John Travolta anapaki ndege nyumbani kama vile ni magari

Maana ya huwo msemo ni kwamba Utajiri wa kujionyesha kama huo wa huyo Travolta ndiyo hautakiwa na ndio maana unaona watu kama kian Warren Buffet, Bill Gates ni mabilonea lkn hata tu private jets hawana au hata kama wanayo huwezi kuiona kapiga nayo picha hivyo huyo Travolta hata milioni 500 USD hafikishi full kujionyesha, sasa hawa ndiyo watu wanaoongelewa kwamba amepata utajiri lkn amepoteza maisha yake, matajiri kama Bill Gates ametoa nusu ya utajiri wake kusaidia ambao hawajapata bahati ya kufanikiwa ...

Mkuu, hapo tutabishana hadi asubuhi. Hao kina Warren, Bill Gates akili zao sio nzuri kama wana mabilioni bado wanataka kuishi kama watu wa kawaida. Sasa hayo mambilioni yanawasiaidia nini? Wanafurahia kuyaona kwenye vitabu vyao vya benki? Watakapokufa yatawasaidia? Kama kweli ni watu humble wayatoe yote kusaidia jamii basi.

Unajua watani zangu wasukuma hata wao siku hizi hawakubali kuwa na ng'ombe 800 halafu nyumbani wanalala kwenye nenekeja (ngozi).

Siwaelewi kabisa watu wenye uwezo wa kununua Landcruiser halafu wanatembelea Corola, ambalo kwanza sio safe sana kama Landcruiser!

Kama Travolta ana uwezo wa kununua ndege sita katika maisha yake na bado akaishi vizuri hadi azeeke na kufa, mwache anunue ndege sita!

Juhudi zote za kupata mabilioni ni ili uyafurahie yakiwa benki? Utakuwa na akili za mwenda wazimu. Tumia, au saidia watu nk. Sio uishi maisha ya kawaida ili watu wakuone uko humble, au uwaachie watu urithi?

Travolta ana akili sana.
 
Kuna viatu vinaitwa Travolta. Sijui vina uhusiano gani
Kama hizi zangu?
1467971061988.jpg
1467971067929.jpg
1467971074076.jpg
 
Maana ya huwo msemo ni kwamba Utajiri wa kujionyesha kama huo wa huyo Travolta ndiyo hautakiwa na ndio maana unaona watu kama kian Warren Buffet, Bill Gates ni mabilonea lkn hata tu private jets hawana au hata kama wanayo huwezi kuiona kapiga nayo picha hivyo huyo Travolta hata milioni 500 USD hafikishi full kujionyesha, sasa hawa ndiyo watu wanaoongelewa kwamba amepata utajiri lkn amepoteza maisha yake, matajiri kama Bill Gates ametoa nusu ya utajiri wake kusaidia ambao hawajapata bahati ya kufanikiwa ...
Wewe na yeye mnautofauti gani? Tena bora yeye mwenye maisha bora kuliko wewe kibaraka wa ccm,usiekua na nyuma wala mbele.
 
Mkuu, hapo tutabishana hadi asubuhi. Hao kina Warren, Bill Gates akili zao sio nzuri kama wana mabilioni bado wanataka kuishi kama watu wa kawaida. Sasa hayo mambilioni yanawasiaidia nini? Wanafurahia kuyaona kwenye vitabu vyao vya benki? Watakapokufa yatawasaidia? Kama kweli ni watu humble wayatoe yote kusaidia jamii basi.

Unajua watani zangu wasukuma hata wao siku hizi hawakubali kuwa na ng'ombe 800 halafu nyumbani wanalala kwenye nenekeja (ngozi).

Siwaelewi kabisa watu wenye uwezo wa kununua Landcruiser halafu wanatembelea Corola, ambalo kwanza sio safe sana kama Landcruiser!

Kama Travolta ana uwezo wa kununua ndege sita katika maisha yake na bado akaishi vizuri hadi azeeke na kufa, mwache anunue ndege sita!

Juhudi zote za kupata mabilioni ni ili uyafurahie yakiwa benki? Utakuwa na akili za mwenda wazimu. Tumia, au saidia watu nk. Sio uishi maisha ya kawaida ili watu wakuone uko humble, au uwaachie watu urithi?

Travolta ana akili sana.

Ndiyo maana nimekwambia Mathayo 26:16 haujailewa, lkn ni swala la mtazamo tu na inategemea wewe kwako kuishi kama mtu wa kaiwada unakutafsiri vipi, kama kigezo chako ni private jet basi pia huyo ni mtazamo wako!
 
MKuu tuambie basi una maana gani kusema Travolta ana utajiri wa kujionyesha kwa kuwa sio tajiri kama kina Bill Gates. Maana tunavyoelewa ni kwamba Travolta anaishi kuliingana na kipato chake wakati kina Bill Gates hawaishi kulingana na kipato chao, wana mkono wa birika.
 
MKuu tuambie basi una maana gani kusema Travolta ana utajiri wa kujionyesha kwa kuwa sio tajiri kama kina Bill Gates. Maana tunavyoelewa ni kwamba Travolta anaishi kuliingana na kipato chake wakati kina Bill Gates hawaishi kulingana na kipato chao, wana kono wa birika.

Ndiyo maana nimesema ni swala la mtazamo tu, halafu mambo mengine inapaswa kwanza uwe nayo ndiyo uweze kuongelea, yaani uwe na 80 Bilion USD ndiyo uweze kuelewa inakuwaje na ina maana gani ni kama vile mtu aanze kukwambia kwamba Siberia baridi inafikia nyuzi joto 40 C chini ya sifuri, sasa kama wewe umezaliwa na kukulia Dar ni ngumu kuweza kutoa tathmini maana yake nini kuishi na nyuzi joto 40 chini ya sifuri!
 
Pamoja na fedha zote na kuwa pilot mwenye rating za kurusha ndege nyingi...kilichoniuzi kuhusu huyu jamaa ni BWABWA....
 
Kipimo changu cha jinsi nchi yangu Tanzania ilivyo masikini ni pale ninapokumbuka kwamba pato letu la taifa kwa mwaka liko chini ya mapato ya matajiri wengi tu duniani. Yaani, kuna watu wanapata fedha nyingi kwa mwaka kuliko ile ambayo Tanzania inakusanya, pamoja na juhudi na kubana sana watu walipe kodi. Wanaweza hata kutuambia tupange bajeti halafu tuwapelekee bili ili walipe!

Hebu fikiria kama nchi tuna-struggle kununua tu-ndege tuwili toka Kanada wakati mwigizaji wa movie John Travolta ana ndege zake binafsi za kutembelea sita, na anazipaki nyumbani kama magari!

View attachment 364129

John Travolta loves flying so much that he lives in a community in Florida dedicated solely to pilots, and has a private runway right in front of his house. He has his jets parked in his driveway!
kwe awamu hii ya tano watanzania wengi tutapaki ndege home.........tena c ndege hata meli tutapaki home
 
ila jamani tukumbuka yeye Travolta anajihudumia mwenyewe ila pato la Tanzania linahudumia watu zaidi ya mil 40..fikiri kabla ya kunena jamani..ni hayo tu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom