Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,617
- 13,320
Chama cha Wafanyakazi wa Vyombo vya Habari Tanzania (JOWUTA) kimetoa maombi hayo baada ya kudai kupokea malalamiko kutoka kwa Wanachama wake kuhusu maslahi yao na haki zao ikiwepo kutolipwa mishahara, kutopewa mikataba licha ya kufanyakazi kwa muda mrefu, kufukuzwa au kusimamishwa kazi bila kufuata Sheria na taratibu.
Mwenyekiti wa JOWUTA Taifa, Mussa Juma amesema Watumishi hao wa Radio Free Afrika (RFA), Kiss FM na Star TV wamekuwa na madai ya kutolipwa mishahara na stahiki zao zaidi ya Tsh. Bilioni 2.5, madai ambayo yamesajiliwa Idara ya Kazi Mkoa wa Mwanza hadi kufikia Mwaka 2022 na tayari madeni yameongezeka.
Ameeleza Idara ya Kazi Mkoa wa Mwanza ilikamilisha mchakato wake wa kufikishwa Mahakamani suala hilo tangu Aprili 2023 kwa kukabidhi nyaraka muhimu Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka Kanda ya Ziwa iliyopo Mwanza lakini halijafikishwa Mahakamani.
Amesema "Tunaiomba Serikali kulifikisha Mahakamani suala hili kwani majadiliano nje ya Mahakama na mwajiri yamekwama na kibaya zaidi Wafanyakazi wanaolalamikia maslahi yao wameendelea kuondolewa kazini bila kulipwa stahiki zao.
Pia soma - Mgogoro wa maslahi ya Wafanyakazi wa Star TV, Radio Free Africa, Kiss FM mambo bado magumu