John Malecela amefikisha miaka 90, Cleopa Msuya amshauri aandike kitabu cha maisha yake

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,968
30,314
MZEE JOHN MALECELA AMEFIKISHA MIAKA 90 MZEE CLEOPA MSUYA KAMSHAURI AANDIKE KITABU CHA MAISHA YAKE TANZANIA IFAHAMU MCHANGO WAKE MKUBWA KATIKA UTUMISHI WA UMMA

Nimeangalia video ya Mzee Malecela aliyepata kuwa Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Waziri Mkuu akisheherekea miaka 90 nyumbani kwake Dodoma.

Katika video hii aliyepata kuwa Waziri wa Fedha na Waziri Mkuu Mzee Cleopa Msuya alisimamishwa kumzungumza Mzee mwenzake John Malecela.

Kote katika mazungumzo yake alikuwa akimtaja Malecela kwa jina lake moja la kwanza, ''John.''

Katika yote aliyosema ya kuvutia na kukumbusha historia ya utumishi wa John Melecela na vipi akumbukwe nimekamata moja na hili alilisema mwisho.

Mzee Cleopa Msuya amemwambia Melecela aandike kitabu cha maisha yake.

Nimekuwa na kawaida siku hizi kila ninaposoma lolote kuhusu viongozi wetu basi mimi huingia Maktaba kuangalia mimi nimeandika nini kuhusu yeye na kisha hukaa chini kitako kujiuliza yapi mengine nayajua lakini sikuyaandika?

Wakati mwingine ninayokutananayo Maktaba hunishtua pakubwa.

Nimeshtuka kuwa John Malecela sikumtaja popote katika kitabu cha Abdul Sykes.

John Malecela hayumo katika kitabu cha Abdul Sykes kinachoeleza harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika.

Nimejiuliza kwa nini na nikapata jibu.

John Malecela hayumo ndani ya kitabu cha Abdul Sykes kwa sababu baina ya mwaka wa 1957 hadi 1959 John Malecela alikuwa masomoni India.

John Malecela alirudi nchini mwaka wa 1959 TANU imevuka Kura Tatu inasubiri kupewa serikali ya ndani maarufu kwa jina, ''Madaraka,'' 1960 na uhuru kamili 1961.

Lakini si kweli kuwa John Malecela hayumo ndani ya kitabu cha Abdul Sykes.

Tarehe 27 Aprili, 1985 Julius Kambarage Nyerere, sasa akijulikana kama Baba wa Taifa, katika sherehe kubwa katika viwanja vya Ikulu, alitoa jumla ya medali 3979 kwa Watanzania waliochangia katika maendeleo ya taifa.

Balozi Abbas Sykes alipata kunieleza kuwa John Malecela ndiye alikuwa mwenyekiti wa kamati ya kupitisha majina.

Balozi Sykes anasema kuwa John Malecela alijadili majina haya na Mwalimu Nyerere na akamweleza Mwalimu kuwa yeye kama Mwenyekiti anaona kuna kasoro kubwa katika orodha ile kwa kukosekana kuwapo majina ya wazalendo waliompokea yeye Mwalimu alipofika Dar es Salaam mwaka wa 1952 na pamoja wakaunda chama cha TANU.

Orodha ile haikubadilishwa.
Ikapita kama ilivyotayarishwa na wajumbe wa kamati.

Natamani sana Mzee John Malecela aandike kitabu cha maisha yake atuhadithie kipande hiki cha historia.

Na yapo mengi nimeyakuta Maktaba yanayomuhusu John Malecela ambayo kwa hakika ningependa sana ayazungumze katika kumbukumbu zake endapo atajaaliwa kuandika.

1714234350316.png

1714234386227.png
 
Usipoandika historia yako basi usubiri kuandikiwa.

Yani huyu Mzee Malecela amezidiwa akili na mtoto wake wa kumzaa Le Mutuz ambaye ameandika historia yake ya American experience kabla hajafa?

Nahisi huyu Mzee untold history yake itakuwa na makandokando mengi yanayompa uvivu wa kuandika historia yake.

Wacha aandikiwe na ikulu tu.
 
Kuna harufu ya upotoshaji,eti alikataa orodha ya wanaostahili kupewa medani,ila mwalimu akapitisha kwa lazima,acha uchonganishi wewe mzee,kama hujui jambo acha uzushi kwa stori zako za kusimuliwa na thirdparties.

Acha aandike kitabu chake atasema vyema sio kumsemea.
 
Usipoandika historia yako basi usubiri kuandikiwa.

Yani huyu Mzee Malecela amezidiwa akili na mtoto wake wa kumzaa Le Mutuz ambaye ameandika historia yake ya American experience kabla hajafa?

Nahisi huyu Mzee untold history yake itakuwa na makandokando mengi yanayompa uvivu wa kuandika historia yake.

Wacha aandikiwe na ikulu tu.
Mzee mmoja mbinafsi tu namuonaga sana sana kwa wananchi wake wa huko mvumi-mtera

Ova
 
Back
Top Bottom