Vugu-Vugu
JF-Expert Member
- Feb 24, 2017
- 1,220
- 1,385
CEO wa PPP Bw David Kafulila amesema Mpango wa Serikali ya Tanzania wa Miaka Mitano umelenga kutekeleza jumla ya miradi yenye thamani ya TZS 114 Trilioni,
TZS 40.6Trilioni zitatoka katika Sekta binafsi Kwa kutumia JV, UBia na Utaratibu Mwingine Serikali itakaoona unafaa.
Mkurugenzi huyo wa Ubia nchini Bw David Kafulila ameliambia Taifa kuwa sera, Kanuni na Sheria zilizoanzisha PPP zimekuwepo hata kabla ya Ujio wa awamu ya Sita ya Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.
Kafulila amefafanua kuwa Tanzania tayari inaendesha miradi kwa Ubia na Sekta binafsi yenye thamani ya US$ 1 billon sawa na karibu ya TZS 2.6 trilioni.
Mkurugenzi huyo ameendelea kwa kusema dhumuni la PPP na Ubia ni kuipa Serikali nafuu ya kutekeleza miradi mingine mingi ambayo ni muhimu zaidi lakini haiwezi kutekelezwa na Sekta binafsi Kwa mfano Mishahara ya Watumishi na mengineyo.