Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,961
- 5,082
Wakuu,
Panazidi kuchangamka huko,
Baadhi ya vyama vya siasa nchini vimesema haviko tayari kususia uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba, mwaka huu kwa kigezo cha marekebisho ya katiba mpya.
Haya yamebainishwa mkoani Morogoro na Makamu Mwenyekiti Taifa Chama cha NCCR Mageuzi Joseph Selasini katika Mkutano wa Baraza la Vyama vya Siasa ambapo amesema kuwa kwa muda uliobaki marekebisho hayo ya katiba mpya hayawezi kufanyika na badala yake amevisihi vyama hivyo kutumia nguvu kubwa katika kuwahamasisha wananchi kwenda kupiga kura.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Naye Katibu Mkuu wa Chama Cha NLD, Doyo Hassan Doyo amewataka baadhi ya wanasiasa kuacha kutoa matamko yasiyofaa, huku Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa Juma Khatibu amevitaka vyama vya siasa nchini kutoa fursa kwa wanawake na wenye ulemavu kushiriki katika siasa.