Kariakoo: Polisi wafanikiwa kuwaua majambazi wanne baada ya majibizano ya risasi

Huyo mama vipi hali yake?Kariakoo usiku huwa kunanogaaa
Nimeona kuna taarifa zinasambaa huko Instagram kwamba kuna majambazi yalitaka kupora ktk mtaa wa Livingston Kariakoo bahati mzuri polisi wamewahi ktk eneo la tukio. Taarifa zinasema kulikuwa na majibizano ya risasi. Na kunaonekana picha za watu wakiwa wamepigwa risasi wapo chini kama watatu hivi.

Je, Kuna mtu anayejua lolote aje atutosheleze hapa?

---Updates---
Maeneo ya kwa Bakhresa Kariakoo usiku huu wameuawa majambazi wanne mtaa wa Livingstone na Aggrey karibu na mtaa wa Lumumba Mnazi Mmoja. Kuna mama mwenye mimba ambaye alienda kununua mikate kapigwa risasi mbili.

Tukio limetokea mida ya saa nne kasoro usiku huu.

57c93a63373eb12ceeabfeef83cd7071.jpg
2793a0407e589ed17c11754c542bf547.jpg
c3850957c8bf3f0353fe109986d9be0a.jpg
 
Huyo mama vipi hali yake?Kariakoo usiku huwa kunanogaaa
Umeona ukitaka kuifaidi kariakoo usiku haswa pale njia panda uhuru na msimbazi kuna vituko kila siku kungekuwa na waandishi wa habari wangefaidi sana... kila aina ya kituko
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Ushaambiwa kuna mwanamke mwenye mimba kapigwa risasi .....uwe unasoma uzi vizuri

Ova

Eeeeeeeeeeeeeeeh

Wewe ndio ungetumia akili yako kujua ameandika neno update kwenye post yake... amemaanisha nini

Jisikitikie kabisaaaa na jicheke.... ndio kupenda kudakia bila kutumia fikra kama viongozi wenu wadaku...hamna jipya.
 
Umeona ukitaka kuifaidi kariakoo usiku haswa pale njia panda uhuru na msimbazi kuna vituko kila siku kungekuwa na waandishi wa habari wangefaidi sana... kila aina ya kituko
Kariakoo usiku tamu sana Duduwasha na alfajiri ukipita Msimbazi Building unawakuta wanasimba wanabishana mambo ya soka tu, unajiuliza hawa wamelala saa ngapi?Mie nshawaah kuwepo kariakoo saa 8 usiku, daladala zinaita abiria kama mchana na nauli ya mchana
 
Kweli kuna tukio la ujambazi ambalo halikufanikiwa na majambazi watatu wa kiume na mwanamke mmoja wameuwawa katika majibizano ya kurushiana risasi na Polisi. Tukio hilo limetokea Mtaa wa livingstone na Aggrey kwenye duka maarufu kwa Bakhresa usiku huu wa leo majira ya saa mbili plus. Picha zitafuata baadae zilizopo si nzuri kuziweka hapa.
Weka tu, jf wote ni watu wazima, hakuna mtoto amabae hajawi ona mtu kapigwa risasi
 
Kariakoo usiku tamu sana Duduwasha na alfajiri ukipita Msimbazi Building unawakuta wanasimba wanabishana mambo ya soka tu, unajiuliza hawa wamelala saa ngapi?Mie nshawaah kuwepo kariakoo saa 8 usiku, daladala zinaita abiria kama mchana na nauli ya mchana
Yah daladala saa tisa tu ndio zinasimama saa kumi zinaamka.. Kuna vitimbi mno kila day za ulevi ugomvi, Fujo ajari wagambo wakamata pikipiki, polisi wakifukuzana na watu n.k yaani balaa tu
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Yah daladala saa tisa tu ndio zinasimama saa kumi zinaamka.. Kuna vitimbi mno kila day za ulevi ugomvi, Fujo ajari wagambo wakamata pikipiki, polisi wakifukuzana na watu n.k yaani balaa tu
Kuna watu nawafahamu maisha yao yooote kariakoo.Ukweli serikali ikiimarisha Ulinzi Kariakoo inaweza fanya kazi 24/7 na serikali ikapata mapato makubwa sana
 
Kuna watu nawafahamu maisha yao yooote kariakoo.Ukweli serikali ikiimarisha Ulinzi Kariakoo inaweza fanya kazi 24/7 na serikali ikapata mapato makubwa sana
Sure kariakoo haswa kona ya msimbazi na uhuru huwa ipo active Muda wote...
 
Back
Top Bottom