JF Exclusive: The Buzwagi Contract

Yaani hii management fee itakuwa badala ya kodi!

4.6 Where 5% ( or in the case of management fees, a rate up to 15%, if applicable) of the gross payment for technical services or management fees is withheld, sums so withheld shall be deemend to satisfy the liability for income tax of the person providing the technical services or management services so far as it relates to the gross payments received.

yaani technical services or management services ndizo zipi?
 
Mkataba umeboreshwa na hawa ndiyo wataalamu tunaowategemea mimi nimekosa imani. Hivi wanasheria walio kwenye wizara zetu hapa ndipo wamejitahidi kweli? Mimi siwezi kuwaelewa.

Na pili hivi mikataba tangu lini ukafutwa? Hata mkataba wa kupanga chumba pale manzese kabla ya kusainiwa huwa mnafanya marekebisho yote na kutoa final draft ambayo ndiyo husainiwa.

Na hivi labda hapa naomba nielimishwe hata mikataba ya mikopo tunayosaini benki huwa ina mwangalizi, Inakuwaje mkataba mkubwa ulio na maslahi ya taifa uwe hivi? Hapa jamani mimi sheria sihijui lakini naona hii ni local sana.

Katika utaalamu ukiambiwa hapa ndo wamejitahidi, mimi ningelikuwa na uwezo ningeunda tume ya kuchunguza elimu za waliohusika katika kuandaa mkataba huu, labda kama nao uliandaliwa sehemu uliposainiwa. Maana unaweza kuwa umeishapata moja baridi ukasahau kabisa baadhi ya majukumu.
 
Naona SWAM INTELLIGENCE imefanya kazi yake.
Yuko mtanzania au watanzania walioona heri lawama kuliko fedheha wakautolea uvivu mktaba kiasi kwamba kila mtanzania sasa ana kopi yake.
Wana JF zindisheni mapambano kazi muifanyayo si Bure. Mitutu yenu ya Key Board imeanza kuwaliza Mijibaba na Mijimama ya SISIEMU.
Wawezavyo kusitiri kwa uhakika kama siri ni nyuchi zao tu, mengine yote si siri tunaanika hadharani

OMBI LANGU.
Ikiwezekana mikataba yote ije hapa kilingeni tuone JK na serikali yake ni wagonjwa kiasi gani.

Mzee MWKJJ tuletee hiyo kopi ya Sheria ya Madini kama iko kwenye Soft Form.

Hongera Mwafrika wa kike kwa kuchambua hoja kwa hoja.

Kaka Mcha angekuwepo hapa kijiwe kingemix kweli, kwani tungembana mbavu vizuri.
 
Yaani hii management fee itakuwa badala ya kodi!


4.6 Where 5% ( or in the case of management fees, a rate up
to 15%, if applicable)of the gross payment for technical
services or management fees is withheld, sums so
withheld shall be deemend to satisfy the liability for income
tax of the person providing the technical services or
management services
so far as it relates to the
gross payments received.



yaani technical services or management services ndizo zipi?

SOMA ARTICAL YANGU HAPO JUU NDIO HAO WANAOITWA EXPATRIATES.


'Expatriate Employee' means a person not normally resident in Tanzania and who is engaged under a contract subject to the grant of a resident Permit...........................
 
Naona SWAM INTELLIGENCE imefanya kazi yake.
Yuko mtanzania au watanzania walioona heri lawama kuliko fedheha wakautolea uvivu mktaba kiasi kwamba kila mtanzania sasa ana kopi yake.
Wana JF zindisheni mapambano kazi muifanyayo si Bure. Mitutu yenu ya Key Board imeanza kuwaliza Mijibaba na Mijimama ya SISIEMU.
Wawezavyo kusitiri kwa uhakika kama siri ni nyuchi zao tu, mengine yote si siri tunaanika hadharani

OMBI LANGU.
Ikiwezekana mikataba yote ije hapa kilingeni tuone JK na serikali yake ni wagonjwa kiasi gani.

Mzee MWKJJ tuletee hiyo kopi ya Sheria ya Madini kama iko kwenye Soft Form.

Hongera Mwafrika wa kike kwa kuchambua hoja kwa hoja.

Kaka Mcha angekuwepo hapa kijiwe kingemix kweli, kwani tungembana mbavu vizuri.

Hiyo hapo ndiyo sheria ya Madini ya 1998. Angalia kwa kina eneo la "Development Agreement) Kifungu cha 10 na sehemu ya Financial provisions kwenye Ibara ya 4..
 
Mazee Geeeeze!

Saafi mkuu weka vitu mkuu, vipi mkuu wangu salama kabisaaa? Tunahitaji wananchi wasioogopa sasa kazi mchezo umekwisha, huo mkataba uwekwe popote inapowezekana, tena ikibidi tuanze kuwatumia kina Karamagi wenyewe waule, au wautupe lakini wajue kuwa tunao!

Saafi sana Mazeee!
 
Huu Mkataba tuliambiwa kuwa ni "mkataba uliofanyiwa marekebisho makubwa sana" na wataalamu wetu waliobobea katika fani hiyo.

Au nakosea jamani?
 
Ndiyo tuliambiwa.. lakini haina maana kuwa ndivyo ulivyo.. nakumbuka waliwahi kutuambia kuwa ndege yetu inapaa.. na hivi karibuni wametuambia kuwa tunagawana kasungura fulani hivi..
 
Huyu jamaa sio ngumbaru ilikuwaje afanye madudu kama haya? Shinikizo? Kutoka kwa nani? .............................
 
4.3 Local Government rates and taxes shall not be:

4.3.1 in excess of those generally applicable on Tanzania, or

4.3.2 based on profit, turnover, sales or output from mining operations, or

4.3.3 based on the value of land used for the mine, mining
infrastructure or installations,

provided that the aggregate of such local Government rates and taxes charged shall not exceed United States Dollars Two Hundred Thousand (US$ 200,000) in any one calendar year.

Halafu hawakutilia maanani hata ongezeko la bei ya dhahabu katika soko la Dunia! Wao wataendelea kutulalia hata ounce moja ya dhahabu ukifika $3,000 huu ni wizi dhahiri na hauwezi kukubali katika nchi yeyote hapa duniani.
 
Huyu jamaa sio ngumbaru ilikuwaje afanye madudu kama haya? Shinikizo? Kutoka kwa nani? .............................

Shinikizo toka kwa Barrick (I guess na tumbo lake pia). It is just that simple.

Soma tena huo mkataba na utagundua kuwa ulikuwa drafted, reviewed na represented by Barrick. Karamagi ame-initial na kutia saini tu. Mzee saini hapa na hapa.........
 
Halafu hawakutilia maanani hata ongezeko la bei ya dhahabu katika soko la Dunia! Wao wataendelea kutulalia hata ounce moja ya dhahabu ukifika $3,000 huu ni wizi dhahiri na hauwezi kukubali katika nchi yeyote hapa duniani.

Bubu,

mambo mengine hata yanatia aibu kuyasema.....
basi tu......
 
Sasa kama huu sio uhujumu uchumi ni nini? Huyu waziri siyo tu kwamba anastahili kufukuzwa kazi. Anastahili kufungwa jela.
 
Mie kama ningekuwa Karamagi saa hii ningekuwa nimelazwa kwa shinikizo la damu!!!. Lakini hili "rijamaa" linadundika tu kama vile business as usual.......hawa watu kweli si wenzetu na inabidi kwenda extra miles na huu ni mwanzo mzuri.
Hongera tele kwa JF!!. Give 'em hell! Piga pale panapo uma kwa sana.
 
Wanachama wenzangu wa JF,
Naanza kwa kuwapa hongera kemkem kutokana na jinsi mnavyomwaga ukweli wenye kuuma pande zote. Baada ya hapo nawaombeni samahani sana kwa kutoweka bila kuaga; wakati mwingine mihangaiko ya maisha haitabiriki. Nimefurahi kukuta mijadala kemkem kibao inaendelea hapa kijiweni. Bado nipo hapa Dar nilipokuja kwa muda mfupi kwa mambo ya kifamilia, jana nilipata bahati ya kukata kinywaji na rafiki zangu wachache ambao wana nyadhifa kubwa serikalini. Nilishangaa sana kugundua kuwa wanaiogopa sana Jambo Forum to death. Wanasema inatoa vijembe vikali ambavyo wakati mwingine huwa vinahusu mambo waliyoshiriki katika kufanyia maamuzi. Nilichojifunza ni kuwa vijembe vya hapa kumbe kweli vinawafundisha adabu baadhi ya vihgogo wetu.

Kwa hapa mtaani nimefanikiwa kupata nakala ya mkataba wa Buzwagi, na kweli kile ni kichekesho kabisa wala siyo mkataba unaweza kuwa umeingiwa na serikali ya watu wenye akili zao. Inawezekana mmekisha ujadili mkataba huo hapa , lakini nitarudi na uchambuzi wangu kipengele kwa kipengele kupitia articles zote 18 ambazo nyingi zinaweka masharti ya kuinufaisha kampuni tu wala wala hakuna masharti ya kuinufaisha serikali. La muhimu ni kutambua kuwa mkataba ule siyo binding kabisa na unaweza kupingwa mahakamani kwa vile hauna "Seal ya Serikali ya Tanzania," na wala hakuna shahidi independent aliyethibistha kuwa ulisainiwa kihalali bila kulazimishana kwa vitisho. Mtu yeyote anaweza kuandika document kama hiyo na kudai kuwa ni mkataba wa serikali.
 
vipengere vifuatavyo vinaweza kukusababisha uombe Karamabhi apigwe na radi bure....

4.7 The company shall be allowed to deduct 80% of capital expenditure in the year incurred, thereafter at 50% per annum on declining balance method, provided that the Government shall have made legislative changes to ensure that this provision is applicable under the laws of Tanzania
Kwa wale mliosoma very simple accouting kama AC 100 au the like, jamaa wanaamua wao ni njia gani ya depreciation watumie.... hii ina maana kwamba kila mwaka wakipata faida.... wanaweza kuifuta faida yote kwa kusingizia kuwa wamefanya capital expenditure na hivyo wanahitaji 80% itolewe kwenye faida kabla ya kulipa kodi..ooooppssss nimesahau kuwa jamaa hawalipi kodi kutokana na faida! ..... my bad

4.8 The purchaser of any mineral products produced from the Contract Area shall not be obliged to withhold any amount from the purchase price.
Hapa jamaa wana-dictate hata kile mnunuzi wa hayo madini atafanya... e bwana hawa jamaa wana-kiburi sijui wamekitoa wapi.

Na huyu JK ambaye anasifiwa kuwa ni safi amesoma hapa?
 
Huu Mkataba tuliambiwa kuwa ni "mkataba uliofanyiwa marekebisho makubwa sana" na wataalamu wetu waliobobea katika fani hiyo.

Au nakosea jamani?

Hivi si kuna wakati Muungwana, alikwenda kutafuta wataalamu wa mikataba huko ma-Norway au?
 
Back
Top Bottom