Je, ni busara kujenga nyumba kwa milioni 150 kisha kukusanya kodi laki 6 kwa mwezi?

Ngwanakilala,
Uwekezaji kwenye real estate, shares au Treasury bill una faida mbili (1) Ni return on investment (2) Appreciation in value of investment. Nyumba kama nyumba utaona hiyo kodi ya TZS 600,000 ni ndogo sana lakini ukiuza hiyo nyumba utapata zaidi mfano hiyo nyumba ya TZS 150,000,000 unaweza ukauza TZS 300,000,000.

Kwa wale tunaowekeza kwa ajili ya elimu ya watoto wetu; bado kuwekeza kwenye nyumba ni bora zaidi kuliko "Fixed deposit" kwani wakati nyumba ikiongezeka thamani kuendana na wakati, Principal amount kwenye Fixed Deposit haiongezeki thamani kinyume chake inapungua thamani (inflation).

Ushauri wangu wekeza kwenye nyumba pesa ambayo huna matumizi nayo yaani mtaji uliozidiki kwenye biashara yako na usiwekeze kwa matazamio ya kuvuna faida
Theory za wahasibu zinavyowadanganya, mbaya zaidi zinawaharibia maisha kbs, hadi aningia kaburini akiamini Ardhi pengine na nyumba zina appreciate in value, its a profitable ,Risk free Assets..
 
Usishangae asilimia kubwa ya watanzania maesabu yalishatupiga chini, ndio maana hatuna mipango ktk maisha tupo kama kuku wa kienyeji akiamka asubuhi kwenda kutafuta chakula bila kujua atapata wapi?

Sent from my Nokia 1 Plus using JamiiForums mobile app
Yaani mtu hujui anapata sh. Ngapi kwa mwezi na amewekeza kiasi gani unashaangaa kujenga nyumna ya mil. 150.
 
Waheshimiwa

Kuna jambo moja ambalo watu wengi wamekua wanalikosea bila kujua. Kwa maoni yangu ni muhimu kuelewa tofauti kati ya business na investments. Ni muhimu kuzingatia suala la return on investment au Retun on Asset wakati wowote unapofanya investment au biashara. Usipozingatia haya utasema huna bahati au unalogwa. Utakua frasturated na kuchukia biashara. Mfano

Mimi na wewe tunaweza kuchukua mkopo wa million 100, tukafungua biashara tofauti. Wewe ukawa unapata faida kubwa kwa haraka kuliko mimi. Au Wewe unaweza kuanzisha biashara ambayo ni capital intensive mimi nikaanzisha biashara ambayo sio capital intensive (haihitaji mtaji mkubwa).

Au wewe unaweza ukafungua biashara yenye matumizi mengi / higher expenses kama daladala/ malori kuliko mimi. Au wewe unaweza ukafungua biashara yenye risk kubwa kuliko mimi kama vile daladala zinazopata ajali kila mara nk. Au wewe unaweza kufungua bishara yenye mzunguko mkubwa wa mauzo kuliko mimi. Yote haya yataamua nani atafanikiwa kuliko mwengine baina yetu

Wakati mwengine hata structure ya biashara inaweza kuamua nani anafanikiwa kuliko mwengine. mimi na wewe wote tunaweza kuanzisha biashara inayofanana lakini tukatofautiana katika structure ya management au operations na hapo mmoja akafanikiwa kuliko mwengine.

Kwa mfano, wote tunaweza tukanunua bajaji kwa million 6 wewe ukaingia mkataba na dereva awe anakuletea kiasi fulani mpaka itakapofika million 10 then bajaji itakua yake. Mimi nikaweka dereva tu akawa analeta hesabu na hapo mmoja wetu akafanikiwa kuliko mwengine.

Wakati mwengine usimamizi tu unaweza kuleta tofauti kubwa sana. Wewe unaweza ukawa na Lori lako liko kijijini kwenu huko kaka zako wanasimamia na mimi nna Lori langu liko hapa Dar nasimamia mwenyewe au wote tunaweza kua na Fuso ziko dar lakini wewe ukapata dereva mwenye nidhamu mimi nikapata dereva asie mwaminifu na hapo tukapata matokeo tofauti kabisa

Tofauti hizi nyingi ndogo ndogo za kiufundi hua zinaleta matokeo tofautisana katika biashara na ni mambo ya kuzingatia kama unataka ufanikiwe kibiashara. ndio maana wewe unaweza ukawa na Daladala likakushinda ukauza mwenzako akanunua hioihilo akaa nalo miaka 10 ukabaki unashangaa

Kingine ni uvumilivu na kujifunza. Ukiwa na biashara na haiendi vizuri jitahidi kuvumilia na kujifunza na kurekebisha mapungufu yako katika biashara. Uyarekebishe na kuendelea. usiruke ruke na kuanzisha biashara mpya kila mwaka

Kingine Muhimu ni kuandika mapato na matumizi yote katika biashara yako ili baada ya mwaka au miaka 2 uweze kufanya tathimini na kuamua kama uendelee au la.

Mwisho nimalizie na mfano ulioko kwenye kichwa cha habari ya bandiko hili - case study. Nimekutana na rafiki zangu kama 4 ambao wanajilaumu kwa uamuzi wao wa kujenga nyumba na kuanza kukusanya kodi.

Wamekuja kugundua baadae kua faida hua ni ndogo na inachukua muda mrefu sana kupata - inachukua zaidi ya miaka 20 kubreak even na kuanza kupata real profit. Yuko mmoja ameachiwa nyumba ya urithi na anasema anatamani angeweza kuuza na hizo fedha akaingiza kwenye biashara nyingine yenye high and quick return - familia haiwezi kumruhusu.

Nyumba haimpi faida yoyote ya maana tena ni kubwa mno na wapangaji hamna. Yuko mwengine yeye alichukua mortgage kama million 200 pamoja na wife wakajenga nyumba. Wamekaa wamepiga hesabu na kugundua watakapomaliza kulipa baada ya miaka kama 15 watakua wamelipa kama million 400 kwa mbinde maana malipo ya mwezi ni zaid ya million 1 ambayo inawatesa sana kwasasa.

Wanajilaumu. Kwamfano: ukijenga nyumba kwa million 150 na kuanza kukusanya kodi ya 600,00 kwa mwezi itachukua miaka 21 kuweza kukusanya kodi ya million 150. Kama unajenga nyumba ya kuishi ni sahihi lakini nyumba kama biashara it might be a challenge. Furthermore, kama una million 150 wapo wanaodhani unaweza kuiingiza kwenye biashara kisha ukatumia faida ya hiyo biashara kujenga nyumba polepole

Tupe maoni yako, tujadiliane, tubadilishane mawazo, tufundishane
=====
MICHANGO ILIYOTOLEWA NA WADAU:

-------------

--------------

-------------

-------------


-------------

------------
 
Jenga apartment za chumba self contain and kitchen kwa kutumia cheap matereals tofali za choma and modern finishing. Jenga nyingi katika compound moja.ie jenga apartment tano kwenye kiwanja kimoja so ukiwa na viwanja viwili unakua na apartment kumi, Apartment moja utarentisha kwa kwa 180-200. Jenga Mwanza, Dodoma Arusha. Mil150 inatosha usikurupuke kujenga bangaloo
 
Jenga apartment za chumba self contain and kitchen kwa kutumia cheap matereals tofali za choma and modern finishing. Jenga nyingi katika compound moja.ie jenga apartment tano kwenye kiwanja kimoja so ukiwa na viwanja viwili unakua na apartment kumi, Apartment moja utarentisha kwa kwa 180-200. Jenga Mwanza, Dodoma Arusha. Mil150 inatosha usikurupuke kujenga bangaloo
Kiwanja je???
 
Ndio maana nikasema kujenga mwanza, dodoma au arusha. Mfano mwanza kiwanja cha mil10 ni kikubwa na kinafikika kiufupi sio nje ya mji
Ndo akapange mtu 180 chumba n'a jiko
 

Attachments

  • Screenshot_20230409-173717_Chrome.jpg
    Screenshot_20230409-173717_Chrome.jpg
    118 KB · Views: 35
Case ya Kariakoo ni very unique and rare. Wote hapa tunajua nan kavuruga uchumi wa nchi na kupelekea hali hiyo, sema tu tunaogopa kumtaja. Ndo hapo utajua biashara ni siasa. So kuwa na imani, hii hali itabadilika 2026.
Na kweli saiv tupo 2024 Hali ishaanza kubadilika
 
Back
Top Bottom