JF Exclusive: The Buzwagi Contract

Ninajua kuna thread inaendelea ya namna ya ku-download mkataba kwa wale watakaofanikiwa ila ninauliza kama ni vyema kuweka hapa vipengere vya mkataba vikajadiliwa na wale wenye utaalamu wa maneno ya kisheria....

Kwa leo nitaweka kipengere cha 4 kinachohusu pesa hapa na baadae nitaweka vingine au kama kuna mtu anataka anaweza kuweka hizo parts zingine!

Katika uk wa saba (7) wa mkataba wa buzwagi... kuna hili:

ARTICLE 4 FISCAL TERMS



Kipengere cha 4.2 kitaendelea hapo chini
 
4.1.3 for each year of production the amount of US$ 125,000
by 31st December of each calendar year a contribution
to the Empowerement Fund

Kipengere cha 4.2 kitaendelea hapo chini

Kwenye mojawapo ya matatizo ni matatizo ya kipengele hicho. Hivi Empowerment Fund imeanzishwa kwa sheria gani? Sheria ya Madini ya 1998 haina mahali inapozungumzia mfuko huu na misingi ya uchangiaji wa mfuko huu. Hilo kwanza.

Pili, walipoamua kuweka kiasi cha dola 125,000 kwa mwaka walitumia kigezo gani cha kuchagua kiasi hicho? Kwanini isiwe 50,000 au 500,000? Kwanini iwe "for each year of production" ina maana wanapoanza kutangaza faida (wakisharudisha mtaji wao?) au hata kama wakizalisha tani moja tu kwa mwaka? What is the basis of this amount?
 
article 4 inaendelea hapa....


maneno yanayofade yamefutwa kwa mkono na kuna sahihi pale!

4.3 itaendelea
 
4.1.3 for each year of production the amount of US$ 125,000 by 31st December of each calendar year a contribution to the Empowerement Fund

Mzee MMJ,

Heshima mbele, Empowerment Fund exactly ni nini as far as taifa letu is concerned? Nani anayepewa hizo Funds, na anzipeleka wapi akishapewa? Je huwa tuna vitu vya namna hii kwenye mikataba mingine ya zamani? Huwa ni kwa faida ya nani? Je kuna any refference za kuback up any claim za hii kitu ya Funds?

I mean just being curious, akma unajua naything au kuna yoyote hapa forum mwenye an idea?
 
FMES... hilo ndilo swali, kwani hadi hivi sasa sijaona mahali popote ambapo mfuko huo ulianzishwa kisheria na kama unahusiana na madini tu au na mambo mengine. Nimeipitia sheria nzima ya madini na sijaona suala la empowerment au fund.
 
Kwa hiyo hii Empowerment Funds, inaweza kuwa inaingia mifukoni mwa wajanja, halafu wanasomeshea watoto wao nje?

Maana siumeiona inasema amount in dollars na wala sio hela zetu madafu!
 
Hii hapa ndio kali kwa zote

article number 4 inaendelea kutoka ukurasa wa 7 kwenda wa 8.


Yaani jamaa wanatupangia hata kodi ya kutulipa ... na wanasisitiza kuwa hiyo kodi haitajali mauzo, faida or anything
 
Kwa hiyo hii Empowerment Funds, inaweza kuwa inaingia mifukoni mwa wajanja, halafu wanasomeshea watoto wao nje?

Maana siumeiona inasema amount in dollars na wala sio hela zetu madafu!

Ndiyo hapo, kwa sababu ukiweka in dollar inaonekana kidogo.. lakini ukiiweka kwenye hela ya madafu inabadiliza kibanda kizuri tu cha mtu. Najua tumeanzisha Constituency Development Fund (Mfuko wa Maendeleo ya Majimbo) ila sidhani kama ni kitu kile kile.
 
USD 125 000 Empowerment fund may be za kutengeneza mabilionea 100 wa JK!!!!!!!
 
Sorry, there are currently no free download slots available on this server.

Please try again later, or you can upgrade to FileFactory Premium for instant access.
-Kweli wameunyofoa ...
 
Hayo mambo ya empowerment fund hata kwenye uanzishwaji wa PSRC wakati wa privatisation wa SUs yalikuwapo. Nia ya fund hiyo ilikuwa ni kuwawezesha wazawa (walalahoi?) kuyanunua mashirika yaliyokuwa yakiuzwa.

Kisichoeleweka ni kuwa hiyo fund ilianzishwa au la; na kama ilianzishwa, ni kiasi gani kilikusanywa; na ni wazawa wangapi walifaidika nazo; majina yao ni kina nani na vilevile, kiasi ambacho hakijatumika na kitatumika vipi.
 

Kifungu hicho ni mojawapo ya vifungu ambavyo ningekuwa miye Rais ningeshamtimua huyo Waziri na wale wote walioandika huo mkataba. NI wazi kuwa kipengele hicho hakikuuingizwa na Karamagi kule London.

Kwa wale wanaofahamu mambo ya kodi wataelewa kuwa kodi zinalipwa kutokana na misingi fulani fulani, kwa mfano kodi ya kichwa (inalipwa na kila mtu aliyefikisha umri huo na ana uwezo), kodi ya asilimia ya mauzo (sales tax - kwa kiasi unachonunua ndivyo kodi yako ilivyo mara nyingi iko fixed); kodi ya mapato (ambayo inaweza kuwa fixed au kulingana na mapato). n.k Hivyo kila kodi inamsingi wake.

Sasa unapoandika kwenye mkataba kuwa kodi haitakuwa based on
"profit, turnover, sales or output from mining operations, or based on the value of land used for the mine, mining
infrastructure or installations".
Kuna uwezekano mmoja tu katika dunia nzima.. kwamba zimekuruka!!! Sasa kama huweki msingi wa kodi utakuwaje, haiwezekani ufikie mahali na kusema kama mtu aliyelewa gongo

"provided that the aggregate of such local Government rates and
taxes charged shall not exceed United States Dollars Two Hundred
Thousand (US$ 200,000) in any one calendar year"
kwamba majumuisho yote ya kodi (isiyo na msingi wowote) hayatazidi Dola laki mbili kwa kalenda ya mwaka mzima. Kama hauna msingi wa kodi (tax base and method) unaweza kufikia vipi hitimisho kuwa kiasi cha kodi hakitazidi dola laki mbili?

Swali kwa Waziri Karamagi:
Kama kodi itakayotozwa Buzwagi haitatokana na faida, marejesho, mauzo au uzalishaji wa mgodi, au isiyotokana na thamani ya ardhi ambapo mgodi huo upo, miundombinu au majengo na vifaa vilivyowekwa hapo; na kama kodi hiyo itakapojumuishwa isizidi dola laki mbili kwa mwaka, ni msingi gani basi mtatumia kukusanya hiyo kodi? Unless you set up a flat tax!! If you do so, then you'll have confirmed to the world your untreatable insanity!
 

Thats right dude, give dem pressure.
We ain't gonna be fools no more,
in dis abundance of water we ain't gonna be thirsty again
in dis ocean of resources we ain't gonna be poor again!!
We gonna "mkoma nyani" untill he returns the children's banana
 
..upuuzi mtupu wakubwa na hao ndio wataalam wetu wametengeneza na wakubwa wanausifia kabisa
 
Hivi ni kwanini hizo funds /rates zinakuwa fixed kwanin isiwe % fulani ya mapato. Ina maana hata wakizalisha zaidi we are not gaining more!
Ila Mzee Kara kaniacha hoi....kufuta pale...duh..hii kweli bongo!
Please educate me angeiacha hiyo clause ingekuwa na implication gani???
 

Mama Lao ingegongana na hicho kipengele nilichochambua hapo juu kwani kodi ingetozwa kufuatana na mojawapo ya vitu hivyo. Sasa huwezi kuwa na vipengele vinavyopingana kwenye mkataba mmoja and he decided to take the path of least resistance.
 
Invisible,
Mimi niliupata jana. Lakini sikusave kwenye desktop yangu. Sasa marafiki zangu wananiomba nakala ndiyo nimeshindwa kuwatumia.
Lakini ninayo printed version
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…