Je, ni busara kujenga nyumba kwa milioni 150 kisha kukusanya kodi laki 6 kwa mwezi?

Nyumba ya kuishi muhimu mana usijekuwa mpangaji milele...

Ila kwa ajili ya kujiongezea kipato ni bora kwa sasa kudeal na huduma zinazohitajika na kuingiza pesa walau kila siku mfano chakula na usafiri
ukiwa mpangaji milele kuna shida gani?
 
Ndachuwa,
Only real estate and Government Bonds can do the rest is un sertain. Shares can depressiet from the primary or secondary value.

With stocks you must know when to HOLD and when to FOLD!!! It is not like bank saving accounts!!!!
 
Waheshimiwa

Kuna jambo moja ambalo watu wengi wamekua wanalikosea bila kujua. Kwa maoni yangu ni muhimu kuelewa tofauti kati ya business na investments. Ni muhimu kuzingatia suala la return on investment au Retun on Asset wakati wowote unapofanya investment au biashara. Usipozingatia haya utasema huna bahati au unalogwa. Utakua frasturated na kuchukia biashara. Mfano

Mimi na wewe tunaweza kuchukua mkopo wa million 100, tukafungua biashara tofauti. Wewe ukawa unapata faida kubwa kwa haraka kuliko mimi. Au Wewe unaweza kuanzisha biashara ambayo ni capital intensive mimi nikaanzisha biashara ambayo sio capital intensive (haihitaji mtaji mkubwa).

Au wewe unaweza ukafungua biashara yenye matumizi mengi / higher expenses kama daladala/ malori kuliko mimi. Au wewe unaweza ukafungua biashara yenye risk kubwa kuliko mimi kama vile daladala zinazopata ajali kila mara nk. Au wewe unaweza kufungua bishara yenye mzunguko mkubwa wa mauzo kuliko mimi. Yote haya yataamua nani atafanikiwa kuliko mwengine baina yetu

Wakati mwengine hata structure ya biashara inaweza kuamua nani anafanikiwa kuliko mwengine. mimi na wewe wote tunaweza kuanzisha biashara inayofanana lakini tukatofautiana katika structure ya management au operations na hapo mmoja akafanikiwa kuliko mwengine.

Kwa mfano, wote tunaweza tukanunua bajaji kwa million 6 wewe ukaingia mkataba na dereva awe anakuletea kiasi fulani mpaka itakapofika million 10 then bajaji itakua yake. Mimi nikaweka dereva tu akawa analeta hesabu na hapo mmoja wetu akafanikiwa kuliko mwengine.

Wakati mwengine usimamizi tu unaweza kuleta tofauti kubwa sana. Wewe unaweza ukawa na Lori lako liko kijijini kwenu huko kaka zako wanasimamia na mimi nna Lori langu liko hapa Dar nasimamia mwenyewe au wote tunaweza kua na Fuso ziko dar lakini wewe ukapata dereva mwenye nidhamu mimi nikapata dereva asie mwaminifu na hapo tukapata matokeo tofauti kabisa

Tofauti hizi nyingi ndogo ndogo za kiufundi hua zinaleta matokeo tofautisana katika biashara na ni mambo ya kuzingatia kama unataka ufanikiwe kibiashara. ndio maana wewe unaweza ukawa na Daladala likakushinda ukauza mwenzako akanunua hioihilo akaa nalo miaka 10 ukabaki unashangaa

Kingine ni uvumilivu na kujifunza. Ukiwa na biashara na haiendi vizuri jitahidi kuvumilia na kujifunza na kurekebisha mapungufu yako katika biashara. Uyarekebishe na kuendelea. usiruke ruke na kuanzisha biashara mpya kila mwaka

Kingine Muhimu ni kuandika mapato na matumizi yote katika biashara yako ili baada ya mwaka au miaka 2 uweze kufanya tathimini na kuamua kama uendelee au la.

Mwisho nimalizie na mfano ulioko kwenye kichwa cha habari ya bandiko hili - case study. Nimekutana na rafiki zangu kama 4 ambao wanajilaumu kwa uamuzi wao wa kujenga nyumba na kuanza kukusanya kodi.

Wamekuja kugundua baadae kua faida hua ni ndogo na inachukua muda mrefu sana kupata - inachukua zaidi ya miaka 20 kubreak even na kuanza kupata real profit. Yuko mmoja ameachiwa nyumba ya urithi na anasema anatamani angeweza kuuza na hizo fedha akaingiza kwenye biashara nyingine yenye high and quick return - familia haiwezi kumruhusu.

Nyumba haimpi faida yoyote ya maana tena ni kubwa mno na wapangaji hamna. Yuko mwengine yeye alichukua mortgage kama million 200 pamoja na wife wakajenga nyumba. Wamekaa wamepiga hesabu na kugundua watakapomaliza kulipa baada ya miaka kama 15 watakua wamelipa kama million 400 kwa mbinde maana malipo ya mwezi ni zaid ya million 1 ambayo inawatesa sana kwasasa.

Wanajilaumu. Kwamfano: ukijenga nyumba kwa million 150 na kuanza kukusanya kodi ya 600,00 kwa mwezi itachukua miaka 21 kuweza kukusanya kodi ya million 150. Kama unajenga nyumba ya kuishi ni sahihi lakini nyumba kama biashara it might be a challenge. Furthermore, kama una million 150 wapo wanaodhani unaweza kuiingiza kwenye biashara kisha ukatumia faida ya hiyo biashara kujenga nyumba polepole

Tupe maoni yako, tujadiliane, tubadilishane mawazo, tufundishane
=====
MICHANGO ILIYOTOLEWA NA WADAU:

-------------

--------------

-------------

-------------


-------------

------------
sijakusoma hadi mwisho ila kichwa cha habari nimekupata
kuna mtu ana hela zinamwagika hazina kazi akifanya hivyo sio mbaya maana hata asipofaidi yeye watafaidi watoto na wajukuu zake.
Nimeshawahi fika sehemu moja kijijini nikaona nyumba zimejengwa za nguvu sana kuuliza nikaambiwa alnayejenga yuko Marekani nilichoshangaa nikaambiwa anajenga nyumba ya English medium nursery school kiukweli ukiingalia ukiambiwa ni chuo kikuu utasema hii sawa.Raisi wa nchi alipita anga izo siku moja akienda kwenye msiba flani akasimamisha msafara wake
Ngwanakilala,
Uwekezaji kwenye real estate, shares au Treasury bill una faida mbili (1) Ni return on investment (2) Appreciation in value of investment. Nyumba kama nyumba utaona hiyo kodi ya TZS 600,000 ni ndogo sana lakini ukiuza hiyo nyumba utapata zaidi mfano hiyo nyumba ya TZS 150,000,000 unaweza ukauza TZS 300,000,000.

Kwa wale tunaowekeza kwa ajili ya elimu ya watoto wetu; bado kuwekeza kwenye nyumba ni bora zaidi kuliko "Fixed deposit" kwani wakati nyumba ikiongezeka thamani kuendana na wakati, Principal amount kwenye Fixed Deposit haiongezeki thamani kinyume chake inapungua thamani (inflation).

Ushauri wangu wekeza kwenye nyumba pesa ambayo huna matumizi nayo yaani mtaji uliozidiki kwenye biashara yako na usiwekeze kwa matazamio ya kuvuna faida
sijakusoma hadi mwisho ila kichwa cha habari nimekupata
kuna mtu ana hela zinamwagika hazina kazi akifanya hivyo sio mbaya maana hata asipofaidi yeye watafaidi watoto na wajukuu zake.
Nimeshawahi fika sehemu moja kijijini nikaona nyumba zimejengwa za nguvu sana kuuliza nikaambiwa alnayejenga yuko Marekani nilichoshangaa nikaambiwa anajenga nyumba ya English medium nursery school kiukweli ukiingalia ukiambiwa ni chuo kikuu utasema hii sawa.Raisi wa nchi alipita anga izo siku moja akienda kwenye msiba flani akasimamisha msafara wake kuangalia.
we differ because we vary my brother
 
Kwa hiyo TZS 150,000,000 ukiwekeza kwenye nyumba na ukawa unapata TZS 7,200,000 watoto wako wawili wana uhakika wa kusoma mpaka chuo kikuu bila bugtha ya kukwama ada hata kama Mungu atakuwa amekupenda zaidi
Tatizo hiyo milioni 150 hujaipata kwa mkupuo, umejenga kidogo kidogo kwa miaka mitano..... . Watu wanadharau nyumba lakini inalipa in the long term. Mimi nimejenga nyumba ya kuishi imechukua zaidi ya 150m, lakini nimejenga kwa miaka 4. Kuna mtu alitaka kupangisha kwa 1.6 m nikakataa maana sikujenga kwa ajili ya kupangisha. Biashara nyingine sio kila mtu anaweza.
 
Mfano umeweka mil 2 na tukitumia mfano interest ya 4.5% then itakua

2mili×3/12×4.5%(1-0.1)=Tsh. 20,450

Huo ndio mpunga utakaopewa mzee baba.

3/12 ni miezi 3 utayoweka pesa yako,hio 12 jumla miezi iliyoko kwa mwaka.

4.5% hio ni riba ya CRDB

10% ni kodi ya serikali kwny faida utakayopata
Si ujuha huu sasa,si bora hio pesa ununue bodaboda upate faida laki 2,kisha uiuze kwa hasara ya laki moja kwa hio miezi mitatu?
 
Tatizo hiyo milioni 150 hujaipata kwa mkupuo, umejenga kidogo kidogo kwa miaka mitano..... . Watu wanadharau nyumba lakini inalipa in the long term. Mimi nimejenga nyumba ya kuishi imechukua zaidi ya 150m, lakini nimejenga kwa miaka 4. Kuna mtu alitaka kupangisha kwa 1.6 m nikakataa maana sikujenga kwa ajili ya kupangisha. Biashara nyingine sio kila mtu anaweza.
Kha watu mna mihela...yaani milion 150 kwa nyumba tuu😲😲😲😲
 
Kha watu mna mihela...yaani milion 150 kwa nyumba tuu
Usishangae asilimia kubwa ya watanzania maesabu yalishatupiga chini, ndio maana hatuna mipango ktk maisha tupo kama kuku wa kienyeji akiamka asubuhi kwenda kutafuta chakula bila kujua atapata wapi?

Sent from my Nokia 1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Ngwanakilala,
Uwekezaji kwenye real estate, shares au Treasury bill una faida mbili (1) Ni return on investment (2) Appreciation in value of investment. Nyumba kama nyumba utaona hiyo kodi ya TZS 600,000 ni ndogo sana lakini ukiuza hiyo nyumba utapata zaidi mfano hiyo nyumba ya TZS 150,000,000 unaweza ukauza TZS 300,000,000.

Kwa wale tunaowekeza kwa ajili ya elimu ya watoto wetu; bado kuwekeza kwenye nyumba ni bora zaidi kuliko "Fixed deposit" kwani wakati nyumba ikiongezeka thamani kuendana na wakati, Principal amount kwenye Fixed Deposit haiongezeki thamani kinyume chake inapungua thamani (inflation).

Ushauri wangu wekeza kwenye nyumba pesa ambayo huna matumizi nayo yaani mtaji uliozidiki kwenye biashara yako na usiwekeze kwa matazamio ya kuvuna faida
KINACHOKUA NI KIWANJA SIYO NYUMBA.
 
Back
Top Bottom