Kairuki: Walimu wa sanaa hawataajiriwa

bado lawama zinapaswa ziende kwa wabunge wetu.hivi serikali inaondoaje upungufu wa walimu shule za msingi kwa kusambaza walimu 7463 tu wa ziada waliopo sekondari? wabunge wetu wengi ni mizigo.
 
Pole zao, ila iwe fundisho kwa Hawa nyoka walioko secondary wanao endekeza mapenzi na kukimbia Sayansi japo hata hio sayansi nayo baadae itakua mule mule
 
Kwa hiyo sasa wasimamishe udahili wa wanafunzi wa sanaa katika vyuo vya ualimu mpaka watakapohitajika. Hakuna haja ya kuwajaza vyuoni wakati hawahitajiki itakuwa ni kupoteza pesa na muda wao
Mkuu umenikosha sana kwa andiko lako.
Nilikuwa nafikiria hilo jambo sana.
Bora wafanye hivyo ili mikopo hata kama ni kidogo ielekezwe kwa wanafunzi wa kozi zingine.
 
bado lawama zinapaswa ziende kwa wabunge wetu.hivi serikali inaondoaje upungufu wa walimu shule za msingi kwa kusambaza walimu 7463 tu wa ziada waliopo sekondari? wabunge wetu wengi ni mizigo.
Kuna mzizi umejichimbia chini sana ambao unakula mizizi mingine na kwa namna hiyo kung'olewa inakuwa ni shida sana.

Tuombe Mungu atufikishe salama
 
Kwa hali hiyo kunahaja ya kuzitoa kozi za education.Vyuoni kwasababu, watu watakuwa wanasioma na kurundikanaa mitaani tu, na mfumo wetu wa elimu huu unaomfanya mwanafunzi kuajiriwa kwa kazi za ofisini
 
Sasa hizi kozi zisimamishwe, vyuo visidahili waalimu kusomea ufundishaji wa sanaa maana hakuna haja. Wasubiri wakiwahitaji ndo waanze.
 
Nani mwingine aliyemsikia mtangazaji wa TBC akisema ''na Mbunge wa utumishi na utawala bora'' anatoa majibu kwa upande wa serikali?
 
Msijali ajira za masomo ya arts zitaruhusiwa msimu wa 2019/2020 ili muwachague tena 2020 baada ya hapo wembe ni ule ule wa namba kusomeka ahsante JK hukua na makuu kwenye ajira japo ww ndio chanzo cha yote haya kweli alieshiba hamjui mwenye njaa
 
Mmewasomeshea nini sasa?
Wengine wanadaiwa na mikopo
Bado mnawadahili wengine huku kuna walioko vyuoni sasa hivi
Nani ametuloga?
 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Angela Kairuki amefunguka na kusema serikali kwa sasa haitaweza kuajiri walimu wapya wa sanaa bali itawatumia walimu wa sanaa wa ziada waliopo katika shule za sekondari.


Waziri Angela KairukiAngela Kairuki amesema hayo leo bungeni na kudai kila shule itaweza kupata walimu wa sanaa kulingana na mahitaji yao

"Utafiti uliofanywa na Ofisi ya Rais Tamisemi mwaka 2015/2016 umebaini kuwepo kwa ziada ya walimu wa masomo ya sanaa wapatao 7463 katika shule za sekondari, kutokana na hali hii serikali inaendelea na zoezi la kuwagawanya walimu hao au kuwa 'redeploy' kwa kuzingatia uwiano na mahitaji halisi ya walimu wa sanaa kwa kila mamlaka za serikali za mitaa ili kila shule iweze kupata walimu wa masomo ya sanaa badala ya kuajiri walimu wapya"

-alisema Angela Kairuki Mbali na hilo Waziri Kairuki amesema serikali inaendelea kuajiri watumishi wa kada mbalimbali ambapo katika mwaka wa fedha 2016/2017 watumishi zaidi ya elfu tisa wameajiriwa serikalini.


"Katika mwaka wa fedha 2016/17 jumla ya watumishi wa Umma 90721 wamekwisha ajiriwa kwa kuzingatia vipaumbele na mahitaji ya kila mwajiri na katika mwaka wa fedha 2017/18 serikali inatarajia kuajiri watumishi 52436 wa sekta mbalimbali kwa kuzingatia vipaumbele v
Sasa hizi kozi zisimamishwe, vyuo visidahili waalimu kusomea ufundishaji wa sanaa maana hakuna haja. Wasubiri wakiwahitaji ndo waanze.


ya taifa pamoja na kuimarisha kila sekta na upungufu mkubwa wa watumishi wa Umma"

-alisema Kairuki



Chanzo : EATV


Waziri amesema 2016/17 hadi sasa serikali imeajiri nafasi 9,721 na siyo elfu 90 kama ilivyoripotiwa
 
Back
Top Bottom