Je, Tundu Lissu bado unaamini kuwa Magufuli ni Dikteta Uchwara?

Wadau, amani iwe kwenu.

Waswahili wanasema tuwe na akiba ya maneno. Kauli ya Lissu kuwa Rais Magufuli hi Dikteta Uchwara haijadhihiri kwake wala kwa wengine.

Licha ya Tundu Lissu kumtukana Rais hadharani, hakuna aliyemtoa hata ngeu. Alikamatwa kistaarabu. Akasafirishwa kistaarabu toka Singida hadi Dar es Salaam na akafunguliwa mashtaka kistaarabu. Kubwa zaidi ni pale mkondo wa sheria ulipopewa nafasi kwa Tundu Lissu kupewa muda wa kutosha kujitetea hadi kesi yake kuvunja rekodi ya kusikilizwa kwa zaidi ya dakika 500. Haya yote hayajapatapo kutokea kwenye utawala wa kidikteta.

Kikubwa zaidi ni pale Tundu Lissu alipopata dhamana na sasa yupo uraiani. Sidhani kama kwa nchi za kidikteta leo hii angeliona jua.

Niwakumbushe ndugu zangu wa upinzani kwamba siasa si ugomvi na wala si uadui. Lowasa amewafundisha muwe na siasa za kistaarabu na kimikakati kama kweli mna dhamira ya kwenda Ikulu. Kinyume chake mtaendelea kuwa wasindikizaji kwani sisi wananchi wa kawaida tunaendelea kuwadharau. Na ndio maana kila awamu kunakuwa na mabadiliko ya chama kikuu cha upinzani lakini CCM inaendelea kujinafasi kileleni. 1995 hadi 2000 tulikuwa na NCCR Mageuzi. 2000 hadi 2010 tulikuwa na CUF. 2010 hadi sasa tuna CHADEMA. Sitashangaa kuona mwaka 2020 tukiwa na chama kingine kikuu cha upinzani.
Udikteta ni pale mwenye mamlaka anapoacha kuheshimu katiba na sheria za nchi yake mwenyewe.
Chama kikuu cha upinzani 2020 chaweza kuja kuwa CCM, badala ya CDM. Amen
 
Sema "wewe" mwananchi wa kawaida,maana wananchi wengine wa kawaida huna haki ya kuwaongelea kwa niaba yao.
Ukisoma tafsiri ya Kamusi ya Kiswahili,Toka UDSM na yenye ithibati ya TUKI inaeleza hivi juu ya "Dikteta"
View attachment 377018

Kwa tafsiri hii,kauli ya Lissu inaendelea kudumu,itadumu mpaka hapo muelekeo wa huyo aliyepiwa jina hilo asiandane na sifa hizi
Vipi kuhusu Mbowe anayetawala milele CHADEMA na yeye ni dikteta? Kwa nini hataki wenzake wawe na kauli na badala yake ni yeye tu ndiye mwenye sauti? Rejea kufukuzwa kwa Zitto Kabwe
 
Udikteta ni pale mwenye mamlaka anapoacha kuheshimu katiba na sheria za nchi yake mwenyewe.
Chama kikuu cha upinzani 2020 chaweza kuja kuwa CCM, badala ya CDM. Amen
Hahahahahaaaaa! Septemba tunaingiza ndege mbili. Mpaka 2020 tutakuwa na ndege Sita. Nyie endeleeni kupiga mayowe
 
Unadhan tundu lisu wangemfanya nn labda ili udicteta udhihilike????
Unapofikiri kuhusu udicteda fikiri kwa mapana
Kumkamata tu ni udicteta pia maana hana kosa kufanya mkutano jimbon kwake
Kutukana watu pia ni udikteta na ni utaahira
 
Tundu lissu ni wakusamahewa hajui alinenalo ila kibri na jeuri ndio inamsumbua vilevile anapaswa kujua kuwa urais ni taasisi kubwa ajifunze nidhamu Luna watu walikuwa na kibri lakini Leo wamepotea kabisa katika kisiasa awe anaweka akiba ya maneno
Watanzania wengi tunashindwa kuelewayanyotendeka nchini mwetu kwani tuna shida zetu za maisha
 
Mngefanya jaribio lolote la kumdhuru mngejua vizuri ka nyie ni uchwara au la???
 
Unadhan tundu lisu wangemfanya nn labda ili udicteta udhihilike????
Unapofikiri kuhusu udicteda fikiri kwa mapana
Kumkamata tu ni udicteta pia maana hana kosa kufanya mkutano jimbon kwake
Hivi kweli nchi ingekuwa inaongozwa kidikteta unafikiri angepata dhamana?
 
Wadau, amani iwe kwenu.

Waswahili wanasema tuwe na akiba ya maneno. Kauli ya Lissu kuwa Rais Magufuli hi Dikteta Uchwara haijadhihiri kwake wala kwa wengine.

Licha ya Tundu Lissu kumtukana Rais hadharani, hakuna aliyemtoa hata ngeu. Alikamatwa kistaarabu. Akasafirishwa kistaarabu toka Singida hadi Dar es Salaam na akafunguliwa mashtaka kistaarabu. Kubwa zaidi ni pale mkondo wa sheria ulipopewa nafasi kwa Tundu Lissu kupewa muda wa kutosha kujitetea hadi kesi yake kuvunja rekodi ya kusikilizwa kwa zaidi ya dakika 500. Haya yote hayajapatapo kutokea kwenye utawala wa kidikteta.

Kikubwa zaidi ni pale Tundu Lissu alipopata dhamana na sasa yupo uraiani. Sidhani kama kwa nchi za kidikteta leo hii angeliona jua.

Niwakumbushe ndugu zangu wa upinzani kwamba siasa si ugomvi na wala si uadui. Lowasa amewafundisha muwe na siasa za kistaarabu na kimikakati kama kweli mna dhamira ya kwenda Ikulu. Kinyume chake mtaendelea kuwa wasindikizaji kwani sisi wananchi wa kawaida tunaendelea kuwadharau. Na ndio maana kila awamu kunakuwa na mabadiliko ya chama kikuu cha upinzani lakini CCM inaendelea kujinafasi kileleni. 1995 hadi 2000 tulikuwa na NCCR Mageuzi. 2000 hadi 2010 tulikuwa na CUF. 2010 hadi sasa tuna CHADEMA. Sitashangaa kuona mwaka 2020 tukiwa na chama kingine kikuu cha upinzani.
Ila kitendo cha polisi kumnyima dhamana hakikua kizuri ndio kinafanya watu wahisi hivyo. Pia wanasheria wa serikali kutumia sheria za Africa kusini za kipindi cha ubaguzi haikua busara. JPM anania nzuri ila wa chini yake wanamwangusha.
 
Wadau, amani iwe kwenu.

Waswahili wanasema tuwe na akiba ya maneno. Kauli ya Lissu kuwa Rais Magufuli hi Dikteta Uchwara haijadhihiri kwake wala kwa wengine.

Licha ya Tundu Lissu kumtukana Rais hadharani, hakuna aliyemtoa hata ngeu. Alikamatwa kistaarabu. Akasafirishwa kistaarabu toka Singida hadi Dar es Salaam na akafunguliwa mashtaka kistaarabu. Kubwa zaidi ni pale mkondo wa sheria ulipopewa nafasi kwa Tundu Lissu kupewa muda wa kutosha kujitetea hadi kesi yake kuvunja rekodi ya kusikilizwa kwa zaidi ya dakika 500. Haya yote hayajapatapo kutokea kwenye utawala wa kidikteta.

Kikubwa zaidi ni pale Tundu Lissu alipopata dhamana na sasa yupo uraiani. Sidhani kama kwa nchi za kidikteta leo hii angeliona jua.

Niwakumbushe ndugu zangu wa upinzani kwamba siasa si ugomvi na wala si uadui. Lowasa amewafundisha muwe na siasa za kistaarabu na kimikakati kama kweli mna dhamira ya kwenda Ikulu. Kinyume chake mtaendelea kuwa wasindikizaji kwani sisi wananchi wa kawaida tunaendelea kuwadharau. Na ndio maana kila awamu kunakuwa na mabadiliko ya chama kikuu cha upinzani lakini CCM inaendelea kujinafasi kileleni. 1995 hadi 2000 tulikuwa na NCCR Mageuzi. 2000 hadi 2010 tulikuwa na CUF. 2010 hadi sasa tuna CHADEMA. Sitashangaa kuona mwaka 2020 tukiwa na chama kingine kikuu cha upinzani.
Kwenye tawala za kidikteta kesi huwa zinaendeshwa kwa dakika tano mtu anatiwa hatia mambo yanaisha.
 
..hoja ya TL ni kwamba Raisi amedharau na kuvunja katiba kwa kutoa amri ya kuzuia mikutano ya hadhara.

..zaidi amekwenda mbali na kuvielekeza vyombo vya dola kutekeleza amri hiyo na hata ikibidi kutumia nguvu.

..watendaji wa serikali kama wakuu wa mikoa na wilaya nao wamekuwa wakisisitiza amri hiyo iliyo kinyume na katiba na kuvichagiza vyombo vya dola ktk maeneo ya kuwa tayari kutumia nguvu dhidi ya wananchi ambao wametangaza kutumia haki yao ya kikatiba kufanya mikutano na kuandamana.

..sasa amri hiyo ya Raisi ni udikteta. Na kumkamata na kumsumbua mwanasiasa anayekemea uvunjifu huo wa katiba ni muendelezo wa udikteta.
Hoja bado haijatimia hiyo. Hivi si ndio hiyo katiba huwa mnasema ni mbaya? Haifai? Leo hii mnatetea katiba mbovu?
Hivi Rais angekuwa dikteta unafikiri Lissu angepata dhamana tena mbele ya majudge anao wateua?
 
Tundu Lisu sifa zitamuua,na awe na akiba ya maneno na kuacha kunogewa na hamasa ya mikutano na kuropoka makubwa,ajue yeye ndiyo wanamtegemea kwa sheria,lakini inakuwa kama hajui sheria hadi anashikiliwa
angekua hajui angeachiwa jana!! usiwe mvivu wa kufikiri asee
 
Kwani udikteta ni kupiga watu tu! Uhaini dhidi ya katiba aliyoapia kuilinda ni Udikteta namba moja!!
Hivi bado unaona ni sawa ile kodi yako ilivyotumika kusafirisha mtu toka singida hadi dar kwa vile tu ameita jembe ni jembe?
Katiba gani mnayo iongelea ? Hii mnayo sema mbaya? Hivi unajua hao majudge mnao wapelekea case zenu ana wateua yeye? Angekuwa dikteta mgeshinda kweli? Au hamfahamu maana ya udikteta?
 
Mleta uzi unataka tasfiri ya DIKTETA UCHWARA au unaelezea UDIKTETA UCHWARA.
 
Wadau, amani iwe kwenu.

Waswahili wanasema tuwe na akiba ya maneno. Kauli ya Lissu kuwa Rais Magufuli hi Dikteta Uchwara haijadhihiri kwake wala kwa wengine.

Licha ya Tundu Lissu kumtukana Rais hadharani, hakuna aliyemtoa hata ngeu. Alikamatwa kistaarabu. Akasafirishwa kistaarabu toka Singida hadi Dar es Salaam na akafunguliwa mashtaka kistaarabu. Kubwa zaidi ni pale mkondo wa sheria ulipopewa nafasi kwa Tundu Lissu kupewa muda wa kutosha kujitetea hadi kesi yake kuvunja rekodi ya kusikilizwa kwa zaidi ya dakika 500. Haya yote hayajapatapo kutokea kwenye utawala wa kidikteta.

Kikubwa zaidi ni pale Tundu Lissu alipopata dhamana na sasa yupo uraiani. Sidhani kama kwa nchi za kidikteta leo hii angeliona jua.

Niwakumbushe ndugu zangu wa upinzani kwamba siasa si ugomvi na wala si uadui. Lowasa amewafundisha muwe na siasa za kistaarabu na kimikakati kama kweli mna dhamira ya kwenda Ikulu. Kinyume chake mtaendelea kuwa wasindikizaji kwani sisi wananchi wa kawaida tunaendelea kuwadharau. Na ndio maana kila awamu kunakuwa na mabadiliko ya chama kikuu cha upinzani lakini CCM inaendelea kujinafasi kileleni. 1995 hadi 2000 tulikuwa na NCCR Mageuzi. 2000 hadi 2010 tulikuwa na CUF. 2010 hadi sasa tuna CHADEMA. Sitashangaa kuona mwaka 2020 tukiwa na chama kingine kikuu cha upinzani.

Mbona hukutuambia limaanisha nini kwa kumwita Dikteta Magufuli Dikteta uchwara ??

Unakurupuka eti upinzani si uadui , hivi hayo mnayoyafanya kule Zanzibar tuite kitu gani ???

Wale masheikh wa Zanzibar itakuwaje wafungiwe Tanganyika na uchunguzi , sasa miaka zaidi ya 3 haujaisha ??

Au Tanganyika imekuwa Guantanamo Bay ??
 
Wewe huelewi tofauti ya kiongozi dikteta na kiongozi muuaji. Kiongozi dikteta ni yule ambaye hufanya maamuzi yeye pekee yake bila ya kujali mihimili na mamlaka nyingine zilizopo kisheria.

Hivi unajua kuwa Mandela alipokamatwa na makaburu, hakuwahi kupigwa? Tena unajua kuwa Mandela akiwa gerezani alipewa mpaka haki ya kujisomea mpaka kuwa na supervisor wa kimasomo, na akapata Masters degree akiwa gerezani? Lakini hiyo yote hayakumaanisha kuwa Afrika Kusini ilikuwa chini ya uongozi dhalimu wa baguzi wa rangi.

Kiongozi dikteta ni yule ambaye hunyang'anya mamlaka ya vyombo vingine vya kiutawala, kikatiba na kisheria, na mamlaka hayo hujipa yeye. Kwa mfano, hivi Rais ana mamlaka kisheria na kukatiba kuzuia mikutano ya kisiasa ya vyama vya upinzani? Kama hana, kwa nini awaagize polisi kutokuruhusu mikutano ya vyama vya upinzani? Hivi kuna sheria inayosema kuwa kunapofanyika mkutano wa chama cha upinzani hakustahili kuwa na kiongozi yeyote wa chama ambaye siyo wa eneo ambako mkutano unafanyika? Majibu ya maswali haya ndiyo yanayotufanya tutambue kuwa tuna kiongozi wa namna gani.
Sasa kwa tafsiri zako hapo kwenye maneno hayo mbona una dhihirisha kuwa Rais wetu si dikteta na nina hakika hujui kama hao majudge ana wateua yeye... Angekuwa dikteta kweli mgeshinda hata case moja au huyo tahira Tundu Lissu angelipata dhamana?
 
Uzi mwingine huu wa kuzima kichapo cha Jana,..sitoi kiki.,na zitakuja nyingi,, makada almost wote washaanzisha nyuzi,,,I choose to ignore u
 
Mimi ningekuwa polisi ningempiga ndani wiki mbili kwanza bila kumfikisha mahakamani.
 
Back
Top Bottom