Valencia_UPV
JF-Expert Member
- Mar 31, 2016
- 6,688
- 8,441
ukiwa mpangaji milele kuna shida gani?Nyumba ya kuishi muhimu mana usijekuwa mpangaji milele...
Ila kwa ajili ya kujiongezea kipato ni bora kwa sasa kudeal na huduma zinazohitajika na kuingiza pesa walau kila siku mfano chakula na usafiri
Ndachuwa,
Only real estate and Government Bonds can do the rest is un sertain. Shares can depressiet from the primary or secondary value.
Mradi ukubali kunyanyasika kama umepanga nyumba ya waswahili!!!ukiwa mpangaji milele kuna shida gani?
kwenye pagala lako hunyanyasiki?Mardi ukubali kunyanyasika kama umepanga nyumba ya waswahili!!!
kwenye pagala lako hunyanyasiki?
sijakusoma hadi mwisho ila kichwa cha habari nimekupataWaheshimiwa
Kuna jambo moja ambalo watu wengi wamekua wanalikosea bila kujua. Kwa maoni yangu ni muhimu kuelewa tofauti kati ya business na investments. Ni muhimu kuzingatia suala la return on investment au Retun on Asset wakati wowote unapofanya investment au biashara. Usipozingatia haya utasema huna bahati au unalogwa. Utakua frasturated na kuchukia biashara. Mfano
Mimi na wewe tunaweza kuchukua mkopo wa million 100, tukafungua biashara tofauti. Wewe ukawa unapata faida kubwa kwa haraka kuliko mimi. Au Wewe unaweza kuanzisha biashara ambayo ni capital intensive mimi nikaanzisha biashara ambayo sio capital intensive (haihitaji mtaji mkubwa).
Au wewe unaweza ukafungua biashara yenye matumizi mengi / higher expenses kama daladala/ malori kuliko mimi. Au wewe unaweza ukafungua biashara yenye risk kubwa kuliko mimi kama vile daladala zinazopata ajali kila mara nk. Au wewe unaweza kufungua bishara yenye mzunguko mkubwa wa mauzo kuliko mimi. Yote haya yataamua nani atafanikiwa kuliko mwengine baina yetu
Wakati mwengine hata structure ya biashara inaweza kuamua nani anafanikiwa kuliko mwengine. mimi na wewe wote tunaweza kuanzisha biashara inayofanana lakini tukatofautiana katika structure ya management au operations na hapo mmoja akafanikiwa kuliko mwengine.
Kwa mfano, wote tunaweza tukanunua bajaji kwa million 6 wewe ukaingia mkataba na dereva awe anakuletea kiasi fulani mpaka itakapofika million 10 then bajaji itakua yake. Mimi nikaweka dereva tu akawa analeta hesabu na hapo mmoja wetu akafanikiwa kuliko mwengine.
Wakati mwengine usimamizi tu unaweza kuleta tofauti kubwa sana. Wewe unaweza ukawa na Lori lako liko kijijini kwenu huko kaka zako wanasimamia na mimi nna Lori langu liko hapa Dar nasimamia mwenyewe au wote tunaweza kua na Fuso ziko dar lakini wewe ukapata dereva mwenye nidhamu mimi nikapata dereva asie mwaminifu na hapo tukapata matokeo tofauti kabisa
Tofauti hizi nyingi ndogo ndogo za kiufundi hua zinaleta matokeo tofautisana katika biashara na ni mambo ya kuzingatia kama unataka ufanikiwe kibiashara. ndio maana wewe unaweza ukawa na Daladala likakushinda ukauza mwenzako akanunua hioihilo akaa nalo miaka 10 ukabaki unashangaa
Kingine ni uvumilivu na kujifunza. Ukiwa na biashara na haiendi vizuri jitahidi kuvumilia na kujifunza na kurekebisha mapungufu yako katika biashara. Uyarekebishe na kuendelea. usiruke ruke na kuanzisha biashara mpya kila mwaka
Kingine Muhimu ni kuandika mapato na matumizi yote katika biashara yako ili baada ya mwaka au miaka 2 uweze kufanya tathimini na kuamua kama uendelee au la.
Mwisho nimalizie na mfano ulioko kwenye kichwa cha habari ya bandiko hili - case study. Nimekutana na rafiki zangu kama 4 ambao wanajilaumu kwa uamuzi wao wa kujenga nyumba na kuanza kukusanya kodi.
Wamekuja kugundua baadae kua faida hua ni ndogo na inachukua muda mrefu sana kupata - inachukua zaidi ya miaka 20 kubreak even na kuanza kupata real profit. Yuko mmoja ameachiwa nyumba ya urithi na anasema anatamani angeweza kuuza na hizo fedha akaingiza kwenye biashara nyingine yenye high and quick return - familia haiwezi kumruhusu.
Nyumba haimpi faida yoyote ya maana tena ni kubwa mno na wapangaji hamna. Yuko mwengine yeye alichukua mortgage kama million 200 pamoja na wife wakajenga nyumba. Wamekaa wamepiga hesabu na kugundua watakapomaliza kulipa baada ya miaka kama 15 watakua wamelipa kama million 400 kwa mbinde maana malipo ya mwezi ni zaid ya million 1 ambayo inawatesa sana kwasasa.
Wanajilaumu. Kwamfano: ukijenga nyumba kwa million 150 na kuanza kukusanya kodi ya 600,00 kwa mwezi itachukua miaka 21 kuweza kukusanya kodi ya million 150. Kama unajenga nyumba ya kuishi ni sahihi lakini nyumba kama biashara it might be a challenge. Furthermore, kama una million 150 wapo wanaodhani unaweza kuiingiza kwenye biashara kisha ukatumia faida ya hiyo biashara kujenga nyumba polepole
Tupe maoni yako, tujadiliane, tubadilishane mawazo, tufundishane
=====
MICHANGO ILIYOTOLEWA NA WADAU:
-------------
--------------
-------------
-------------
-------------
------------
sijakusoma hadi mwisho ila kichwa cha habari nimekupataNgwanakilala,
Uwekezaji kwenye real estate, shares au Treasury bill una faida mbili (1) Ni return on investment (2) Appreciation in value of investment. Nyumba kama nyumba utaona hiyo kodi ya TZS 600,000 ni ndogo sana lakini ukiuza hiyo nyumba utapata zaidi mfano hiyo nyumba ya TZS 150,000,000 unaweza ukauza TZS 300,000,000.
Kwa wale tunaowekeza kwa ajili ya elimu ya watoto wetu; bado kuwekeza kwenye nyumba ni bora zaidi kuliko "Fixed deposit" kwani wakati nyumba ikiongezeka thamani kuendana na wakati, Principal amount kwenye Fixed Deposit haiongezeki thamani kinyume chake inapungua thamani (inflation).
Ushauri wangu wekeza kwenye nyumba pesa ambayo huna matumizi nayo yaani mtaji uliozidiki kwenye biashara yako na usiwekeze kwa matazamio ya kuvuna faida
Tatizo hiyo milioni 150 hujaipata kwa mkupuo, umejenga kidogo kidogo kwa miaka mitano..... . Watu wanadharau nyumba lakini inalipa in the long term. Mimi nimejenga nyumba ya kuishi imechukua zaidi ya 150m, lakini nimejenga kwa miaka 4. Kuna mtu alitaka kupangisha kwa 1.6 m nikakataa maana sikujenga kwa ajili ya kupangisha. Biashara nyingine sio kila mtu anaweza.Kwa hiyo TZS 150,000,000 ukiwekeza kwenye nyumba na ukawa unapata TZS 7,200,000 watoto wako wawili wana uhakika wa kusoma mpaka chuo kikuu bila bugtha ya kukwama ada hata kama Mungu atakuwa amekupenda zaidi
Si ujuha huu sasa,si bora hio pesa ununue bodaboda upate faida laki 2,kisha uiuze kwa hasara ya laki moja kwa hio miezi mitatu?Mfano umeweka mil 2 na tukitumia mfano interest ya 4.5% then itakua
2mili×3/12×4.5%(1-0.1)=Tsh. 20,450
Huo ndio mpunga utakaopewa mzee baba.
3/12 ni miezi 3 utayoweka pesa yako,hio 12 jumla miezi iliyoko kwa mwaka.
4.5% hio ni riba ya CRDB
10% ni kodi ya serikali kwny faida utakayopata
Kha watu mna mihela...yaani milion 150 kwa nyumba tuu😲😲😲😲Tatizo hiyo milioni 150 hujaipata kwa mkupuo, umejenga kidogo kidogo kwa miaka mitano..... . Watu wanadharau nyumba lakini inalipa in the long term. Mimi nimejenga nyumba ya kuishi imechukua zaidi ya 150m, lakini nimejenga kwa miaka 4. Kuna mtu alitaka kupangisha kwa 1.6 m nikakataa maana sikujenga kwa ajili ya kupangisha. Biashara nyingine sio kila mtu anaweza.
Mbona ziko za gharama zaidi ya hiiKha watu mna mihela...yaani milion 150 kwa nyumba tuu😲😲😲😲
Aisee....ningetamani kuiona hii nyumba ya million 150. Japo nilale siku moja nione kama kuna utofauti wa usingizi na hizi nyumba zetu za mbavu za mbwaMbona ziko za gharama zaidi ya hii
Makubwa hayaAisee....ningetamani kuiona hii nyumba ya million 150. Japo nilale siku moja nione kama kuna utofauti wa usingizi na hizi nyumba zetu za mbavu za mbwa
Na sie wote wakubwa so no problemMakubwa haya
Nakubaliana na wewe, hivi wewe unaweza jenga nyumba ya bishara India ilihali wewe ni Mtanzania unayeishi kule? Wenyewe wako mguu nje ndaniWao hawana guarantee ya maisha, hapa sio kwao na ndio maana hawajengi...Wengi wananunua tu!
Usishangae asilimia kubwa ya watanzania maesabu yalishatupiga chini, ndio maana hatuna mipango ktk maisha tupo kama kuku wa kienyeji akiamka asubuhi kwenda kutafuta chakula bila kujua atapata wapi?Kha watu mna mihela...yaani milion 150 kwa nyumba tuu
Hakuna uraisi uraisi ktk maisha kama unavyosema apa150 nipe nakupa 12mil kila mwaka Kama riba
KINACHOKUA NI KIWANJA SIYO NYUMBA.Ngwanakilala,
Uwekezaji kwenye real estate, shares au Treasury bill una faida mbili (1) Ni return on investment (2) Appreciation in value of investment. Nyumba kama nyumba utaona hiyo kodi ya TZS 600,000 ni ndogo sana lakini ukiuza hiyo nyumba utapata zaidi mfano hiyo nyumba ya TZS 150,000,000 unaweza ukauza TZS 300,000,000.
Kwa wale tunaowekeza kwa ajili ya elimu ya watoto wetu; bado kuwekeza kwenye nyumba ni bora zaidi kuliko "Fixed deposit" kwani wakati nyumba ikiongezeka thamani kuendana na wakati, Principal amount kwenye Fixed Deposit haiongezeki thamani kinyume chake inapungua thamani (inflation).
Ushauri wangu wekeza kwenye nyumba pesa ambayo huna matumizi nayo yaani mtaji uliozidiki kwenye biashara yako na usiwekeze kwa matazamio ya kuvuna faida