Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
2,181
5,553
Salaam,

Leo Februari 29, 2024 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametangaza kifo cha aliyekuwa Rais wa awamu ya pili wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi. Soma: Rais wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi afariki dunia

Kunako Utawala wake Hayati Mwinyi alifanya mambo mengi na kuacha historia kupitia Utawala wake na sera zake.

Mimi nitamkumbuka zaidi namna alivyoifungua nchi kupitia sera yake ya ruksa Miaka ya 1990.

Je, wewe utamkumbuka Mzee wetu huyu kwa mambo gani hasa?

 
Kiukweli, wasifu mzuri wa Hayati Ali Hassan Mwinyi uliimbwa kwenye miaka ya 90 na kundi la Mnanda/Mchiriku lililokuwa likiitwa Topaz.

Pumzika Hayati Mwinyi. Nilibahatika kuonana naye, nikiwa kijana mdogo, alipokuja shuleni kwetu (Shule ya Msingi) mwanzoni mwa miaka ya 90 akiwa Rais. Alikuwa mtu mwema, mkarimu, baba na kiongozi.
 
1. Kupenda Dini na Kusali sana.

2. Kupenda Utani na Ucheshi.

3. Kukitukuza Kiswahili na Kujivunia Kukiongea Kiufasaha.

4. Kuridhika na Maisha aliyonayo huku akipenda sana Kula Vyakula vya Kiasili na vya kuutunza Mwili kwa muda mrefu.

5. Kupenda mno Mazoezi hasa ya Kutembea kwa Miguu kwa Umbali mrefu.

6. Huruma,, Kusamehe na kutokiwa na Kinyongo na Mtu hasa hasa Adui.

7. Kutopenda Kujitukuza kama Kiongozi na kupenda Ushirikiano na Watu na kuwa mwepesi Kushaurika na Kujifunza.

Pumzika Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mzee Alhaji Ali Hassan Mwinyi hakika Mwendo Umeumaliza na huna baya hata kama lipo Watanzania tulishakusamehe Kitambo na Uhai wako huu mrefu ulikuwa ni Zawadi na Faraja kwetu.

Ulale mahala pema. Peponi AHM.
 
Ninachokumbuka enzi za utawala wa Mzee Mwinyi, hela ilikuwa inapatikana kwa urahisi sana! Yaani huwezi kulinganisha na utawala wa Nyerere, Mkapa, Magufuli, na huyu mama. Hawa kiukweli wameumiza wananchi walio wengi kwa ukata.

Anayemkaribia Mwinyi kwa kuruhusu hela nyingi mtaani, tena kwa mbaaali! Ni Kikwete.
 
Nakumbuka neno "mtukufu Rais"lilitamalaki.

Biashara ya boda kwa boda ilivuma, watu wakatoboa, nakumbuka mabasi ya sirari ya akina zacharia yalivyokuwa "yanauma" mzigo kwenye keria, kufulia majani ya mpapai kukaisha, shule binafsi zikaanza, magazeti binafsi, nakumbuka muhariri mmoja alichapwa na njiwa ofisini akachanwachanwa wakati akimfatafata mzee.

Waliosoma shule binafsi kwa nini wasimkumbuke Mwinyi?
 
Shukran zake wakati wa kuzindua kitabu chake sitosahau abadan

1) Namshukuru Mola kwa kuniumba maana angetaka angeniumba Mnyama pori nikawindwa lila sehemu ( ni binadamu wachache hukumbuka hii neema ya Mola kukuchagua kuwa mmoja wa binadamu maana angetaka angeweza kukuweka kwny kundi la mende au chawa )

2) Namshukuru Mola kwa kunipa umri mrefu wenye Afya njema ya mwili na akili ( hajajikweza sijui kuanza kusema siri ya umri sijui mazoezi sijui vyakula na blaa blaa kadhaa za kijanabi janabi )

3) Namshukuru mola kwa kunipa maisha ya mahusiano mema na Viongozi wangu pamoja na Rais wenzangu ( hajajikweza kujiweka kundi la Viongozi )
 
Kuuzwa Loliondo, Zanzibar kujaribu kujiunga OIC, kutaka kuundwa kwa serikali ya Tanganyika (Azimio la bunge lililochagizwa na wale G55), kufutwa kwa azimio la Arusha (matokeo yake viongozi wakuu wa serikali na familia zao ndio wafanyabiashara wakubwa nchini) N.K, Tuna bahati Mwalimu alikuwa hai na alifanya kazi ya ziada kuinusuru nchi.
 
Back
Top Bottom