Mr Dudumizi
JF-Expert Member
- Sep 9, 2020
- 7,731
- 14,085
Habari zenu wanaJF wenzangu, ama baada ya salam zangu kwenu, ningependa kuendelea na mada yangu nzuri hapo chini.
Wakuu kwa wale wajuzi wenzangu wa mambo mbali mbali yanayoendelea duniani, nafikiri mshawahi kuusikia ule msemo unaosema kuwa "Paka akitoka, akiondoka au kuondolewa sehemu, basi Panya hutawala".
Msemo huu umedhihirishwa na kile kinachoendelea sasa nchini Tanzania. Nakumbuka mwanzo kabisa mwa mwaka jana, rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mhe Samia Suluhu Hassani aliruhusu ufanyaji wa mikutano ya hadhara kwa vyama vyote. Kwa masharti kwamba mikutano hiyo ijikite zaidi katika hoja za msingi, na sio matusi, ugomvi, wala vurugu.
Baada ya tamko hilo, vyama vyote vya siasa vilifurahi, na kujipanga kwa ajili ya kuzunguka nchi nzima kufanya mikutano mbali mbali.
1. CUF kilifanya mkutano wake mmoja tu pale Magomeni kikiongozwa na mwenyekiti wao Prof Ibrahim Lipumba kikaangukia pua na kuacha kabisa kuendelea na mikutano.
2. ACT Wazalendo wao nguvu yao wakaielekeza huko Zanzibar baada ya kugundua kwamba bara hawana uungaji mkono kutoka kwa watanzania bara, maana hoja zao zinajikita zaidi kuipigania Zanzibar badala ya Tanzania yetu yote.
3. Hawa walikuja na mikwara mizito, mwenyekiti na makamu wake wakagawana mikoa ya kuzunguka. List ikatengenezwa. Ikawa mwenyekiti huku, makamu kule. Ikafika kipindi mpaka mwenyekiti akaja amelewa kule Mwanza na katika hotuba yake akajiita na yeye mwana CCM. So likafunikwa funikwa na chawa wake siku zikapita. Sipati picha kama kauli ile ingetolewa na mtu kama Mbatia.. moja kwa moja angeonekana ni mwana CCM alievaa ngozi ya upinzani butu ili kuwahadaa wapinzani wenzake. Lakini kwa vile kauli ile ilitamkwa na mwenyekiti wao basi hilo halikupewa sana voice likafunikwa lipite. Kuna msemo unaosema "kunya anye kuku tu, lakini akinya bata kaharisha".
Pilika za Chadema zikawa nyingi hadi tukaletewa na list ya mikoa watakayozunguka kufanya mikutano yao. Mwaka huo huo wakati Chadema na vyama vingine vikiendelea kuzunguka huku na huko kufanya mikutano yao wakiongozwa na viongozi wao kina Lissu na Mbowe. Ghafla raisi Samia akachafua hali ya hewa katika mikutano hiyo kwa kumteuwa ndugu Paul Makonda kuwa katibu mwenezi na itikadi wa CCM.
Uteuzi huo ulionekana kukinyong'onyesha Chadema na viongozi wake wote. Kwani ghafla mikutano ikasitishwa kuogopa aibu ya kulinganishwa muitikio wa watu katika mikutano ya kina Lisu na Makonda.
Mbowe akaanza kudai amenyimwa vibali vya kurusha ndege hewani, baada ya kuona Makonda amesema atamsaidia kupata vibali anavyotaka ili waendelee kupambana kwa hoja kupitia mikutano mbali mbali, mwenyekiti na makamu wake wakaamua kukaa kimya.
Huku wakimuacha Makonda anazunguka tu peke yake mkoa kwa mkoa. Tupo tuliokuwa tukihoji walipo viongozi wa vyama vya siasa waliokuwa wakipiga kelele mikutano ya siasa iruhusiwe, sasa imeruhusiwa baada ya kumuona Makonda wamekimbia. Wengine wakahisi huenda Makamu amesafiri au kuna mambo ambayo hakubaliani na viongozi wa nchi ndomaana muda wote alikuwa kimya hazunguki tena mikutanoni wala kuonekana hadharani.
Mwezi uliopita rais Samia kafanya mabadiliko ambayo yamemuondoa Makonda katika nafasi ya chama aliyokuwa nayo, na kumpeleka kuwa mkuu wa mkoa wa Arusha, hivyo hatokuwa anazunguka tena kama alivyokuwa anazunguka miezi kadhaa iliyopita. Ndo tunaanza kuwaona tena kina Lisu wanatoka mafichoni na kuanza kuzunguka huku na huko wakijua kwamba yule aliekuwa anawafanya wajifiche hawezi tena kuwasumbua maana ashapewa nafasi nyingine ambayo haiingiliani kabisa na yale wanayoyafanya sasa hivi.
Lissu badala ya kumshambulia rais Samia anatakiwa amshukuru kwa kumtoa Makonda kule alipokuwepo, na kumtupa kwenye ukuu wa mkoa, maana bila hivyo wangeendelea kukaa mafichoni kukwepa kuaibishwa na muitikio wa mikutano ya Makonda hadi 2025, ndo pengine wangejitokeza kupigania nafasi zao za ubunge, uraisi nk.
Sometimes tuseme tu ukweli hata kama ni mchungu.