Je, Makonda naye yupo mtegoni, suala la watumishi hewa?

Anachokifanya Magufuli ni kutumbua wale ambao hawakuwa chaguo lake hivyo anawatafutia kosa hata liwe dogo namna gani ili awaondoe aweke wale chaguo lake, hivyo kwa Makonda, Nape, Mwigulu, Kitwanga na January Makamba hata wafanye madudu kiasi gani kamwe hawezi kuwafanya chochote kwani anajua wazi wamempigania ili yeye aonekane ameshinda nafasi ya Urais.

makonda sio chaguo la ridhwan tena?
 
Acha uongo lete hiyo kauli ya kilango kuwa zoezi ni endelevu

Ulisikiliza kauli ya Kilango?, alisema exactly alichosema makonda kuwa zoezi ni endelevu


Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anne Kilango Malecela amesema mkoa wake hauna mfanyakazi hewa hata mmoja wakati wa uhakiki wa wafanyakazi uliofanyika mkoani humo.

Mama Kilango ameyasema hayo alipokuwa akiwasilisha serikalini ripoti ya mkoa wake kufuatia agizo la Rais kwa wakuuu wa mikoa kote nchini kuwasilisha majina ya watumishi hewa wanaoliingizia taifa hasara huku wakiwa hawapo kazini.

''Mkoa wa Shinyanga hauna mfanyakazi hewa hata mmoja kutokana na mpango waliojiwekea viongozi wa mkoa kwa kufuatilia watumishi waliopo kazini na kulipa mishahara kwa watumishi waliopo maeneo ya kazi pekee.'' Amesema Kilango.

Aidha kwa ripoti za wakuu wa mikoa zilizowasilishwa mkoa wa Mwanza unaongoza kwa kuwa na watumishi hewa 334 na Arusha 270 na Singida 231ikifuatiwa na mikoa mingine.

Hata hivyo waziri George Simbachawene amewataka wakuu wa Mikoa kuhakikisha wanaendeleza zoezi hilo kwani kuna wafanyakazi ambao wameaga wapo likizo na wengine masomoni wakati uhalisia haupo
 
kwa kinondoni tu alipokuwa mkuu wa wilaya hapakosi watumishi hewa zaidi ya idadi aliyoiwasilisha
 
Wanajamvi,

Kutokana na Anne Kilango kutumbuliwa kwa kudanganya kuwa mkoa wa Shinyanga hauna watumishi hewa, turudi Dar ambapo mkuu wa mkoa aliitangazia Tanzania kuwa mkoa wake unawatumish hewa 11.

Kiukweli Dar ni moja ya mikoa yenye watumishi wengi sana katika halmashauri zake na ni mkoa unao vutia watu wengi kufanya kazi. Lakini lazima tuangalie kwa mapana zaidi, hii inawezekana mkoa kuwa na watumishi hewa 11 tu.

Mimi naamini kwamba sehemu yeyote inayokimbiliwa, kuwa uwezakono mkubwa vile vile kwa watu wengi kuondoka pia. Kufuata maslahi zaidi.

Naamini mkuu wa mkoa kadanganywa na wasaidizi wake, siamini kabisa kama mkoa mzima una idadi hiyo ya watumishi hewa. Hasa kutokana na hofu ya hawa watendaji kutumbuliwa kama wangeitaja idadi halisi.
Mimi ningependa tutajiwe majina sio kugewa number tu, mfano hao 11 si rahisi tu kutajwa au mimi ndio sielewi wanaposema watumishi hewa wana maana gani? Na kama ni mtumishi hewa tutamkamata wapi au nani atalipa pesa alizokula uyo mtumishi hewa??
 
Mkoa wa Dar Es Salaam.

Akiwasilisha ripoti ya watumishi hewa, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema katika mkoa wake baada ya kufanya uchunguzi kwa kushirikiana na kamati mbali mbali wamebaini kuwepo kwa watumishi hewa 73 ambao watumishi hao hewa wamepelekea serikali kupotea pesa zaidi ya Milioni 316 kwa mwaka mmoja.

“Katika mkoa huu tumepata watumioshi hewa 73,ila wengi watahoji mkoa huu mkubwa kwanini unakuwa na watumishi hewa wachache,nakata kukwambia Waziri, bado tunaendelea na uchunguzi wa kina”amesema Makonda .

Mkoa wa Arusha.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Daudi Felix Ntibenda amesema katika mkoa huo umegundurika kuwepo na watumishi hewa 270 ambao wamekuwa wakiisababishia hasara serikali ya Bilioni 1.8 kwa kipindi cha Mwaka mmoja.

Mkoa wa Mwanza.

Mkuu wa Mkoa wa John Mongella amesema mkoa wake umengundurika kuwepo kwa watumishi hewa 334.

Mkoa wa Pwani.

Mkuu wa Mkoa huyo, Mhandisi Evarist Ndikilo amesema Mkoa wake umekuwa na watumishi hewa 150 huku akishindwa kusema hasara ya fedha za serikali kwa madai kuwa uchunguzi unaendelea.

Mkoa wa Singida,

Mkuu wa mkoa wa huo,Mhandisi Methew Mtigumwe amesema kuwa wafanyakazi hewa katika mkoa wake,231nakueleza kuwa uchunguzi bado unaendelea ili kubaini zaidi.

BADO NAMTAKAFARI... namtafakur huyu DOGO JANJA na hii idadi yake bado sijaikubali ukizingatia hili jiji ndio kwenye waajiriwa lukuki kuzidi mikoa yote TZ wizara zote ziko hapa mpaka IKULU IKO HAPA.
 
Back
Top Bottom