John Mrema, kwenye conference yake ya leo na wanahabari, kwa mtu ambaye hamjui, angedhani ni msemaji wa Tume ya ucjaguzi.
Wale waliokuwa na mashaka na G55 unayoongozwa na John Mrema, leo wamepata jibu la wazi.
Katika kikao chake na vyombo vya habari, Mrema ametumia muda wake mwingi kuonesha kuwa Tume ya uchaguzi ipo sahihi kuizuia CHADEMA kutoshiriki uchaguzi kwa sababu hawajasaini kanuni za uchaguzi.
Wakati CHADEMA na wadau mbalimbali wameeleza kuwa siku zote sheria na kanuni zinazotungwa na chombo chochote, ikiwa ni pamoja na zile za Tume ya ucjaguzi ni lazima zizingatie Sheria mama, yaani katiba ya nchi. Na zikiwa kinyume au zinakizana na katiba, sheria au kanuni hizo zinakuwa Null and Void. Maana yake zinakuwa ni batili. Lakini John Mrema ameonesha kuwa kanuni yoyote inayotungwa na Tume ya uchaguzi ni final.
Kwa Mrema, leo hii, Tume ya uchaguzi hata ikaandika kwenye kanuni kuwa wagombea watakaokiuka taratibu wacharazwe fimbo, kwake ni sawa, kwa sababu ni kanuni iliyotungwa na Tume ya uchaguzi!!
Kwa sasa, John Mrema, ameelekeza mapambano yake dhidi ya CHADEMA, na siyo dhidi ya sheria, kanuni na mifumo gandamizi ya uchaguzi. Mrema anasema kuwa watu ambao wamekuwa wakifa wakati wa uchaguzi ni wachache kuliko wale ambao watakufa wakati wa kuzuia uchaguzi. Kwake yeye, ni aheri watu waendelee kufa kidogo kidogo kwente chaguzi batili kuliko kupambana mara moja, halafu mkapata mifumo ya haki ya kusimamia uchaguzi ifakayoondoa hatari zozote za watu ama kuuawa, kuumizwa au kuonewa wakati wa uchaguzi.
Watanzania, wamepoteza muda wao mwingi ndani ya CHADEMA ya akina John Mrema, wakijua wanapigania haki, kumbe yumkini waliowatangulia mbele ni mamluki dhidi ya mapambano ya haki.
Mungu yu mkuu. Amewafichua na kuwaanika mamluki wote. Sasa kuna uwezekano mkubwa mapambano dhidi ya wadhulumaji wa haki na demomrasia, yatafanikiwa.
Mod, tafadhali naomba urekebishe kichwa cha mada kisomeke .... Uchaguzi...na siyo ....Uchaguziji..