Je, ni sahihi kununua shamba ambalo lilikuwa na mgogoro kwa zaidi ya miaka mitano?

MWANAHARAKATI MWEMA

JF-Expert Member
Dec 16, 2022
209
303
Namshukuru mungu mwingi wa Rehema na muumbambaji wa vitu vyote vilivyopo duniani.

Mimi ninampango wa kuanza kufanya shughuli za kilimo ili nifanikiwe, sasa katika kufuatilia utaratibu nitumie kilimo kipi Kwa maana nikodi mashamba au ninunue ndipo nikapewa mchongo na mtu ambaye nafahamiana naye kwamba kuna eneo lenye majaruba linauzwa.

Nikaenda kufuatilia NI kweli maeneo ni mazuri na kuna mtaro, shida ikaja kwamba nikagundua maeneo hayo siku chache zilizopita yalikuwa na MGOGORO ila kesi ilikwisha wauzaji walishinda kesi.

Sasa wanajamvi naombeni ushauri eneo hilo kupata gunia 150 NI kawaida ila Nina hofu nisije toa pesa nikajiingiza kwenye matatizo na hasara, na pesa yenyewe ni ya mkopo naona kama pesa yangu inatamaniwa na shetani.

Asanteni.
 
Fuata utaratibu wa kisheria kununuwa, nenda kaandikishiane mahakamani usitumie advocate.
No, you're wrong.
Anapaswa aende kuandikishana kwa Mawakili au kwa Kamishina wa Viapo, ikiwezekana kwa wenye makampuni ya Uwakili.
Namshukuru mungu mwingi wa Rehema na muumbambaji wa vitu vyote vilivyopo duniani.

Mimi ninampango wa kuanza kufanya shughuli za kilimo ili nifanikiwe, sasa katika kufuatilia utaratibu nitumie kilimo kipi Kwa maana nikodi mashamba au ninunue ndipo nikapewa mchongo na mtu ambaye nafahamiana naye kwamba kuna eneo lenye majaruba linauzwa.

Nikaenda kufuatilia NI kweli maeneo ni mazuri na kuna mtaro, shida ikaja kwamba nikagundua maeneo hayo siku chache zilizopita yalikuwa na MGOGORO ila kesi ilikwisha wauzaji walishinda kesi.

Sasa wanajamvi naombeni ushauri eneo hilo kupata gunia 150 NI kawaida ila Nina hofu nisije toa pesa nikajiingiza kwenye matatizo na hasara, na pesa yenyewe ni ya mkopo naona kama pesa yangu inatamaniwa na shetani.

Asanteni.
Unaweza kununua.
Lakini, Kabla ya kununua ardhi hiyo hakikisha unapata photocopy za nyaraka zote kabisa kuhusu Kesi husika, na ujiridjishe kwa uhakika kuhusu Kesi husika pamoja na nakala ya hukumu.

ANGALIZO: Usithubutu kukurupuka kununua ardhi hiyo kabla ya kujua yote yaliyojiri kuhusu Kesi ya ardhi hiyo
 
No, you're wrong.
Anapaswa aende kuandikishana kwa Mawakili au kwa Kamishina wa Viapo, ikiwezekana kwa wenye makampuni ya Uwakili.

Unaweza kununua.
Lakini, Kabla ya kununua ardhi hiyo hakikisha unapata photocopy za nyaraka zote kabisa kuhusu Kesi husika, na ujiridjishe kwa uhakika kuhusu Kesi husika pamoja na nakala ya hukumu.

ANGALIZO: Usithubutu kukurupuka kununua ardhi hiyo kabla ya kujua yote yaliyojiri kuhusu Kesi ya ardhi hiyo
Mimi nilijaribu kutafuta ushauri wapo walioniambia kama itawezekana siku ya manunuzi awepo mtu Yule ambaye alikuwa ameshtakiana na muuzaji, hapo vipi kuna unafuu?
 
Naomba unipe elimu kidogo mkuu,maadvocate wana shida gani hadi aende mahakamani?
Ukitafuta haki unakimbilia wapi? Mauziano yakifanyika mahakamani kikitokea chochote hakuna mwenye ubavu wa kuichezea mahakama, hawa mawakili siku hizi wao wenyewe wanawekwa ndani.

Nawashauri watu issue za mauziano wadeal na mahakama moja kwa moja, bora ulipe kodi lakini uwe salama.
 
No, you're wrong.
Anapaswa aende kuandikishana kwa Mawakili au kwa Kamishina wa Viapo, ikiwezekana kwa wenye makampuni ya Uwakili.

Unaweza kununua.
Lakini, Kabla ya kununua ardhi hiyo hakikisha unapata photocopy za nyaraka zote kabisa kuhusu Kesi husika, na ujiridjishe kwa uhakika kuhusu Kesi husika pamoja na nakala ya hukumu.

ANGALIZO: Usithubutu kukurupuka kununua ardhi hiyo kabla ya kujua yote yaliyojiri kuhusu Kesi ya ardhi hiyo
Unasema am wrong una uhakika na ulichoandika?
 
Ukitafuta haki unakimbilia wapi? Mauziano yakifanyika mahakamani kikitokea chochote hakuna mwenye ubavu wa kuichezea mahakama, hawa mawakili siku hizi wao wenyewe wanawekwa ndani.

Nawashauri watu issue za mauziano wadeal na mahakama moja kwa moja, bora ulipe kodi lakini uwe salama.
Kwa mbaali una hoja, upewe Maiki usikilizwe
 
Siyo kwa mbali, huo ndio ukweli mtupu.

Kama una rafiki au ndugu hakimu muulize atakwambia ukweli.

Hata serikali za mitaa hawahusiki labda kuthibitisha tu wanamtambuwa muuzaji ndio mmiliki.
 
Ukitafuta haki unakimbilia wapi? Mauziano yakifanyika mahakamani kikitokea chochote hakuna mwenye ubavu wa kuichezea mahakama, hawa mawakili siku hizi wao wenyewe wanawekwa ndani.

Nawashauri watu issue za mauziano wadeal na mahakama moja kwa moja, bora ulipe kodi lakini uwe salama.
Endapo kama Mahakama ndio iliyoshuhudia Mkataba wa Mauziano ya ardhi, Halafu ardhi hiyo ikakumbwa na mgogoro, na Kisha mgogoro huo/Kesi ikafikishwa Mahakamani, Basi Mahakama itakuwa na Mgongano wa Maslahi kwenye Kesi hiyo.
"You cannot be a Judge for your own case."
 
Back
Top Bottom