BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 500
- 1,209
NDUGU WATANZANIA,
Kama huu sio mkataba wenyewe, watwambie mkataba wenyewe uko wapi.
Na kwanini bunge linaacha kujadili mkataba wenyewe linajadili mkataba ambao sio.
Viongozi, Bunge, Wapiga debe wao, na madalali wa rasilimali zetu wanasema huu mkataba uliosambaa na uliojadiliwa sio wenyewe. Wanasema huu unaitwa "IGA" Intergovernmental Agreement.
Wanasema huu ni mkataba wa kuweka mahusiano tu ya Kibiashara baina ya nchi mbili. Wanasema mkataba wenyewe unaitwa "HGA" Host Government Agreements.
Kwa maelezo ya vinywa vyao " IGA" inaweka tu mahusiano ya Tanzania na Dubai wakati "HGA" ndiyo itakayoeleza kuhusu uwekezaji wenyewe, yaani itaeleza nini tutapata, muda gani, tutagawana nini, wataweka mtaji kiasi gani, baada ya miaka mingapi tutaanza kufaidika, uchumi utakua kiasi gani nk, nk, nk. Kwa ufupi ni kuwa "IGA" ni ganda na "HGA" ndio ni tunda .
Swali letu kwenu Wabunge, kwanini mnajadili ganda "IGA" mnaacha kujadili tunda "HGA". Shida yetu sisi wananchi si kujua kuwa leo tarehe fulani Tanzania imeingia mahusiano ya kibiashara na Dubai basi. Sio hata kidogo.
Shida yetu ni kujua Tanzania imeingia makubaliano ya nini, tutatapata nini, kwa muda gani, thamani ya makubaliano ni ipi, maeneo gani, ajira ni ngapi kwa namba, miundo mbinu ipi inaboreshwa, thamani yake ni ipi, tulikuwa tunapata nini na baada ya makubaliano tutapata nini, uchumi wetu utakua kwa asilimia ngap, nk , nk. Hii ndio "HGA" ambayo mpaka sasa hatujui iko wapi.
Hii ndio kiu yetu, hiki ndicho tunachotaka kusikia, na hapa haswaaaa ndo kuna maslahi ya taifa.
"HGA"imeandaliwa au haijaandaliwa ?. Na hata kama "HGA" ni zaidi ya moja zimeandaliwa au bado. Kama haijaandaliwa au itaandaliwa baadae kwenye utekelezaji wa mradi, Wabunge na Serikali wanaosema mradi huu una TIJA kwa taifa hiyo tija wameiona wapi. Katika maandishi yapi na mkataba upi.
Na kama "HGA" imeshaandaliwa na ipo kwanini inaachwa kutolewa kama ilivyotolewa "IGA" ili ijadiliwe na Watanzania, na walau kwanini haijapelekwa Bungeni ili ijadiliwe.
Imeficchwa wapi na iko na nani, na kwanini inafichwa.
Kama ipo, kwa mtu mwenye akili yenye utimamu, kipi kilitakiwa kujadiliwa kwa maslahi ta taifa, " IGA" ambayo inaeleza kuanzisha tu mahusiano, au " HGA" ambayo inaeleza Tanzania inapata nini, kwa muda gani, thamani ya uwekezaji ni ipi, maeneo gani,ajira zitakuwa ngapi kwa namba, uchumi wetu utainuka kwa asilimia ngapi nk.
Kipi hapo kati ya viwili kinachostahili kulipotezea muda bunge.
KUHUSU WABUNGE.
Nyie tumewasikiliza kwa umakini jana. Karibia nyote isipokuwa wawili tu, mlikuwa mnasema MKATABA HUU UNA TIJA KUBWA KWA TAIFA.
Aghalabu mkimaliza kusema hivyo mnasema mkataba wenyewe ambao ni "HGA" bado haujaingiwa na serikali.
Sasa mtwambie hayo maslahi ya taifa mliyoyasema mmeyaona katika mkataba upi. Ndio, huo mliojadili "IGA"mnasema unaanzisha tu mahusiano na sio mkataba wa mradi, mkataba wa utekelezaji mradi"HGA" bado ila upo unakuja. Hayo MASLAHI YA TAIFA mmeyaona wapi?
Mmeyaona katika mkataba "IGA" ambao wenyewe mnasema hauelezi chochote kuhusu Tanzania inapata nini. Nyie watu MUOGOPENI MUNGU.
Na kama hayo maslahi ya taifa mmeyaona "HGA" basi kwanini mnakubali kujadili "IGA" ambayo haielezi maslahi ya taifa mnaacha kujadili "HGA" ambayo inaeleza maslahi ya taifa, ambayo inaeleza idadi ya ajira, ambayo inaeleza tutapata asilimia ngapi, ambayo inaeleza uchumi utakua vipi nk, nk.
Nyie wabunge, kweli waliotunga Ibara ya 63 ya Katiba inayotaka mjadili mikataba ya kimataifa kabla ya kuingiwa na serikali walilenga mjadili kuingia tu mahusiano "IGA" na sio Tanzania inanufaika vipi "HGA". Kweli, kweli, kweli hicho ndicho walichokilenga.
Pili, kweli sisi tumewatuma mkajadilli kuingia tu mahusiano "IGA" badala ya tunapata kiasi gani, ajira zetu ni ngap,nk,nk"HGA". Kweli,kweli,kweli hiki ndicho tulichokutumeni.
Tunakulipeni posho,mishahara, na marupurupu kibao mkawe sauti na jicho letu namna hii?
Hapana, hapana, nikwambieni sisi tuna akili kuliko nyinyi na kwa taarifa yenu tumewatangulia sana katika uwezo wa kufikiri. Ni basi tu hatuna hizo nafasi.
Sasa tunataka kujua "HGA" iko wapi na inasema nini. Hiyo "IGA" wala hatuna haja nayo sababu haizungumzii lolote la kwetu. Haizungumzii ugali wetu wala hatima yetu.
Twambieni "HGA" iko tayari au haiko tayari. Kama iko tayari iko wapi na kwa nini haijadiliwi wala kuoneshwa hadharani. Na kama haiko tayari labda itaandaliwa badae hayo MASLAHI YA TAIFA mnayosema yapo kwenye biashara hii mmeyaona wapi?
Andiko la Bashir Yakub, WAKILI.