Je, vioo vya TCL vina hali ya kuwa na mambo haya?

ngude Masanja

New Member
Mar 23, 2025
4
5
Habari!

Nihitaji kununua TCL android tv 32 ". Kwa Bahati nzuri nilifika Kariakoo nikatafuta hizo TCL na kuzIpata lakini cha ajabu vioo vyake naona si kama nlivyotarajia kwani ukivipiga piga (gusa gusa) wakati screen inaplay video vinaleta hali ya mawimbi au mwanga mweupe mdogo.(Unapo vigusa kwa kutumia mgandamizo mdogo wa vidole. Mithili ya kupiga piga kidogo kioo kwa kutumia kidole kimoja au viwili).

Nikauliza wauzaji mbona hizi screen zipo hivi nitofauti naTV nyIngne kama good vision?? (ambayo unaweza kutumia hata Bisibisi kugonga screen bila kupata shida yoyote)

Wanasema brand za TV kama TCL, Hisense, Samsung vioo vyao sio double Glass. Ni kioo kimoja na hawana double Glass.

Wakanionesha hizo Hisense na Samsung vioo vyake ukigusa na mkono vinaleta hali sawa na ya TCL. Sasa nikauliza mbona TCL niliyotumia nyumbani haikuwa hivi mpaka sasa ipo na kioo hakipo hivyo? Au kwa sababu ilikuwa ni inch ndogo (19" led tv). Wakajibu hiyo yawezekana ni mtumba.

Sasa wadau naomba KUSAIDIWA kitu kimoja nanyi. Kwanza Je, hali ya vioo vya TCL android na Smart TV nyingine za TCL za toleo la karbun ndiyo zina hali hii niliyokutana nayo? Au Je, hizo TV ni fake zinakuwa zImechakachuliwa siku hizi (na nilizunguka zaidi ya maduka 7 na nikakuta hali ipo vile vile kwa maduka yote kuhusu hali ya vioo vya TCL.)
Screenshot_20250324-000620.jpg
Screenshot_20250324-000509.jpg
Screenshot_20250324-000408.jpg
 
Back
Top Bottom