Je, Tundu Lissu bado unaamini kuwa Magufuli ni Dikteta Uchwara?

Lizaboni humtendei haki Rais kwa kuanzisha mijadala yenye kujadili maneno ya CHUKI na KUUDHI ambayo tayari yanalalamikiwa mahakamani,Si lazima sana kuanzisha mijadala kama hatuna hoja madhubuti.
 
Hivi Raisi katukanwa tusi gani na Tundu Lisu? na kwanini mahakama haijamtia hatianI mpaka sasa?
Kwani kesi imeshasikilizwa? Shauri lililokuwa linasikilizwa jana ni Dhamana ya Lissu. Kesi halisi itasikilizwa Agosti 19
 
Wadau, amani iwe kwenu.

Waswahili wanasema tuwe na akiba ya maneno. Kauli ya Lissu kuwa Rais Magufuli hi Dikteta Uchwara haijadhihiri kwake wala kwa wengine.

Licha ya Tundu Lissu kumtukana Rais hadharani, hakuna aliyemtoa hata ngeu. Alikamatwa kistaarabu. Akasafirishwa kistaarabu toka Singida hadi Dar es Salaam na akafunguliwa mashtaka kistaarabu. Kubwa zaidi ni pale mkondo wa sheria ulipopewa nafasi kwa Tundu Lissu kupewa muda wa kutosha kujitetea hadi kesi yake kuvunja rekodi ya kusikilizwa kwa zaidi ya masaa 500. Haya yote hayajapatapo kutokea kwenye utawala wa kidikteta.

Kikubwa zaidi ni pale Tundu Lissu alipopata dhamana na sasa yupo uraiani. Sidhani kama kwa nchi za kidikteta leo hii angeliona jua.

Niwakumbushe ndugu zangu wa upinzani kwamba siasa si ugomvi na wala si uadui. Lowasa amewafundisha muwe na siasa za kistaarabu na kimikakati kama kweli mna dhamira ya kwenda Ikulu. Kinyume chake mtaendelea kuwa wasindikizaji kwani sisi wananchi wa kawaida tunaendelea kuwadharau. Na ndio maana kila awamu kunakuwa na mabadiliko ya chama kikuu cha upinzani lakini CCM inaendelea kujinafasi kileleni. 1995 hadi 2000 tulikuwa na NCCR Mageuzi. 2000 hadi 2010 tulikuwa na CUF. 2010 hadi sasa tuna CHADEMA. Sitashangaa kuona mwaka 2020 tukiwa na chama kingine kikuu cha upinzani.
Nilichokiona hapo ni masaa 500.
 
Warudisheni shule kwanza ao wanasheria wenu waliochoka namna ii hata kuandika anuani hawajui wanashindwa ata na mtoto wa darasa la pili
Kwa hiyo kama Lissu asingepata dhamana mngeendelea kulaumu ama?
 
Back
Top Bottom