Jumanne Mwita
JF-Expert Member
- Nov 18, 2014
- 516
- 1,348
UTANGULIZI:
SURA YA KWANZA
- UTENGENEZAJI SABUNI ZA MAJI
- SABUNI ZA KUNAWIA MIKONO
- SABUNI ZA CHOONI
- SABUNI ZA KUFULIA
- SHAMPOO
- UTENGENEZAJI SABUNI ZA MICHE
SEHEMU YA PILI
UTENGENEZAJI WA :
- BATIKI AINA ZOTE
- UTENGENEZAJI VIKOI
- SHANGA, HERENI, BANGILI
- UTENGENEZAJI ZURIA
UTENGENEZAJI VITAFUNWA
- MAANDAZI
- SKONZI
- KARANGA ZA MAYAI
- TAMBI
AINA ZA SABUNI.
- Sabuni za kunawia mikono
- Sabuni za usafi wa chooni
- Sabuni za kufulia.
- Sulphonic asid - Inafanana na asali
- Siless - Kuimarisha povu la sabuni,sabuni iwe imara
- Sodaash - Inang'arisha sabuni,kuongeza povu
- Formalinge - kuuwa bacteria, sabuni kukaa kwa muda mrefu.
- Rangi - Kuongeza uzito wa sabuni
- Maji -Kibebeo inabeba sabuni yote
- Griseline - Inarainisha ngozi, mikono
- Perfume -Inaleta harufu nzuri ya sabuni/
- Chumvi
- Maji lita 10 yaliyochujwa
- Sulphonic acid vijiko 3 vya chakule
- Koroga kwa dakika 5-15 kulia au kushoto
- Siless ½ lita weka kwenye mkoroho changanya koroga
- Formalinge kyiko 1 cha chakula koroga
- Griseline vijiko 3 vya chakula koroga
- Rangi ½ kijiko cha chai koroga /kijani/Bluu
- Sodaash vijiko 2 vya chai weka katika sabuni koroga
- Chumvi Robo 3 koroga pembeni mimina, endelea kukoroga chumvi inaleta uzito kwenye sabuni endapo itakuwa nzito zaidi ongeza maji koroga.
- Perfume weka vijiko 2 vya chakula koroga tayari kwa matumizi iache ipoe kwa masaa 2 na fungasha kwenye vifungashio.
SABUNI YA CHOONI
MALIGHAFI
- Maji lita 10.
- Sulphonic asid ½
- Siless vijiko 5 vya chakula
- Formalinge vijiko 5
- Chumvi ¼ ilo, kuongeza uzito
- Sodaash vijiko 4 vya chakula
- Rangi kijiko 1 cha chakula
- Perfume vijiko 2 vya chakula
- Weka maji lita 10.
- Sulphonic acid 1/2 lita.
- Siless - vijiko 5 vya chakula
- Formaline vijiko 5 vya chakula
- Rangi kijiko 1 cha chakula
- Chumvi 1/4 kilo
- Sodaash vijiko 4 vya chakula
- Perfume vijiko 2 vya chakula
NB: Funika acha kwa masaa 2 ipoe weka kwenye vifungashio.
- SHAMPOO
- MALIGHAFI
- SULPHONIC ASID - Inaongeza pavu
- SODAASH - Kukata asid
- MAJI
- SLESS - Huongeza povu na kung'arisha
- FOMALINE - Kwa ajili ya kuuwa wadudu
- GRYCELINE -Kuleta umafuta
- PERFUME/HARUFU NZURI YA KUNUKIA
- CHUMVI YA MAWE - Kuleta uzito.
SHAMPOO
Andaa ndoo au beseni na malighafi fuata mtiririko ufuatao:
- Maji lita 10
- Sulphonic asid vijiko 4 vya chakula
- Silesi ½ kg koroga kwa dakika 15
- Sodaash vijiko 2 vya chakula endelea kukoroga
- Griseline vijiko 5 vya chakula koroga
- Fomaline vijiko 4 vya chai
- Rangi ¼ kijiko cha chai (kijani,bluu)
- Chumvi ¼ koroga
- Kiini cha mayai 2 koroga pembeni na maji ya sabuni dk 15 changanya koroga
- Perfume vijiko 3 vya chakula
- Shampoo iwe nzito
- Funika Shampoo iache muda wa masaa 2 tayari kwa matumizi paki kwenye vifungashio tayari kwa kuuza.
UTENGENEZAJI SABUNI ZA MCHE
(sabuni za magadi au Gwanji)
1. Kuna sabuni ambazo zinaharufu (perfumu) na ambazo hazina.
-Povu jingi la kutosha
-Iwe haina mwasho
-Rangi (bluu)
-Iwe ngumu
-Iwe imara
-Iwe na shepu nzuri inayoweza kuvutia mteja.
2. MALIGHAFI
- Cost soda(itunzwe juu ya kitu kama mbao ukiweka chini inaganda
- Mafuta, Mbosa,(Mise), mawese,kolie,alizeti.
- Hydrogen peloc side - kugeuza mafuta, sabuni kuwa nyeupe ing'ae kuipa imara
- Sodiam silicate- kuondoa muwasho.
- Hydrometer- kifaa kinachotumika kupima kiwango cha joto kinatakiwa kiwe kuanzia nyuzi joto 28 hadi 30
- Meza hutumika kukatia sabuni
- Box, umbo la sabuni , box la mbao hutengenezwa kwa kufuata vipimo vya sabuni ni urefu, upana na kina .
- Kisu ,kamba, karatasi la nailoni kuzuia uji wa sabuni usivuje endapo box lina matundu.
MALIGHAFI
1. Mafuta lita 20
2. Maji yaliyochanganywa na costic soda lita 10
3. Bluu vijiko 6 vya chakula
4. Vaa glovus
5. Maxic/puani
6. Gamu boot.
JINSI YA KUCHANGANYA COSTIC NA MAJI
-Pima maji lita 10
-Cost soda lita 4kg
-Koroga maji na costic mpaka iyeyuke costic,
-koroga kwa muda wa dakika 40-45 kwa kutumia mwiko mrefu.
- ANGALIZO
-Hakikisha unakorogea mahali palipo na hewa ya kutosha costic ni hatari sana, hakikisha isikirukie wakati wa kukoroga pia hakikisha usishike kwa mikono mitupu kama imetokea imekudondokea bahati mbaya osha kwa maji haraka sana.
- HUDUMA YA KWANZA
-Baada ya kukoroga kwa dakika 40 - 45 utaiacha kwa muda wa masaa 24
- ANGALIZO
-Baada ya kupoa unachukua kipimo ambacho ni Hydrometer temprecher ni kipimo kinchopima joto hakikisha Hydrometer imesoma nyuzi joto 280,29 -30.
JINSI YA KUFANYA
- Andaa box la mbao
- Karatasi ya mpira ya bluu - mita 2 ½
- Ndoo kubwa 2 na dyaba.
- Chukuwa mafuta lita 20 unamimina kwenye ndoo kubwa, mafuta yaliyoyeyuka sio mgando.
- Chukua maji yaliyochanganywa na costic soda yenye nyuzi joto 30? unamimina kwenye ndoo yenye mafuta , unamimina kidogo kidogo huku mtu mwingine akiendelea kukoroga kwa kutumia mwiko mrefu, koroga kwa dakika 30 huku ukiwa unaandaa box umeliwekea karatasi ndani ya prastic /mpira. Baada ya dakika 30 kuisha utamimina uji uliokoroga kwenye box hilo. Baada ya kumimina utaweka rangi.
- Rangi ya bluu
- Rangi ya mafuta
- Chukua mafuta kidogo robo lita
- Pima vijiko 6 vya chakula vya rangi ya bluu
- Changanya na mafuta robo lita koroga mpaka ilainike pembeni.
- Changanya, mimina kwenye box lenye uji huku ukiwa na kibao kirefu kama fimbo una kata mistari ili kuweka mawingu.
- Acha ipoe kwa muda wa masaa 24 . Baada ya masaa 24 sabuni iko tayari kwa matumizi!.
• Beseni la plastic, ndoo
• Gloves, mask, mkasi,meza, mkaa, kuni
AINA ZA BATIKI
1. Kufinyanga
2. Kufunga
3. Kukunja
4. Box au Tofali
JINSI YA KUTENGENEZA
-Andaa kitambaa mita 3 kwa dizaini unayotaka
-Andaa maji ya moto
-Changanya sodium. Caustic, rangi na black fixcer gm 30 kwa mita 3 au 4
-Weka kitambaa chako kwenye mchanganyiko huo huku ukigeuza geuza kwa muda wa dakika 15
-Ondoa kitambaa chako kwenye mchanganyiko huo weka juu ya kamba
-Toa juu ya kamba weka kwenye beseni lenye maji baridi fua na suuza baada ya hapo anika juani.
-Kikikauka piga pasi tayari kwa kuuza.
BATIKI ZA BLEACH
MALIGHAFI
• Kitambaa cha plain wax 6 mita
• Blichi ya maji
• Maji ya kawaida
JINSI YA KUTENGEZA
• Chukua maji 1/2 kikombe
• Changanya nab rich vifuniko 3
• Hakikisha unachanganya vizuri na maji yanateleza baada ya kuweka brich.
• Funga kitambaa au nyunyiza sehemu ulizo funga au ulizolenga
• Acha dk 10 kisha fungua mafundo kama ulifunga na kama ulinyunyiza weka kwenye maji safi.
• Suuza kwenye maji ya baridi kasha anika kivulini.
• Piga pasi tayari kwa kuuza
NB: Batiki zipo za aina nyingi waweza kutengeneza Batiki za printi kwa kutumia mishumaa na kugonga maua mbalimbali kwa kutumia vibao.
UTENGENEZAJI VIKOI
MALIGHAFI
• Vikoi
• Shanga (rangi, bluu,nyeupe, nyekundu, njano n.k.)
• Uzi
• Mkasi
• Sindano (spesho kwa ajili ya kutungia shaga)
• Vitambaa kwa ajili ya kuchorea picha za wanyama mbalimbali Kiberiti cha gesi.
JINSI YA KUTENGENEZA
- Andaa kikoi kwa saini unayotaka
- Fumua pande mbili ili kusokota kikoi (urembo)
- Sokota kwa kufuata saizi moja ili kuleta mlinganyo sahihi wa urembo wako.
- Tunga uzi kwenye sindano
- Ingiza shanga kwa rangi ulizokusudia na anza kushona kwa kuchoma juu juu ili kuzuia uzi kuonekana kwa ndani.
- Unapomaliza choma sehemu za nyuzi zilizojitokeza kwa kutumia kiberiti cha gesi pia waweza kubandika picha za wanyama kwa kudalizi ukipenda.
- Panga shanga kwa mahesabu (kuhesabu ili kuleta mchanganyiko mzuri wa rangi ulizokusudia .
- Sindano za shanga ni nyembamba sana, tunza vizuri tumia kwa uangalifu kuepuka kuvunjika kwa sindano
- Unapochora michoro ya maua, tumia chaki ili kukusaidia kuona vizuri wakati wa kushonelea shanga pia unapobandika picha za wanyama weka alama kwa kutumia chaki nyeupe.
MALIGHAFI
-Sindano
-Uzi Shanga (mbalimbali)
-Waya uliojikunja kwa ajili ya kutungia shanga
-Nozo
-Mkasi
UTENGENEZAJI WA ZURIA
MALIGHAFI
- Sindano (spesho)Mfuko wa gunia safi
- Mkasi
- Uzi
- Maorkapen (kwa ajili ya kuchorea maua).
SEHEMU YA TATU
UTENGENEZAJI WA VITAFUNWA
MAANDAZI
- Ngano 1kg
- Sukari ¼ kg
- Baking powder kijiko kimoja cha chakula
- Amira kijiko 1 cha chakula
- Rangi ya chakula kijiko 1 cha chai Mafuta kiasi kwa ajili ya kukandia
- Chumvi kidogo (ukipenda)
- Vanila ukipenda yanakuwa na radhi nzuri.
- Umua Amira pembeni kwenye kikombe iumuke
- Changanya vitu vyote anza kukanda kanda mpaka unga wote uchanganyikevizuri na usiwe mgumu sana.
- Baada ya kukanda vizuri, funika kwa karatasi ya nailoni au chombo kikavu uumuke kwa muda wa dakika 20.
- Weka kwenye meza anza kusukuma bonge la unga liwe mfano wa umbo la chapatti katakata kwa saizi unayotaka.
- Andaa kikaango moto wa wastani ili mandazi yaive bila kuungua.
MALIGHAFI
- Ngano kilo 1 kg
- Amila kijiko 1 cha chakula
- Mayai 2
- Maziwa 1/4 kikombe (ukipenda)
- Sukari vijiko 4 vya chai
- Chumvi kidogo.
- Umua Amila
- Gonga mayai kwenye bakuli pembeni pigapiga kwa kijiko yachanganyikane vizuri.
- Changanya vitu vyote na anza kukanda mpaka unga uchanganyike vizuri.
- Weka maziwa ya uvuguuvugu yaliyochanganywa na maji, weka maziwa kidogo kidogo huku ukiendelea kukanda unga.
- Kata mabonge mabonge kama ya chapati.
- Andaa sufuria, paka mafuta ndani.
- Weka mabonge,funika na mfuniko wa bati acha yaumuke
- Baada ya kuumuka weka kwenye jiko moto chini wa wastani juu weka mwingi kiaisi. Kuhakikisha kama zimeiva choma kijiti ukiona unga haung'anganii basi zitakuwa tayari
- Acha zipoe kwa muda, weka kwenye vifungashio au tumia kwa kula.
MALIGHAFI
- Mayai - 2
- Sukari - 1/4 kg
- Ngano -1/4 kg
- Karanga - 1 kg
- Mafuta ya kula (kupikia)
- Andaa bakuli gonga mayai changanya na sukari koroga weka chumvi kiasi koroga hakikisha sukari na chumvi vimeyeyuka.
- Weka karanga ulizochambua vizuri ndani ya bakuli lenye Mkorogo huo kisha nyunyiza unga wa ngano kidogokidogo hakikisha kila punje ya karanga imepata rojo na unga wa ngano.
- Andaa sufuria au karai weka mafuta yachemke moto wa wastani tumbukiza karanga zichemke katika mafuta hakikisha zinaiva na kuwa rangi kahawia zisiungue ipua na wekakwenye chombo chenye matundu (chujio) ili kuchuja mafuta.
- Acha zipoe, tayari kwa kuliwa au kuuza.
TAMBI MAHITAJI
- Unga wa dengu 1kg
- Baking powder kijiko 1 cha chakula
- Pilipili mbuzi 1 kama utapenda
- Chumvi
- Pilau masala ya unga kijiko 1 cha chai
- Mashine ya kutolea tambi.
- Jiko, mafuta , sufuria , karai .
- Kanda mchanganyiko wako kupata uji mzito kwa kutumia mikono hakikisha wote umechanganyikana vizuriAndaa jiko mafuta yaive kwa wastani
- Weka unga kwenye mashine ya tambi anza kuzungusha mashine
- Hakikisha unaweka tambi kiasi ili ziweze kuiva vizuri na tumia karai au sufuria iwe pana.
- Tambi zikiiva weka kwenye chujio mafuta fungasha peleka sokoni.
HITIMISHO
Asante kwa kusoma maelezo ya namna ya kutengeneza sabuni za maji n.k. Hakikisha wewe unayesoma zingatia hatua zote katika ujifunzaji . Mungu akuzidishie Baraka tele zenye mafanikio THUBUTU UTAONA MAFANIKIO.
Hakimiliki©2022 Jumanne255 Haki Zote Zimehifadhiwa. Makala hizi hutolewa kwa ajili ya kuboresha maisha yako. Ruksa "kushare" na usibadili kitu chochote bila ya idhini/ruhusa ya mwandishi.