Leak
JF-Expert Member
- Feb 22, 2012
- 52,854
- 43,354
MBUNGE AACHIE JIMBO!
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimemtaka Mbunge wa Mbongwe, Nicodemus Maganga kama anataka kuhudumia wananchi afuate utaratibu wa nchi na akitaka kulipwa kwa dola ahamie katika nchi zinazofanya hivyo.
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo aliopohijiwa na gazeti la Nipashe
Kwa upande wake kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe alipoulizwa na Nipashe kuhusu suala hilo alisema
Kama maslahi hayatoshi aache kazi ya Ubunge.
"Wabunge wasipoogopa wananchi hawatakuwa wabunge, Wakati Rais anawaambia wafanyakazi hawawezi kupandishia mishahara kwa sababu ya hali ya uchumi, Mbunge anataka malipo zaidi ni hujuma kwa Rais"
Maoni yangu:
Kwanza kabisa niseme wazi kabisa Mimi nilipata wasaha wa kumsikiliza vizuri mbunge aliyesema wazi kuwa mishahara yao wabunge haiwatoshi na alieleza vizuri kabisa kwanini aseme hayo, na mimi nilitarajia kabisa haya ni maoni yake binafsi na anao uhuru wa kutoa maoni yake akiwa bungeni na kama ni hukumu basi sisi wananchi ndio tunajua chakufanya.
Kwenye hili kumekuwa na unafiki mwingi sana na wengi watajidai kuwa hawaungi mkono hoja ya Maganga lakini ukweli ni kwamba wabunge wote kwenye mioyo yao wanaunga mkono hoja lakini wanaogopa wananchi kuusema ukweli. Ukimsikiliza Maganga akijieleza vyema utamuelewa kuwa wabunge wanao mzigo mkubwa sana pamoja na mshahara huo unaotajwa.
Nimeshangazwa na Katibu mkuu bwana Chongolo kumtishia mbunge anayetoa maoni yake na kusema kama hataki aachie ubunge hii ni kinyume kabisa na haki za bunge na mbunge na pia uhuru wa maoni.
Kama kweli tunajali wananchi na wewe ni katibu mkuu tunaomba ukishauri chama na serikali mishahara ya wabunge na viongozi wote ianze kukatwa kodi kama wafanya kazi wengine na wananchi wengine.
Ukweli ni kwamba wabunge na viongozi wakubwa mishahara yao haikatwi kodi kwa hiyo wanakula tuu mishahara kama ilivyo na hii hoja ya mbunge Maganga iwe chachu ya kubadilisha sheria zetu na kuishauri serikali kubadili sheria ili kila mtu alipe kodi sio kuwahamisha wananchi kulipa kodi huku wengine tena kundi kubwa lenye kipato kikubwa halilipi kodi.
Kwako katibu mkuu Chongolo.