Kafulila: UNDP imetoa orodha ya nchi 54 duniani zilizoelemewa na deni la Taifa. 25 zinatoka Afrika Tanzania haipo, tukope zaidi tujenge Uchumi zaidi

Mwanahabari wa Taifa

JF-Expert Member
May 27, 2020
1,453
807
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe David Kafulila kupitia Ukurasa wake wa Instagram amewafunda wanaolalamika Kuhusu ukuaji wa deni la Taifa.

Kafulila amesisitiza kama Taifa lazima tukope zaidi ili tujenge uchumi wetu zaidi,

Mhe Kafulila anasema hata Japan ambayo ni nchi ya tatu Duniani kwa Utajiri bajeti yake 40% ni mikopo hivyo tuache maneno maneno Tanzania tuko vizuri,

**************************************
Kafulila anasema, Ripoti ya UNDP Nov2022, imetaja nchi54 zenye hali mbaya ya deni la Taifa Dunian, huku 25 zikitoka Afrika wala Tanzania sio miongoni mwao,

Kafulila anaendelea kwa kusema " Ripoti za Taasisi ya MOODY'S, ambayo ni moja ya taasisi 3 kubwa duniani kwa kupima afya ya uchumi kumudu kulipa deni ( MOODY'S, S&P na Fitch zinamiliki 95% ya biashara hii duniani),

Agust 2021 na Oktoba 2022 imeonesha Tanzania bado inafanya vema usimamizi wa deni kutokana kupata mikopo ya muda mrefu na nafuu (concessional loans).

Anaendelea kusisitiza, Tukope kujenga uchumi,Ulaya ilikopa kujenga uchumi baada ya vita ya dunia kwa kusaidiwa na USA( Marshall Plan, )

Bajeti ya Japan ya mwaka 2021, nchi ya 3 kwa ukubwa wa uchumi dunaini, asilimia 40% ni mikopo.

Anasema, "Naam, tukope zaidi kujenga zaidi hasa mikopo ya muda mrefu ambayo uwekezaji miradi hii itaongeza msuli wa uchumi wetu kulipa deni.

Mwaka 2021/22 ndio mwaka deni limeongeka kwa trilioni10(BoT- MER) lakn ndio mwaka uchumi uliongezeka kwa zaidi ya dola bilioni 5.4 kufikia $67.7bn kutoka $62.3bn ambazo ni sawa na nyongeza ya uchumi kwa miaka miwili ( 2019|20 na 2020|21 ),

Hii ndio maana ya kukopa kujenga uchumi wa nchi.

***************************************

Anasema David Kafulila
 
Kigoma mko vizuri sana kwenye UCHAWA
Fh8w3VuWIAEnh7K.jpeg
 
Back
Top Bottom