Je, kufungua nchi ndio kuifanya dampo?

PerKnot

Member
Jan 15, 2018
61
74
Wasalaam ndugu zangu,Nimepende kuchukua fursa hii kuwasalimu watanzania wote wapenda maendeleo kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristo ,amani iwe kwenu.

Lipo jambo linanitatiza,maana kwa jinsi nionavyoo,huku tunapoelekea ni kwenyewe au tumeingia chaka.Jambo lenyewe ni swala la kufungua mipaka yetu,hasa kwaajili ya biashara na huduma.

Katika, karne hii ni kweli huwezi kuwa na maendeleo kama hutaruhusu muingiliano wa bidhaa na huduma, hasa kwa mataifa kama letu linaloendelea ,ila je tunafungua mipaka au tunaancha mlango wazi.

Katika swali langu lengo kuu ni kuangalia ,sera au mbinu hii ya kufungua mipaka ,ni jambo zuri ila ,Je katika kufungua mipaka yetu ,tuelezwe tunafungua ili
Tuuziwe nini?
Tukauze nini?
Swala la nani au wapi si la mantiki sana?

Tumefungua mipaka ndio kusema ,uhuru wa mtanzania kuuza au kununua na kuja kuuza nje na ndani ya nchi umeimarishaa ,kwa hilo lahasha sina pingamizi.

Ila, kisokorokwinyo changu kipo hapa kwenye kufungua mipaka ili
Nani aje auze?
Nini jike kiuzwe?
Tufungue mipaka ili,.
Tuuziwe pumba za kuku?
Tuuziwe mayai ?.
Wauze na manyoya ya kuku
Tufungue mipaka,sio ndio mapato yataongezeka.

Au tufungue mipaka.
Tuuze simba
Tuchanganye na mbuzi
Tena wakiwa hai,tuwaongeze na tembo
Sisi tuuze maneno.
Watanzania tufungue mipaka.

Maana kwenye mipaka tunalinda ,uchumi wetu,tunalinda tamaduni zetu, desturu zetu, imani ,afya na vyakula vyetu.

Nauliza kwenye kufungua mipaka tunayaona haya yote .Sipingi kwenye suala la biashara huria na mzunguko wa watu na bidhaa ,ila kikwazo tunafungua hii mipaka kwaajili ya nani na nini kipite.

Leo,tunafungua mipaka kwaajili ya mayai,manyoya ya kuku na pumba ,hivi baada ya miaka 10 nchi hii itakuwaje ,kama hata vitu vidogo kama hivi tunaagiza nje .Tutasema labda uzalishaji mdogo,ila kimsingi uzalishaji mkubwa hauji siku moja, iweke mikakati.

Tukisema hatuna teknolojia na ujuzi, pia hii sio sababau maana teknolojia ni maisha huja pale tunapotaka kutatua matataizo ya maisha .

Uhusiano mzuri kati yetu na majirani au washirika wengine unaweza ukawepo ,hata tusipokuwa dampo la bidhaa kutoka kwao,ni rai yangu kwa serikali sasa kuangalia ,nini kinahitajika zaidi kwa watanzania ndio tukifungulie mipaka.

Masoko makubwa kama kariakoo yamejaa bidhaa ambazo hata hapa Tanzania zinatengenzwa ,ukiangalia vizuri unakutana na sera mbovu na tamaa za kodi ,zisizo endelevu.

Nipende kuwakumbusha viongozi,kizazi cha sasa ni cha tisini na elfu mbili, na kwa pamoja tunasema ,tumejiandikisha na tutajiandikisha ,kwa uweza wa Mungu 2025 si mbali, sanduku la kura litaongea .
#Ninakitambulishochangumfukoni,
 
Yanayoendelea hapa nchini wala tusiyashangae. Ni mambo tuliyoyatarajia baada ya kundi flani kushika madaraka. Ni mengi tunayaona na kusikia lakini tufanyeje sasa.
 
Mkuu, huwez kuwa na soko huria huku unachagua cha kuuza na kununua, mfano, tukizuia baadhi ya bidhaa za kenya, nao wakazuia mahindi yetu (iliwahi tokea kesi kama hii kipind cha Magu) utakuta mnakua two losers, so hivyo vitu acha walete, kikubwa tupambane tufanye uzalishaji wa ndani uwe wa tija, mbna carbonated drinks zinaletwa ila zinashindwa penya mtaani, pombe zenyewe imported zinapata shida sana sokon,

Tuboreshe sera za uwekezaji huku tukimaintain soko huria
 
K

Kwa uongozi tilionao sidhani kuwa inawezekana kuongeza uzalishaji wa ndani wakati wameua sera ya viwanda
 
Mkuu, huwez kuwa na soko huria huku unachagua cha kuuza na kununua, mfano, tukizuia baadhi ya bidhaa za kenya, nao wakazuia mahindi yetu (iliwahi tokea kesi kama hii kipind cha Magu) utakuta mnakua two losers, so hivyo vitu acha walete, kikubwa tupambane tufanye uzalishaji wa ndani uwe wa tija, mbna carbonated drinks zinaletwa ila zinashindwa penya mtaani, pombe zenyewe imported zinapata shida sana sokon,

Tuboreshe sera za uwekezaji huku tukimaintain soko huria
Kiongozi sipingi ,ila kweli ndio waje wauze hata mayai ya kuku.Na tunasema Kilimo ndio uti wa mgongo,hapo kweli tutainua kilimo na huyu mkulima?, ushindani uwepo ila uwe wa ndani sisi kwa sisi.
 
Kiongozi sipingi ,ila kweli ndio waje wauze hata mayai ya kuku.Na tunasema Kilimo ndio uti wa mgongo,hapo kweli tutainua kilimo na huyu mkulima?, ushindani uwepo ila uwe wa ndani sisi kwa sisi.
Mzee, ukipenda ua penda na Boga lake,
Huwez chagua vya kuingizwa nchini mwako, kwa maana unatoa vyote pia,

Focus iwe kuweka uzalishaji wa ndani imara, sio kuzuia vya nje, wew hakikisha dar mayai yapo ya kutosha toka hapo pwani,
Hakuna ataeleta mayai ya Malawi,

Hizi habari za kulindana kwa kuzuia ni za kipuuzi na kijamaa,

Serikali naona iongeze wigo wa ruzuku, eg, ruzuku kwenye madawa ziongezwe, na pia kwenye mbolea, ili watu wafuge na walime zaidi na automatically tutawafukuza wanao import mayai na maziwa
 
Back
Top Bottom