Je, ni vibaya kuandika jina la mtoto katika kiwanja cha mke wangu?

UWOGA=UMASKINI

JF-Expert Member
Dec 30, 2013
2,400
1,015
Wanajamvi msaada, Mke wangu mtarajiwa amenishauri tununue kiwanja nikakubali na tukaamua kukinunua kiwanja hicho milioni mbili na akalazimisha tuandike majina ya mtoto wetu wa kwanza.

Tulizozana kidogo lakini nikakubali, sasa ananishauri na mimi nikakope benki ili tukajenge kwenye kiwanja chake maana anasema amechoka sana kupanga na ni gharama.

Je, kuna madhara kwangu kwa kuandika jina la mtoto kwasababu najua hicho kiwanja ni mke wangu aliyekinunua?
 
Si vibaya kuandika jina la mtoto au la mkeo,
Wewe kama wewe una kiwanja kingine au hicho ndio cha kwanza? Kama huna kiwanja kingine kwa jina lako inabidi uwe makini, unaweza kurudi tena hapa jf kutafuta ushauri.

Kwa nini msiandike Mr and Mrs?
 
Nina mwanamke nimezaa naye sina ndoa naye ila tunaishi pamoja na nategemea kufunga naye ndoa mwezi ujao, shida ni huyu mwanamama tumeshauriana akakopa yeye na kuamua kununua kiwanja na tukaamua kuandika jina la mtoto wetu huyu mmoja tuliyenaye sasa tumeshauriana tena mimi nikakope tupajenge.

Je kuna shida kwa kuandika jina hilo la mtoto wetu na mimi kupajenga?

Naombeni ushahuri jamani wapendwa.

Kiwanja ndo hicho2 hatuna kingine
 
Jina la hati ya kiwanja ni jina la mtoto, bila shaka hata nyumba itayojengwa mmliki wake atakuwa ni yule mwenye kiwanja...sasa sijui ukengeufu wa mawazo unautoa wapi!!!
 
Mwambie Kisheria Hamruhusiwi Kujenga Kwenye Kiwanja Ambacho Siyo Chenu. Asubiri Mnunue Chenu Na Si Kujenga Kiwanja Cha Mtoto. Wanawake Wakiwa Wanapata Pesa Utu Huwatoka Kabisa.

Kwa hiyo mkuu hatuaminiani au?
 
Yaani hukuona tatizo kabisa mpenzi wako alipokopa mkanunua kiwanja na kukipa jina la mtoto wenu ILA unaona tatizo kubwa wewe kukopa na kujenga kwenye kiwanja cha mtoto wenu hadi unaanzisha thread??? Acha huo ubinafsi kaka.
 
nina mwanamke nimezaa naye sina ndoa naye ila tunaishi pamoja na nategemea kufunga naye ndoa mwezi ujao.shida ni huyu mwanamama tumeshauriani akakopa yeye na kuamua kununua kiwanja na tukaamua kuandika jina la mtoto wetu huyu mmoja tuliyenaye sasa tumeshauriana tena mimi nikakope tupajenge. jE kUNA SHIDA KWA KUANDIKA JINA HILO LA MTOTO WETU NA MIMI KUPAJENGA? .naombeni ushahuri jamani wapendwa.kiwanja ndo hicho2 hatuna kingine

kwanini hamkopi mkafunga ndoa? mtazini hadi lini?
 
Wewe ndo kichwa cha familia, lazima mali ziandikwe kwa jina lako, kuhusu kumuandika mtoto sio sahihi unless hamna mpango wa kuzaa mwingine!
 
Kuna baadhi ya wanaume wabinafsi sana......


Mkeo tarajari kukopa kununua kiwanja (tena kuandika jina la mtoto) ni sawa hukukosa usingizi

Sasa inapokUja zamu yako kukopa ili mjenge, unataharuki
 
Unakopa ili kujenga?! Du kweli mitazamo tunatofautiana.

Ukijenga hela haizunguki, ila unailalia.

Usije kuanzisha uzi kuomba ushauri ufanyeje ili msilale njaa.
 
Kuna baadhi ya wanaume wabinafsi sana......


Mkeo tarajari kukopa kununua kiwanja (tena kuandika jina la mtoto) ni sawa hukukosa usingizi

Sasa inapokUja zamu yako kukopa ili mjenge, unataharuki

Kuna mtihani mkubwa katika hii issue ukiingia deeply!!
Makabila mengi mtoto aliezaliwa kabla ya ndoa ni Mali ya mama. Kwa hiyo hata kama kiwanja kitaandikwa jina la huyo mtoto lakini bado mama ana nafasi kubwa zaidi maana ndie mwenye mtoto!!
 
Back
Top Bottom