Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,820
- 31,847
KAMA NILIVYOWAONA KATIKA UTAFITI WA HISTORIA YA TANGANYIKA
BARAZA LA MAWAZIRI WA TANGANYIKA 1963
Julius K. Nyerere, 41 years old, President
Rashidi Mfaume Kawawa, 34 years old, Vice-President
Sheikh Amri Karuta Abedi, 39 years old, Minister of Justice
Derek Noel Maclean Bryceson, 40 years old, Minister of Agriculture
Clement George Kahama, 34 years old, Minister of Commerce
Oscar Salathiel Kambona, 35 years old, Minister of External Affairs and Defense
Job Malecela Lusinde, 32 years old, Minister of Home Affairs
Amir H. Jamal, 41 years old, Minister of Communication
Paul Bomani, 38 years old, Minister of Finance
Alhaj Tewa Said Tewa, 37 years old, Minister of Lands
Jeremiah Sam Kasambala, 38 Years old, Minister of Co-operative and Community Development
Solomon Nkya Eliufoo, 42 years old, Minister of Education
Saidi Ali Maswanya, 39 years old, Minister of Health
Michael Kamaliza, 33 years old, Minister of Labor
Austine K.E. Shaba, 38 years old, Minister of Local Government
L. Nang’wanda Sijaona, 35 years old, Minister of National Culture and Youth
Nsilo Swai, 38 years old, Minister of Development Planning.
Haya majina ya Baraza la Mawaziri mwaka wa 1963 yamekuwa yakizunguka katika mitandao kwa muda kiasi.
Imenijia fikra nirejee kwenye Maktaba yangu niangalie ni wapi majina haya nimekutananayo katika utafiti wangu wa historia ya Tanganyika/Tanzania.
Naamini kuna taarifa muhimu katika historia ya maisha ya mawaziri hawa ambao wakati ule walikuwa vijana sana kama umri wao unavyoonyesha Tanganyika ilipopata uhuru na kuanza kujitawala yenyewe.
Katika hili nitaweka yale mimi nimeyaandika na nitahariri kidogo kwa ajili ya ufahamu wa msomaji:
JULIUS KAMBARAGE NYERERE
‘’Lakini aliyeshika nafasi ya juu kabisa katika fikra zangu nikiwa mtoto alikuwa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, na ni kupitia kwake ndipo tukapata kujua kwa mara ya kwanza kuwa kuna kabila linaitwa, ‘’Wazanaki.’’
Kila alipokuwa anakuja nyumbani kwetu kuja kwake kulikuwa jambo maalum kulikosababisha minong’ono watu wakizungumza kwa sauti za chini wakipeana taarifa kuwa, ‘’Nyerere anakuja au keshafika.”
Kwangu mimi hii ilikuwa ishara ya kutimiza kazi yangu kwani siku zote nilikuwa nikiambiwa kutengeneza kifungua kinywa cha chai na mayai kila alipokuja nyumbani akitokea Shule ya Mt. Franci(s, Pugu alipokuwa akisomesha.’’
(Aisha ‘’Daisy Sykes’’ akimweleza Julius Nyerere miaka ya mwanzo ya kuundwa kwa TANU alipokuwa akifika nyumbani kwa baba yake Abdulwahid Sykes Mtaa wa Stanley na Sikukuu, ‘’Abdulwahid Sykes niliyemjua,’’ Daisy Sykes Buruku, 2018).
RASHID MFAUME KAWAWA
‘’Kwa mara ya kwanza Tanzania ilishuhudia kuandikwa kwa historia ya mmoja wa viongozi wakuu wake kupitia kitabu “Simba wa Vita Katika Historia ya Tanzania Rashidi Mfaume Kawawa” kilichoandikwa na Dk. John M. J. Magotti. Wahariri wa magazeti yote walikataa kuchapa hili pitio langu la kitabu alichoandika John Magotti wa Chuo Cha CCM Kivukoni).
Sidhani kama katika historia ya Tanzania kuna kumbukumbu ya kuandikwa kwa kitabu kinachohusu maisha ya kingozi yoyote achilia mbali kufanyika kwa sherehe ya kukizindua kitabu hicho Ikulu ikiongozwa na Rais mwenyewe.
Kwa hakika sherehe ilifana sana na tukakisubiri kwa hamu kitabu madukani ili tupate kunufaika na kumbukumbu za Mzee Kawawa.
Msomaji anaweza kukisoma kitabu chote chenye kurasa 127 kwa muda wa saa moja akawa kakimaliza chote na atakapokiweka chini akawa hakubakia na chochote cha maana katika fikra yake.
Kwa nini iwe msomaji asibaki na kumbukumbu yoyote ya kiongozi mkubwa kama Mzee Kawawa mtu aliyeshuhudia kwa macho yake mwenyewe harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika na si hivyo tu yeye mwenyewe ni mmoja wa wale waliopigania uhuru wa Tanganyika na kushika nyadhifa kubwa za uongozi chini ya Mwalimu Julius Nyerere.
Kwa kawaida vitabu vya maisha ya viongozi hasa wapigania uhuru huwa vina mambo mengi sana ambayo kwa muda mrefu huwa siri, hayafahamiki hadi hapo kitabu kitakapoandikwa ama kwa mkono wake kiongozi mwenyewe au kuandikwa na muandishi.
Mifano ipo mingi. Kitabu kama “Mahatma Gandhi” kilichoandikwa na Robert Payne au “Long Walk to Freedom” alichoandika Nelson Mandela mwenyewe au “Seeds of Freedom” alichoandika Bildad Kaggia hakika unapomaliza kusoma vitabu hivi lazima urudi nyuma kufungua kurasa hapa na pale kuzisoma upya zile sehemu zinasosisimua.
Huwezi kupata haya katika kitabu cha Mzee Kawawa. Huwezi kuyapata haya kwa kuwa mwandishi hakuandika kitu.
Hakuandika kitu si kama Mzee Kawawa hana historia ya kusisimua na kuwa hana mengi ambayo wengi hawayajui katika maisha yake, nadhani mwandishi hakuwezakuja na jipya labda kwa sababu hakufanya utafiti wa kutosha kuweza kuandika kitabu kinachomuhusu simba wa vita aneunguruma.
Kuna msemo wa Kiswahili usemao “Aungurumapo simba mcheza ni nani?”
Kwa hakika Simba wa Vita hakuunguruma kabisa katika kitabu hiki.
Sijui lawama zielekezwe wapi.’’
(Pitio la kitabu ’’ Simba wa Vita,’’ katika historia ya Tanzania Rashidi Mfaume Kawawa, Mohamed Said 26 December, 2016.
Wahariri wa magazeti yote walikataa kuchapa hili pitio langu la kitabu alichoandika John Magotti wa Chuo Cha CCM Kivukoni).
KALUTA AMRI ABEID
‘’Mazishi ya Abdulwahid Sykes yalifanyika siku ya Jumapili tarehe 13 Oktoba, 1968. Mazishi yake yalikuwa makubwa yasiyo kifani.
Ukitoa mazishi ya mwaka 1951 ya Sheikh Idrissa bin Saad, muasisi na Khalifa wa Tariqa Askariyya na mazishi ya Sheikh Kaluta Amri Abeid mwaka 1963, Dar es Salaam ilikuwa haijapata kushuhudia mazishi kama hayo.’’ ‘’Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes (1924 – 1968)...’’ 1998, Mohamed Said).
CLEMENT GEORGE KAHAMA
‘’Sheikh Hassan bin Ameir alikereka na hili na hasa pale George Kahama, Waziri wa Mambo ya Ndani, alipokwenda Italia kuweka uhusiano baina ya Tanganyika na Vatikano.’’
(‘’Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes (1924 – 1968)...’’ 1998
Mohamed Said).
OSCAR SALATHIEL KAMBONA
Albert Rothschild alikuwa Myahudi akiishi Paris.
Nilijuananae Nairobi kupitia kwa rafiki yangu Peter Colmore.
Tukawa marafiki na mshirika wangu katika biashara.
Nikamtia hima Rothschild aje Tanzania kuangalia maeneo ambayo angeweza kuwekeza na tukafungua biashara.
Akiwa Madagascar akanipigia simu kuwa yuko Madagascar na anakuja Dar es Salaam kwa hiyo nikampokee Uwanja wa Ndege.
Mimi sikujua kumbe Oscar Kambona, Waziri wa Mambo ya Nchi za Njee amekuja na yeye kumpokea Rothschild kama mgeni wa serikali.
Rothschild alikuwa amekuja na ndege yake binafsi akiongozana na wasaidizi wake.
Kwa haraka alipitishwa VIP Lounge na Kambona alishangaa Rothschild alipomwambia kuwa hatioanda gari ya serikali bali atapanda gari yangu.
Hii ilikuwa kinyume na itifaki lakini Rothschild alikataa kata kata kupanda gari ya serikali pamoja na Kambona akanga’nga’nia kupanda gari yangu.’’
(‘’Under the Shadow of British Colonialism The Life of Ally Kleist Sykes''
As told to Mohamed Said ,’’ (Unpublished)1999).
SOLOMON NKYA ELIUFOO NA NSILO SWAI
‘’Nyerere akawa sasa kazungukwa na wa tu wapya.
Kulikuwa na watu kama Nesmo Eliufoo ambae aliingia serikalini kwa ajili ya Uchaguzi wa Kura Tatu wa mwaka wa 1958.
Mimi ndiye niliyemuingiza Eliufoo TANU.
Nakumbuka masharti ambato Eliufoo alinipa ili ajiunge na harakati za kudai uhuru na kusimama kama mgombea wa TANU ni kuwa apewe nafasi katika serikali.
Alikuwapo na Nsilo Swai ambae alipewa nafasi katika serikali baada ya uchaguzi wa kwanza 1965 baada ya uhuru mwaka wa 1961.
Hawa walikuwa wageni katika TANU.
Wale waliojiunga na TANU katika uchaguzi wa Kura Tatu wengi wao hawakuthamini mchango wa watu kama Dossa Aziz au John Rupia.
Utii wao ulikuwa umeegemezwa kwengine.
Lakini jambo muhimu sana ni kuwa tulipopata uhuru mwaka wa 1961, uhuru ukawa umefungua milango kwa wanasiasa kujitajirisha kupitia migongo ya wananchi.
TANU na serikali ikawa ina watu wa kujipendekeza kwa wakubwa, walamba nyayo na watu ambao walitaka kutengeneza fedha kwa haraka na kutoweka mara moja.
Nyerere akawa mbali na sisi ambao ndiyo tulikuwa msingi wake wa mwanzo akawa sasa kazungukwa na watu waliojali maslahi yao wenyewe.
Ikawa sasa si viongozi na wanachama kuihudumia TANU bali sasa ikawa TANU ndiyo inahudumia viongozi.
Fitna wivu na wizi wa fedha za chama vikawa sehemu ya utamaduni wa chama cha TANU.’’
(‘’Under the Shadow of British Colonialism The Life of Ally Kleist Sykes’’As told to Mohamed Said,’’ (Unpublished) 1999).
TEWA SAID TEWA
''Tewa Said anakumbuka siku kabla ya uchaguzi pale Ukumbi wa Arnatouglo, Abdulwahid alikwenda nyumbani kwake jioni.
Wakati huo Tewa alikuwa akikaa mtaa wa Stanley na Swahili, si mbali sana kutoka nyumbani kwa Abdul Sykes.
Abdul alimwambia Tewa maneno haya kuhusu mabadiliko ya uongozi ambayo waliamua kuyafanya katika TAA,
‘’Tewa, kesho tunakwenda kumpa huyu mtu, Nyerere, mamlaka ya kuendesha nchi hii.
Kuanzia hapo, mara tu tutakapomchagua kutuongoza hakuna namna tena ya kumnyangíanya madaraka tuliyompa.
Hatumfahamu vizuri sana lakini natumaini kila kitu kitakwenda sawa.’’

Naamini wasomaji wangu nyie kama mimi mmeweza kuona kuwa nyakati zile za kudai uhuru wa Tanganyika zilikuwa nyakati za mambo makubwa, mambo ambayo yalikuja kuleta mambo mengine makubwa zaidi si kwa Tanzania peke yake kama nchi bali hata katika maisha ya wale ambao moja kwa moja walihusika katika kupigania uhuru.
Muhimu sana kwetu kuhifadhi historia hii.