Katavi: Kiwanda cha Maziwa chafungwa baada ya uhaba wa mali ghafi ya maziwa

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,884
12,133
Licha ya Serikali kuhamasisha uanzishwaji wa viwanda nchini lakini bado upatikanaji wa mali ghafi za kuendesha baadhi ya viwanda ni changamoto.

Kiwanda cha maziwa cha MMS kilichopo Halmashauri ya Nsimbo mkoani Katavi kimefungwa na mmiliki wa kiwanda hicho.

Kiwanda hicho kilichozinduliwa Disemba 2022 na Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassimu Majaliwa kimefikia hatua ya kufungwa na mmiliki wa kiwanda hicho, Maliki Said ikiwa ni baada ya uhaba wa maziwa ya kuendesha kiwanda hicho.

Daniel Walakunga ambaye ni Afisa Mifugo w Halmashauri ya Nsimbo amesema ushindani wa bei ya maziwa imekuwa changamoto katika kiwanda hicho huku Nehemia James ambaye ni Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uwekezaji amesisitiza wafugaji kufuga ng' ombe kisasa zaidi ili kukidhi upatikanaji wa maziwa na soko kwa ujumla.

Mkuu wa Nkoa wa Katavi, Mwanamvua Mrindoko ametoa agizo la watumishi wanaohusika na idara za ufugaji, uchimi na uwekezaji kumaa pamoja ili kuona namna bora ya kutatua changamoto hiyo ya uhaba wa maziwa katika kiwanda hicho.
 
Back
Top Bottom