Blasio Kachuchu

JF-Expert Member
Sep 7, 2016
326
223




Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii imeipongeza Serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa uamuzi wake wa uwekezaji kwenye kiwanda cha Chai Mponde

Uwekezaji huo umefanywa kupitia Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) kwa kushirikiana na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii kwa Wafanyakazi wa Umma (PSSSF), ambapo kiwanda hicho kinawanufaisha wakulima wa Halmashauri ya Bumbuli na maeneo yanayozunguka Wilaya ya Lushoto.

Pongezi hizo zimetolewa leo Novembe 9, 2024 Jijini Tanga na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Fatma Toufiq alipotembelea kiwanda hicho na wajumbe wa kamati hiyo kwa lengo la kuona namna gani kiwanda hicho kinavyo fanya kazi.
Aidha, Mhe. Fatma amiepongeza mifuko ya WCF na PSSSF kwa uwekezaji wenye tija unaofanywa na kwenye kiwanda cha Chai Mponde.

Awali akizungumza baada ya kuembelea kiwanda hicho, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema miongoni mwa faida za kiwanda hicho ni pamoja na kutoa ajira kwa wananchi pamoja na uhakika wa soko la chai kwa wakulima.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu WCF, Dkt. John Mduma, amesema kiwanda hicho kitawawezesha wananchi wa Lushoto, Bumbuli Korogwe na maeneo jirani kupata kipato na hivyo kuwainua kiuchumi kwani wengi wanategemea zao hilo.
Naye, mmoja kati ya wakulima wa zao la Chai katika kiwanda hicho, Mwanyemi Mdoe ameishukuru serikali ya Awamu ya Sita kwa hatua iliyoichukua ya kufufua kiwanda hicho, ambacho kinasaidia kukuza Uchumi wao.
 
Back
Top Bottom