Kallaghe kwenda UK Mlima kwenda Canada?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,746
40,894
Katika pita pita vi inzi vinadokeza kuwa balozi wa TZ huko Canada anatarajiwa kuhamishiwa UK na yule ambaye tulidokeza miezi michache nyuma kuwa ameshindwa kupelekwa kule Scandinavia anaweza kupelekwa Canada badala yake. Na upo uwezekano hatimaye wa yale mabadiliko ya Bandari ambapo rafiki yetu mmoja amepigania sana kulepekwa huko na kuna uwezekano atakwenda.
 
MKJJ wa bandari yupi huyoo?? ina maana kalaghe naye kazi za kufungua matawi ya ccm alishaanza huko Canada??
 
Long live kainzi. Kwa hiyo Mlima anapelekwa Canada. A Swedish citizen representing Tanzania in Canada. How sweet!
 
Long live kainzi. Kwa hiyo Mlima anapelekwa Canada. A Swedish citizen representing Tanzania in Canada. How sweet!

Jasusi, Dual citizenship inakubalika kwa mlango wa nyuma, kwa mlango wa mbele ukishachukua uraia wa nchi nyingine basi wewe si Mtanzania tena!! Hawa "viongozi" wetu wana maamuzi ya ajabu sana. Hivi hakuna Mtanzania anayeweza kuteuliwa katika nafasi hiyo mpaka huyu jamaa? Au kwa kuwa kapigiwa debe kali na Mkapa?
 
Ngoja huyu Milima wamnyang'anye passport na urai kama yule mturuki. Sema mturuki alidanganya ndoa. Tusbiri tone reaction ya hawa Scandnavia maana nao wako strict sana na masuala ya uraia. Lakini kama Dr. Milima ni mtendaji mzuri kihivyo ni kwa nini mzee Chen Kapa anamwachia? Isije ikawa ni mzigo! Lo nawaza kwa mbali tu wajameni!
 
BJ good to hear from you.....sikuoni kwa kina Messi...Karibu Bondeni tupige mavuvuzela
 
Nimekuaminia Mwanakijiji, kainzi hakachezi mbali

JK ateua mabalozi saba kushika nafasi mbalimbali

Rais Jakaya Kikwete ameteuwa mabalozi saba kushika nafasi mbalimbali katika balozi zetu nchini Sweden, Canada, Ehiopia, Paris-Ufaransa na Balozi wa Kudumu Kwenye Umoja wa Mataifa.

Katika uteuzi huo Rais Kikwete amemteua Mohamed Mwinyi Haji Mzale kuwa balozi wetu Stockholm Sweden, anachukua nafasi iliachwa wazazi na Ben Moses aliyestaafu utumishi wa Umma.

Wengine walioteuliwa ni Alexander Masinda kuwa balozi mpya Ottawa, Canada kuziba nafasi ya Peter Kallaghe aliyeteuliwa kuwa balozi wa Tanzania London. Kallaghe anachukua nafasi ya Mwanaidi Sinare Maajar ambaye mapema mwaka huu alihamishiwa Washington DC.

Aidha, aliyekuwa Balozi wa Tanzania Washngton DC, Ombeni Sefue ameteuliwa kuwa Mwakilishi wa Kudumu kwenye Umoja wa Mataifa kushika nafasi iliyoachwa wazi na Augustine Mahiga ambaye ameteuliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuwa mwakilishi wake maalum kwenye mgogoro nchini Somalia.

Katika uteuzi huo pia aliyekuwa balozi wa Tanzania Brazil, DKT Joram Biswaro amehamishiwa Addis Ababa na Umoja wa Afrika wakati aliyekuwa Balozi Mohamed Maundi amerejehswa nchini kuwa Mkuu wa Chuo Cha Diplomasia, Dar es Salaam.

Aidha Rais Kikwete amemteau Begum KArim-Taj kuwa balozi, Paris kujaza nafasi iliyoachw awazi na Hassan Gumbo Kibelloh aliyestaafu
Source: Issa Michuzi​
 
well.. habari ndiyo hiyo tena!! Asante Bi. Senti 50 si unajua tena vinzi havichezi mbali...
 
Hivi ugimbi unapatikana wapi akili ikae sawasawa maana naona nahitaji akili ya ziada kwa sasa
 
Naona Ambassador Sefue anazidi kubaki huko East Coast [Big Apple]

Raisi Jakaya Kikwete amewateua na kuwahamisha vituo vya kazi mabalozi saba kushika nyadhifa mbalimbali ndani na nje ya nchi.

Wizara ya Mambo ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa imewataja mabalozi hao kuwa ni:


  1. Mohamed Mwinyi Haji Mzale - balozi nchini Sweden
  2. Alexander Masinda - balozi Canada
  3. Peter Allan Kalaghe - balozi Uingereza
  4. Dk. Joram Mukama Biswalo - balozi Ethiopia
  5. Begum Karim Taj - balozi Ufaransa
  6. Ombeni Sefue - mwakilishi wa kudumu katika Umoja wa Mataifa
  7. Dk. Mohamed Omar Maundi - Mkuu wa chuo cha Diplomasia jijini Dar Es Salaam
 
Dr Mahiga kaenda wapi? Nilidhani yeye ni kati ya mabalozi wazuri tuliowahi kuwa nao ukimwondoa SAS!
 
Long live kainzi. Kwa hiyo Mlima anapelekwa Canada. A Swedish citizen representing Tanzania in Canada. How sweet!
WHAT???
please tell me that this is not another venting or sorry vetting mishap!!!
 
Back
Top Bottom