Je, ni kweli maisha hayana formula?

Duuh ndugu yangu umenikumbusha mbali mno nakumbuka miaka ya themanini,niliifanya hiyo kazi Sweden nusura nikiue kibb cha kizungu,ile naweka gazei mlangoni kwake alfajiri na chenyewe kinafungua mlango, tukakutana uso kwa uso,na vile nilivyo mweusi kibibi kikajua ni gorilla, kikaanguka na kuzimia.
Mkuu ungeshtakiwa kwa kosa la kuua bila kukusudia..
 
Bado naamini maisha hayana formula kabisa kwa sababu watu wawili wanaweza kupita katika njia za kufanana sana chukulia mfumo wa elimu mmeanza wote toka primary mpaka chuo na mmesoma course moja na uelewa wenu ukawa unashabiiana sana katika matokeo ya darasani mkamaliza wote lakini kuja kwenye mafanikio ya kimaisha mkaja kuwa tofauti sana mwenzako akapata kazi mapema tena shirika linalopita sana wewe ukaja pata kazi miaka 4 ijayo tena kwa robo ya mshahara wa yule mwenzako na hii ipo sana ...So kama maisha yangekuwa na formula watu hawa wawili sababu wametumia njia moja ilibidi wote wapate majina sawa katika maisha lakini kwa mfano huo tu umeona walivyotofautiana...
 
Post # 11 mkuu ametoa mfano mzuri sana kua;

"kuna vijana wengi wenye vipaji kama Diamond lakini wanajitahidi kila siku ila inashindikana"

hapo ni wazi kabisa Maisha hayana formula,coz wangefata formula ya Diamond na wakafanikiwa,

Hata ukitizama kwenye Soccer, mfano huko South America kuna madogo wanacheza mpira kama hawana akili nzuri! Lakini wameshindwa kutoka kama wenzao kina Neymar,kama kuna formula wangefuata hiyo formula ya Neymar na wakatoka, Maisha yangekua na formula tusingekua na utofauti katika mafanikio, watu wote tungekua sawa coz wote tungefuata formula ile ile ya mafanikio,

Maisha sio sawa na kutengeneza Pepsi au Coca cola kusema wote tunatumia formula moja na kutoa result sawa!
 
Ata mm naona pamoja na formula kuwepo kuna bahati pia ya mtu angalia mfano mwingine akina mbwana samata kaka yake hua anasema hakudhani kama mbwana atakuja fikia pale manake tangia akiwa mdogo walikua wakicheza wote mchangani saa nyingine alikua akimwombea namba si unajua michezo ya kitoto mwenye mpira ndo anachagua nani acheze yy amekaza mpira huo huo lakin ameishia jkt
 
unapenda kutisha watu wewe..huna lolote unalojua
Mkuu huyo Kiumbe anayeitwa sijui Mshana jr anawaza mambo ya kufikirika tu,hata kama thread haihusu ushirikina lazima alete mambo yake tu kuhusu mambo ya kufikirika,

Watu akili zinawaza mbali yeye kakaa na mawazo mgando tu ya kushirikina!! Cha kusikitisha kuna watu hua wanaamini uongo wake wa kuongopea watu!!

Huyu ni wa kupuuzwa tu asiharibu hii thread ya watu wanaofikiria life,aende kwenye thread zake za Kitoto.
 
Duuh ndugu yangu umenikumbusha mbali mno nakumbuka miaka ya themanini,niliifanya hiyo kazi Sweden nusura nikiue kibb cha kizungu,ile naweka gazei mlangoni kwake alfajiri na chenyewe kinafungua mlango, tukakutana uso kwa uso,na vile nilivyo mweusi kibibi kikajua ni gorilla, kikaanguka na kuzimia.
 
Katika ulimwengu huu uliojaa mahangaiko na machungu watu tunazaliwa tukiwa hatuna ufahamu wowote wala kuelewa mambo ya mbele zaidi ya kutabili namna mambo yatakavyokuwa.....ndio maana kwenye masuala ya kutafuta ridhki haishangazi kumuona mtu aliyetumia miaka mingi kusomea masuala ya sheria anakuja kuwa mfanyabiashara maarufu......
Kwa kifupi ni kuwa maisha ni vita vinavyohitaji jitihada na maarifa ili kuweza kuvishinda na hatimaye kuyaona mafanikio.....lakini jitihada zetu na maarifa yetu havitafaa kitu bila ya kumtegemea muumba na kumtumainia yeye kwani yeye ndiye mtoaji na RIDHKI na humpa amtakaye kwa muda anaoona unafaa......wapo watu waliokuwa mafukara lakini neema zimewaangukia sasa hivi wanaogelea katika fedha.....ili hali kuna watu kibao nyuma ya pazia bado wanapambana na muda unazidi kwenda.......
Watu wenye vipaji kama alichonacho Diamond ni wengi sana mitaani na kila uchao wanajitahidi kwa kadri ya uwezo wao ili kufikia alipofikia huyo msanii lakini jitihada zinashindikana.....
Wapo watu walianza biashara pamoja na watu fulani lakini leo hii wenzao wakipiga hatua huku wao bado wakiendelea kusua sua kwenye biashara hiyo hiyo....

Kitu kimoja kikubwa kinachokosewa na vijana au tuseme kuwa wachakarikaji wa miaka hii ni kutafuta maisha au ridhiki kwa nia au kujiringanisha na fulani au nimpite fulani.....hiyo ni mbaya kwani kamwe hutakuja kuyaona wala kuyafurahia mafanikio yako kwani maisha hayataki haraka wala pupa...bali yanataka uvumilivu na busara za hali ya juu......huwezi kujua kuwa huyo unayetaka kuwa kama yeye imemchukua miaka mingapi hadi kufikia hapo alipo sasa na je upo tayari kupita njia hizo ili nawe ufike hapo.....!!!???
Stori na sifa huvuma baada ya mafanikio kuja lakini nyuma ya hayo mafanikio kumejaa vita kubwa sana hadi kufikia hapo....??

Usitafute maisha kwa kushindana na fulani bali jiwekee malengo yako na mikakati yako na upambane kwa uwezo wako wote ili kufanikisha mipango yako huku ukiwa na ndoto zenye kutekelezeka.......pia tujifunze kushukuru hata kile kidogo tulichojaaliwa.......
Nimekuelewa sana kiongozi
 
Maisha yana formula tena iko very clear. . .haya mengine ni maneno ya wakosoaji kujikataa na kukata tamaa
Wanatumia mifano michache ya watu waliofanikiwa kisha wakaanguka au ambao hawa kwenda shule lakini leo ni matajiri! Lakini jiulize wako wangapi?
Kama ingekuwa maisha hayana formula basi
Tusingeenda shule kusoma na kupata ujuzi na maarifa mbalimbali
Au tusingedamka na kuwahi kazini au kukesha nje gizani kwenye baridi na hatari zote za usiku kama mimi
Badala yake tungejifungia majumbani mwetu na kusubiri kupata kwa njia ya muujiza
kusema maisha hayana mathematical fomula ni kuwa huwezi kuwa Na jibu moja Kama 2+2=4. Maana yake ni kuwa mafanikio hayana single direction Na huwezi kuiga mtu ukategemea the same results. Mfano membe alikuwa Na uhakika WA kuingia magogoni Na sasa hivi yupo wapi? Mbinu zilizomwingiza jk hazikufanikiwa kwake. Mtoa mada anazungumzia kanuni tu. Au utasikia mtu anauliza ulifanyeje mpaka ukawa tajiri, hapo mtu anatafuta fomula ili aapply Matokeo yanaweza kuwa vyovyote Na wala si jibu moja Kama quadratic equation
 
kusema maisha hayana mathematical fomula ni kuwa huwezi kuwa Na jibu moja Kama 2+2=4. Maana yake ni kuwa mafanikio hayana single direction Na huwezi kuiga mtu ukategemea the same results. Mfano membe alikuwa Na uhakika WA kuingia magogoni Na sasa hivi yupo wapi? Mbinu zilizomwingiza jk hazikufanikiwa kwake. Mtoa mada anazungumzia kanuni tu. Au utasikia mtu anauliza ulifanyeje mpaka ukawa tajiri, hapo mtu anatafuta fomula ili aapply Matokeo yanaweza kuwa vyovyote Na wala si jibu moja Kama quadratic equation
Nakubaliana nawe ila mimi nimeongelea misingi na sio hizo alternatives nyingine.... kinachoanza ni misingi hapa ndio asili ya kila kitu halafu hayo mengine hufuata baadae ndio maana nikatoa mfano wa mtu aliyelala ndani akitegemea mafanikio
 
Nakubaliana nawe ila mimi nimeongelea misingi na sio hizo alternatives nyingine.... kinachoanza ni misingi hapa ndio asili ya kila kitu halafu hayo mengine hufuata baadae ndio maana nikatoa mfano wa mtu aliyelala ndani akitegemea mafanikio
Pamoja mkuu
 
Usinielewe vibaya mtaalamu. Hapa unaongelea jinsi unavyopigwa na baridi na hatari zote za usiku wakati ukiwa katika mambo yako ya kishirikina na matunguli? Nimesoma hiyo sentensi moja kwa moja wazo likanijia nikakuona kabisa laivu ukisafiri kwa ungo usiku kutoka Upareni kwenda DRC kupeleka ripoti. Pole sana mkuu. Ndo maisha ati!
Hahahahaa!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom