisi Samia mwenyewe, japo ni raisi wa Tanzania, hapaswi kujisahau kwamba yeye ni Mzanzibar, na yapo mambo ambayo ni afadhali asiyafanyie uamuzi kwa sababu yana "political sensitivity" katika context ya kwamba yeye ni Mzanzibar. Hii ni pamoja na uamuzi ambao binafsi naona haukuwa wa busara wa mkataba wa bandari za bara, ajira za Wazanzibar upande wa bara, teuzi zake nk. Raisi Samia aliamua kupambana na watu wa bara katika hili, akijua yeye na Waziri wa Miundombinu, wenye maamuzi makubwa juu ya huu mkataba, walikuwa Wazanzibar. Hilo lilikuwa kosa (political blunder) hata kama mkataba unaweza uwe na manufaa.

Kuna maamuzi ambayo Raisi Samia anapaswa kutumia busara ya kuyaacha hadi raisi kutoka bara aje awe madarakani na ayashuhulikie, pamoja na mikataba yenye impact kubwa upande wa bara. Raisi Samia, kama atatumia busara, atakuwa mwangalifu sana katika kufanya maamuzi ambayo yanaathiri watu wa bara na sio watu wa Zanzibar, japo yanafanyika katika kivuli cha muungano. Kama hatafanya hivyo, basi aelewe wazi kwamba vyama kama Chadema watatumia maamuzi hayo ili kujaribu kumwondoa madarakani. Asisahau kwamba ni Watanzania bara wanaomuweka raisi madarakani kwa sababu ya wingi wao. Lissu anajua hilo, na Chadema hawatakuwa hawajaiva kisiasa kama hawatalitumia hilo katika njia yenye akili kujaribu kuiondoa CCM madarakani.

Pia soma
Ujumbe mzito huu
 
Kila marais wakitokea upande wa Zanzibar wanafanya maamuzi ya kuiumiza Tanganyika.
Sijawahi sikia rais Mtanganyika katoa ardhi ya Zanzibar kwa wawekezaji au kauza bandari au rasilimali yoyote kubwa ya Zanzibar kwa wageni.

Samia anafanya makosa makubwa sana
 
Kwani Rais wa muungano Ana mamlaka ya mambo yasio ya muungano upande wa Zanzibar,? Pole sana
 
Huu ndiyo udhaifu wenyewe wa Muungano. Aidha huu muungano uwe wa Serikali 3 ili kila mtu awe na maamuzi na mambo yake au Serikali moja au uvunjwe kabisa maana ni full unafiki kwa hali ilivyo sasa.

Unashangaa unaenda Wilaya za ndani ndani huko unakuta kuna watumishi Wazanzibar unajiuliza hivi mjini Magharibi unaweza kukuta Afisa Afya Mtanganyika?
 
Kila marais wakitokea upande wa Zanzibar wanafanya maamuzi ya kuiumiza Tanganyika.
Sijawahi sikia rais Mtanganyika katoa ardhi ya Zanzibar kwa wawekezaji au kauza bandari au rasilimali yoyote kubwa ya Zanzibar kwa wageni.

Samia anafanya makosa makubwa sana
marais wa zanzibar ni wangapi? Ali Hassan Mwinyi ni wa kwenu, na yeye mwenyewe alifafanua kwenye kitabu chake. Alikwenda Zanzibar kwa ajili ya kupata elimu akabakia kule, sasa tena hao marais wako wapi? Miaka 57 mumetutawala, bado tu munalalamika na hiyo mitatu ya Samia?
 
Huu Ndio ukweli mchungu..! Juzi Fatma Karume kutuambia Watanganyika hatujitambui!
 
Kwanza niombe moderators muiache hii thread ijitegemee, inaenda mbali zaidi ya kauli ya Lissu.

Kama una akili timamu na za kutosha, utakuwa umegundua kwamba suala la kusema kero za muungano zinatatuliwa limekuwa ni suala la kuzidi kuipa Zanzibar mamlaka yake kama nchi kamili na kuiondoa kwenye mambo yanayohusu muungano. Hii inatia ndani kuwapa zaidi nafasi waZanzibar kufanya kazi upande wa bara, si katika taasisi za muungano tu, bali hata maeneo ambayo sio ya muungano. Na tunajua ukweli suala hili limekua kubwa sana kipindi hiki cha Raisi Samia.

Sasa nyie watu mnaojiita viongozi wetu mkidhani kwamba watu wa bara hawaoni hili, basi mnajidanganya. In fact viongozi wa bara mnaoshupalia kumlaumu Lissu kwa kauli yake mnaonekana kama wasaliti wa Tanganyika, traitors. Kila mtu wa bara kwa sasa anaona ukweli kwamba katika suala la Muungano, Zanzibar ina mamlaka kamili kama nchi japo kuna kidanganyio cha muungano, wakati rasirimali za bara zinazidi kuibeba Zanzibar kila siku kwa kisingizio cha muungano. Zanzibar walipohisi kuna mafuta visiwani waliamua mafuta yaondolewe kwenye muungano. Mnafikiri watu wa bara hawaoni haya?

Kwa mfano, Zanzibar wanaruhusiwa kumiliki ardhi bara, lakini watu wa bara hawawezi kumiliki ardhi Zanzibar kwa kisingizio Zanzibar ni kisiwa kidogo. Sasa kama ni kisiwa kidogo, si ndio maana Wa Zanzibar wanaruhusiwa kuhamia bara? Ingekuwa sawa kusema ni kisiwa kidogo kama Wazanzibar wasingeruhusiwa kumiliki ardhi upande wa bara. Sasa unaruhusu waje bara kupunguza pressure ya population kule, lakini unasema watu wa bara msinunue ardhi Zanzibar. Unawahadaa nani kwa kisingizio hiki, watu wa bara? Kwa sababu tunajua sababu ya kuwanyima watu wa bara kununua ardhi Zanzibar sio upungufu wa ardhi. Kama ardhi ya kununua haipo basi haitawezekana kununua, na watu watajipatia ardhi bara. Sio rahisi kununua ardhi Moshi kwa sababu hakuna ardhi ya kununua, sasa leo utasema Wasukuma wasinunue ardhi Moshi kwa sababu Moshi kuna upungufu wa ardhi kwa ajili ya Wachaga, una akili sawasawa wewe?

Zanzibar sasa imekuwa ikifanya kitu kinaitwa "cherry picking" kuamua nini kiwe katika muungano, na inaonyesha wazi kwamba katika suala la wao kufanya hivyo, watu wa bara hawatakiwi kupinga lolote. Na tunajua kwamba kwa sasa Zanzibar wanatumia nafasi ya uwepo wa Rais Samia kwenye kiti cha Uraisi kama nafasi pekee ya kuvutia mambo mengi upande wao. Hilo sio siri.

Zanzibar wamejisahau sana katika kuvutia upande wao hadi imefikia watu wachache wameanza kudokeza kwamba suala la watu wa bara kwenda Zanzibar kwa passport lirudishwe! Ni wazi mapendekezo kama hayo ya kipumbavu yasingetokea katika kipindi cha raisi mwingine, bali kunakuwa na ujasiri wa kuyatoa chini ya Raisi Samia.

Sasa kumlaumu Tundu Lissu kwa kauli aliyotoa juu ya Raisi wa Zanzibar kufukuza Wamasai ni kumwonea. Tundu Lissu alichofanya ni kueleza hisia za Watanzania bara wenye akili timamu karibu wote. Ni wale tu ambao hawana uwezo wa kufikiri ulio sawa watapingana na Lissu, na sio kwa sababu kuna tatizo katika kauli ya Lissu, bali kwa sababu nafasi walizonazo katika uongozi wa serikali zinawataka wamkosoe Lissu. Ndani ya mioyo ya hawa watu wanajua Tundu Lissu anaongea ukweli.

Sasa, onyo langu kwa serikali ni kwamba inabidi iwe makini sana na suala hili la muungano. Hata Raisi Samia mwenyewe, japo ni raisi wa Tanzania, hapaswi kujisahau kwamba yeye ni Mzanzibar, na yapo mambo ambayo ni afadhali asiyafanyie uamuzi kwa sababu yana "political sensitivity" katika context ya kwamba yeye ni Mzanzibar. Hii ni pamoja na uamuzi ambao binafsi naona haukuwa wa busara wa mkataba wa bandari za bara, ajira za Wazanzibar upande wa bara, teuzi zake nk. Raisi Samia aliamua kupambana na watu wa bara katika hili, akijua yeye na Waziri wa Miundombinu, wenye maamuzi makubwa juu ya huu mkataba, walikuwa Wazanzibar. Hilo lilikuwa kosa (political blunder) hata kama mkataba unaweza uwe na manufaa.

Kuna maamuzi ambayo Raisi Samia anapaswa kutumia busara ya kuyaacha hadi raisi kutoka bara aje awe madarakani na ayashughulikie, pamoja na mikataba yenye impact kubwa upande wa bara. Raisi Samia, kama atatumia busara, atakuwa mwangalifu sana katika kufanya maamuzi ambayo yanaathiri watu wa bara na sio watu wa Zanzibar, japo yanafanyika katika kivuli cha muungano. Kama hatafanya hivyo, basi aelewe wazi kwamba vyama kama Chadema watatumia maamuzi hayo ili kujaribu kumwondoa madarakani. Asisahau kwamba ni Watanzania bara wanaomuweka raisi madarakani kwa sababu ya wingi wao. Lissu anajua hilo, na Chadema hawatakuwa hawajaiva kisiasa kama hawatalitumia hilo katika njia yenye akili kujaribu kuiondoa CCM madarakani.

Pia soma

WELL SAID ......!!
 
wazanzibar wametuchezea na kudeka kwa miaka mingi sana. ifike mahali tumwage tu mboga na ugali.
 
Back
Top Bottom