Mzalendo Uchwara
JF-Expert Member
- Jan 26, 2020
- 4,356
- 13,684
Mkuu unayo hoja ya msingi kabisa. Lakini ni lazima turekebishe muungano.
Kuna sababu inayosababisha wapokwe ushindi, kwa nini wapinzani wa serikali ya mapinduzi wawe na kufanana kwa ethnic moja?Hawapokwi ushindi kwa sababu wana asili ya kiarabu bali ni kwa sababu wao ni wapinzani. Hata bara CCM ikishindwa uchaguzi, itafanya yale yale inayofanya Zanzibar. Kwa mtazamo wangu, solution ya issue ya Zanzibar sio kufanya reconciliation ya mapinduzi bali ni kufuata sheria za uchaguzi. Chaguzi lazima ziwe free and fair.
No sihitaji reconciliation kwasababu tume move on, nimetolea mfano huo ili kuonyesha jinsi ukweli unavyoponya. Zanzibar wapindua na wapinduliwa wakae meza moja wasemezane ukweli, waombane msamaha na kupeana pole kuponya machungu ya mapinduzi.Teh teh teh 😃 😃 😃 kwa hiyo na wewe unahitaji 'reconciliation' Ili mkeo arejee kwako ?
No Sultan hakuwa mwakilishi wa mkoloni, Zanzibar was never colonized!, kwenye ule mkutano wa Berlin, wa mwaka 1884, Zanzibar, visiwa vyote vya bahari ya Hindi, na 10 miles costal stripe, vilimilikishwa kwa Siltan of Zanzibar. It is as if Zanzibar haikuwahi kuwa na mwenyewe, Sultani alitoka zake Oman mwaka 1732 akavikuta visiwa havina mwenyewe, akajiokotea kama embe dodo chini mwembe.Wow! Kumbe sultan hakuwa mwakilishi wa mkoloni?
CCM hawana msamiati wa kushindwa bwasheeWanabodi,
Makala yangu kwenye Nipashe ya Jumaoili ya Leo。
Leo Tarehe 12 January 2025, imedondokea siku ile ile ya Januari 12, 1964, ilikuwa ni siku ya Jumapili. Leo Tanzania inaadhimisha miaka 61 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, wakati Wazanzibari wengi wanashereheka kuyapongeza Mapinduzi hayo (na wengine hadi kuyapa utukufu kwa kuyaita Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, ambalo neno Utukufu, kwa dini mbili kuu, Wakristu na Waislamu, Utukufu ni kwake tuu na wake tuu, Mwenyeenzi Mungu, hivyo kuita kitu kingine chochote kitukufu ni kama kufuru!), kuna Wazanzibari wengine, japo wachache, siku hii ni siku ya kumbukumbu mbaya, kwa kuwapoteza wapendwa wao, kutokana na umwagwaji damu wa Mapinduzi hayo na baada ya Mapinduzi.
Hivyo makala hii ni swali Je Zanzibar Inahitaji Truth & Reconciliation Commission ili Kuponya Makovu ya Mapinduzi, ili Upinzani Ukishinda,Upewe?。Hili ni ombi kwa Sister wangu na Brother wangu,yaani Kaka mtu na Dada Mtu, Can You Please Do The Needfu?。
Hakuna ubishi kabisa, kuwa Mapinduzi ya Zanzibar, yameleta kheri, lakini ni ukweli mchungu pia yameleta shari iliyosababishwa na umwagaji damu mkubwa uliosababisha maumivu makubwa kwa waliopinduliwa ambao wanaishi na makovu ya Mapinduzi hadi leo!。
Kule kwenye mtandao maarufu kuliko mitandao yote ya kijamii nchini Tanzania, Jamii Forums, shamra shamra za kuisubiria siku hii, zilianza siku nying kabla kushamirishwa na Fake News kuwa Sultan mpinduliwa anarejea Zanzibar kufanya ziara rasmi na atahudhuria maadhimisho ya leo. December 28 lilipanda bandiko hili Zanzibar Kumpokea Sultan Jamshid: Ziara ya Kihistoria Baada ya Miaka 60 Uhamishoni
Hilo la Sultani kurejea mimi nikalidaka na kulitolea mapendekezo yangu kumi kwa SMZ.
Ndipo kaka yangu mmoja, kutoka Zanzibar, naomba kumtaja kwa jina moja tuu Kaka Chalz, ni kaka yangu alinipokea RTD, ile mwaka 2000, akatufundisha kazi ya utangazaji, hivyo tunawaheshimu sana kaka zetu hawa, na hata tunapokosea, hawaachi kutupigia simu kuendelea kutuongoza mpaka leo mpaka kesho, Asante Kaka Chale!.
Basi Kaka Chale akaniuliza una uhakika na chanzo chako cha habari kuwa hii ni habari ya kweli?, nikamjibu kwa vile imetangwa na Jamiiforums, kwa jina maarufu JF, ni chombo cha kuaminika, ingekuwa fake, JF inatumia mfumo wa Jamii Check kubaini fake news na kuzifuta, hivyo itakuwa kweli.
Ndipo nikaipitia ile habari kwa mara ya pili kuisoma source, nikakuta ni jamaa yuko Oman!, nikamtafuta kaka yangu mwingine Zanzibar huyu ni Mzee Salim Said Salim, mwandishi wa siku nyingi, tunamuita jina la Mzee SSS, yeye ana nasaba kidogo na ukoo wa Sultan, ukitaka kumtibua SSS, mwambie Mapinduzi Matukufu!. Salim akawapandia kwa simu, Oman, familia ya Sultan wakakanusha kuwa ni fake news!. Asante Mzee SSS!.
Ndipo nikawasiliana na Mkuu Maxence Mello, chapisho langu likaondolewa, na nikabandika chaousho jingine Story ya kurejea kwa Sultan wa Zanzibar ni Fake News! JF Tumelishwa Tango Pori!. Asante Kaka Chale kuniwezesha kuupata ukweli
ila chapisho la msingi halikuondolewa mpaka leo lipo. Nikamrudia Kaka Chale, nikamshukuru kwa angalizo lake, ila nikamwambia baadhi ya yale mapendekezo yangu 10, mengine ni valid, yafanyiwe kazi!. Baada ya hii fake news, jibu la familia ya Sultan alilotoa, ndilo likanijulisha bado kuna watu wana machungu na Mapinduzi yale.
Watu hawa wapoozwe!, waponywe!。 Na Baada ya ujumbe huo mkali kutoka Oman, masikini sultani akaitwa na Mola wake!TANZIA - Aliyekuwa Sultani wa Mwisho Zanzibar, Sultan Sayyid Jamshid Al Said, Afariki Usiku Huu, Omani, usikute ni hii fake news ya jf imemsababishia mtu kifo!。
Huu ni mwaka wa uchaguzi, na hakuna ubishi siasa za Zanzibar, licha ya uwepo wa SUK, bado zinaathiriwa na mzimu wa machozi, jasho na damu, zilizomwaika na kufukiwa bila kufanyiwa hitma, na kuna watu wana makovu ya machungu ya mapinduzi yale,wakija kushika madaraka,kuna watu watakoma!。
Hivyo matokeo ya baadhi ya chaguzi za Zanzibar, ni matokeo yale yale ya ule uchaguzi wa mwaka 1963. Mfano mzuri ni uchaguzi wa mwaka 2015, kuna msemo wa Kiingereza unaosema numba haziongopi!.
Matokeo ya NEC ya uchaguzi wa 2015 kwa Zanzibar, yamethibitisha pasi shaka kuwa uchaguzi wa Zanzibar wa 2015, kama usinge futwa, Maalim Seif Shariff Hamad wa Chama cha Wananchi CUF ndie angelikuwa mshindi wa uchaguzi wa rais wa Zanzibar kwa kutumia kigezo cha matokeo ya uchaguzi wa urais wa JMT, uliosimamiwa na NEC kule Zanzibar ambao uchaguzi haukuwa na dosari, katika uchaguzi huo, mgombea wa UKAWA, Edward Ngoyai Lowassa, alimshinda mgombea wa CCM, Dr. John Pombe Magufuli.
MGOMBEA KURA HALALI ASILIMIA
DR. JOHN POMBE MAGUFULI 194,317 46.5%
EDWARD NGOYAYE LOWASSA 211,033 50.50%
IDADI YA KURA HALALI 417,882
Hii maana yake Zanzibar upinzani unaweza kushinda, sasa kwa vile bado kuna hostilities za machungu ya Mapinduzi, siku upinzania ukishinda Zanzibar, kutaibuka kulipiza kisasi!.
Mwaka 2015 niliandika Iwapo CCM itashindwa Zanzibar, Nini Majaaliwa ya Muungano?
Nilishauri kisha nikashauri Kumuepushia aibu ya Kushindwa, CCM isimsimamishe Dr. Shein hili halikufanyika,na matokeo ndio yale ikabidi watu wafunike kombe。。。
The like scenario naiona Zanzibar 2025,hivyo nashauri
Hivyo nawashauri Dada yangu Rais Samia, na kaka yangu rais Dr. Mwinyi, kubalini kutibu makovu ya Mapinduzi, ili kuzimaliza siasa za hostilities, ikitokea upinzani umeshinda Zanzibar, hakuna haja kufunika kombe tena mwanaharamu apite, iwe ni kupokezana kwa amani na upendo. Miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar, Tuyaenzi kwa 4R za Rais Samia?, JMT Tuitendee Haki Zanzibar?, Tuwatendee Haki Wazanzibari? Mshindi Halali Apewe?
- Zanzibar ianzishe truth and reconciliation commission watu waruhusiwe to vent,hivyo to heal machungu ya mapinduzi。
- Decemba 10 iwe ni siku ya mapumziko ya uhuru wa Zanzibar,sio lazima iadhimishwe kwa shamra shamra,inaweza kubadili jina ikaitwa Sultan Day。
- Neno Matukufu kwenye Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,lisiendelee kutumika,yaitwe tuu Mapinduzi ya Zanzibar na vibwagizo Mapinduzi Daima, na Tutayalinda kwa gharama yoyote, tuachane nayo ili kuponya wapinga mapinduzi
- Falsafa ya 4R za Samia,itumike hadi Zanzibar,mshindi wa kweli wa uchaguzi wa Zanzibar atangazwe,mfano mzuri ni huu Elections 2015 - Imethibitishwa pasi na shaka kuwa ni kweli kabisa, Zanzibar, Maalim Seif na CUF ndio walioshinda na ili kumuondolea posibility ya aibu ya kushindwa,nimetoa ushauri hapa kwenye HII mada。
Namalizia kwa lile swali la msingi la uzi huu Je Zanzibar Inahitaji Truth & Reconciliation Comm。Kuponya Makovu ya Mapinduzi, ili Upinzani Ukishinda,Upewe?。Sis & Bro,Can You Please Do The Needful?。
Heri ya Mapinduzi.
Paskali.
Tribalism ni human nature. Hata South Africa kuna political parties za Africans, whites na Indians. Reconciliation haikuweza kuiondoa hii hali.Kuna sababu inayosababisha wapokwe ushindi, kwa nini wapinzani wa serikali ya mapinduzi wawe na kufanana kwa ethnic moja?
Umeishawahi kujiuliza kwa nini walioko madarakani wana slogans kama mapinduzi daima? Tutalinda mapinduzi kwa gharama yeyote?
Waliokimbilia Mombasa Kenya baada ya uchaguzi wa 2000 kwa nini wengi wana asili ya kipemba na kiarabu? Paskali ana point kuna jamii kubwa mbili Zanzibar zinazokinzana, hawaaminiani na hawapendani bila kukaa na kuweka tume ya reconciliation moto utaendelea kufukuta.
Ukizungumza kwa chuki dhidi ya hao wenye asili ya kiarabu na wapemba unakuwa kama hao wa mapinduzi daima wanaosema hawawezi kutoa nchi kwa kipande cha karatasi. Sheria za uchaguzi zikirekebishwa na ACT wakashinda uongozi wa serikali kuna uwezekano mkubwa na wao wakaanza intimidation dhidi ya mapinduzi daima.
Hili suala halihitaji emotion ya wale waarabu, wakoloni etc, ni suala la kuponya jamii ya wazanzibari from their past. Nakubaliana na Pascal Mayalla kwenye hoja hii.
Tribalism ni human nature. Hata South Africa kuna political parties za Africans, whites na Indians. Reconciliation haikuweza kuiondoa hii hali.
Aliyepunduliwa sio Wazanzibar wenye asili ya kiarabu bali ni mkoloni Sultan. Ipo mifano mingi ya aina hii. Moja ya mifano ni USA. Marekani ni nchi yenye watu wengi wenye asili ya Ulaya, including Great Britain. Wakati wa nusu ya pili ya karne ya 18, Wamarekani waliamua kupigana vita kumng’oa Muingereza, mkoloni, na walifanikiwa kumng’oa wakawa taifa huru. Umewahi kusikia hoja ya Wamarekani kufanya reconciliation eti kwa sababu tu baadhi ya Wamarekani wana asili ya Uingereza (mkoloni aliyeng’olewa)?
Yawezekana, lakini fafanua huo mkwamo!Mkuu kuna sehemu unakwama kifikra.
“…Zanzibar was never colonized! …”??? Kwani kwa definition, colonization ni nini? As far as I know, wakoloni wote walikuwa wanajimilikisha territories zozote walizozipenda kama hakuwa challenged militarily.No Sultan hakuwa mwakilishi wa mkoloni, Zanzibar was never colonized!, kwenye ule mkutano wa Berlin, wa mwaka 1884, Zanzibar, visiwa vyote vya bahari ya Hindi, na 10 miles costal stripe, vilimilikishwa kwa Siltan of Zanzibar. It is as if Zanzibar haikuwahi kuwa na mwenyewe, Sultani alitoka zake Oman mwaka 1732 akavikuta visiwa havina mwenyewe, akajiokotea kama embe dodo chini mwembe.
Mwaka 1890 Zanzibar ikaziachia zile maili 10!.
P.
“…Zanzibar was never colonized! …”??? Kwani kwa definition, colonization ni nini? As far as I know, wakoloni wote walikuwa wanajimilikisha territories zozote walizozipenda kama hakuwa challenged militarily.
Na kama Zanzibar haikuwa colonized, independence ilikuwa ya nini, labda?
Zanzibar imepita kwenye mikono mingi ya wakoloni. Soma post #19.technical Zanzibar haikuwa colonized, British walikua ni protectors, although new nyuma ya pazia ulikuwa ni ukoloni tu.