Je, Kasi ya Magufuli itaua Upinzani Uchwara na Kuimarisha Upinzani Makini? - Prof. Kitila Mkumbo

upinzani uchwala ni kama wa CHADEMA waliokuwa wanapinga ufisadi sasa hivi mafisadi wanao kwenye chama chao kwahiyo watakuwa kimya na Magufuli atadhibiti ufisadi.

wao hoja zao ulikuwa ufisadi hawana sera mbadala upinzani unaotakiwa hivi sasa ni wa kukosoana kisera.

mfano CCM wakisema hawana fedha za kusomesha wanafunzi bure hadi chuo kikuu inatakiwa wao waje na mkakati waulezee kisomi hizo fedha zitatoka kwenye vyanzo gani.

Nani kakamatwa mpaka sasa akitokea CHADEMA?

We Mchwala kabisaaa. Bila Upinzani wa kweli hata Magufuli asingepata nafasi aliyo nayo.

Sera za Elimu bure, kubana matumizi ya serikali n.k. ambazo Hon. Magufuli anazifanya kwa sasa zipo kwenye Sera ya CDM.
 
Sina tatizo na anachosema Prof. Kitila Mkumbo kwani ndio demokrasia. Lakini ukijaribu kuungalia ACT ni chama kilichojengeka kama mpinzani halisi wa cdm na kinalengo la kujibu chuki yao kwanini walifukuzwa na hata wanapozungumza majukwaani unaona ile chuki yao halisi dhidi ya cdm. Huwa kinajinasibu kama chama bora na chenye sera bora tena kuliko cdm na kwa mtazamo wao sera hizo hata ccm wanazikubali!! Ni nadra sana kuwaona Act wakivitambua vyama vingine vya upinzani kama wapinzani bali cdm tu tena kwa chuki na hoja zao zinapata nguvu pindi ccm wanapowaunga mkono.

Wanachoshindwa kufahamu Act ni kwamba nchi hii ni nadra sana kujivunia sera bora kwani wananchi huchagua kiongozi kwa hisia na sababu nyingine kabisa mbali na sera. Kwa mtazamo wangu ni chini ya 10% wanaochagua kwa kuangalia sera. Wengi huchagua kwa rushwa, udini, ukanda, hofu na ushabiki. Mfano mrahisi mbunge pekee wa Act ni Zitto, na alikoshinda sio kwa ubora wa sera bali ukanda kwani hali hiyo aliijenga Zitto kwamba kwann waha wawape kura cdm (wachaga) badala ya muha mwenzao? Kwa hili Zitto amefanikiwa, je Prof ndio aina ya upinzani anaomaanisha? Kama kweli suala ni wananchi kujali upinzani wenye sera bora na sio sababu nyinginezo nilizotaja hapo juu, basi Act hawawezi kusema wana sera bora kwa kuwa na mbunge mmoja wakati ndio kilikuwa chama chenye wagombea wengi baada ya ccm. Kwa prof kama yeye kushindwa kujua aina ya wapiga kura naona kama ni kufikiria ndani ya box. Nimuhakikishie Professa iwapo si nguvu ya cdm basj hiki tulichokiona kwa ccm kumchagua Magufuli leo kisingetokea, ama anataka tuamini ccm waliogopa sera bora za Act ndio maana wakamchagua Magufuli ambaye alikuwa hata anapata tabu kuomba kura kupitia jina la chama chake?

Angalizo, wengi wa wasomi wetu ni watu wa nadharia na ndio maana ni nadra sana kukuta msomi anaendesha shughuli yake kwa mafanikio ukilinganisha na mwenye elimu ya wastani. Wengi wa wasomi ni watu wa kuajiriwa maana hawana matokeo mazuri kwenye shughuli zao. Mfano mrahisi ni hao Act waliamini kwamba chama chao kina sera bora kwani zimetungwa na kusimamiwa na wasomi, lakini matokeo halisi kwenye kura yanaonyesha ukweli wa hoja yangu.

CC: Pasco, Kitila Mkumbo
 
Mkuu tindo, nimekubali!.

Pasco
 
Ukawa bado wapo kwenye siasa za Kikwete bado hawajustuka mpinzani wao mpya (Magufuli) anahitaji tactics nyingine kumkabili na wasipokuwa makini next election hawataamini watakavyoshindwa.Binafsi nadhani viongozi wa upinzani wanahitaji akili na sura nyingine za viongozi.

Nakubaliana nawe kwa asilimia kadhaa lkn Kinachonisikitisha ni pale watu wanaposhangilia MAFANIKIO ya Mhe Magufuli kama tulivyofanya kwa Taifa Stars dhidi ya Algeria mechi ya kwanza iliyochezwa Dar. Taifa Stars ilikuwa inaongoza hadi Half time 2 - 0, tulishangilia sana lkn mwisho wa mchezo matokeo yalikuwa Tanzania Stars 2 Algeria 2, Hakuna aliyeamini! Utawala wa Mhe Magufuli kila mtu anaupongeza kwa jinsi alivyoanza lkn bado ana safari ndefu sana ya kuweka misingi imara na kurekebisha mifumo mibovu ambayo imeligharimu sana taifa letu. Kwa upande mwingine mtu mwaminifu kabisa hawezi kubeza upinzani wa Tanzania hata kidogo, kinachooneka tanzania ni pressure iliyosukumwa na vyama vya upinzani hasa UKAWA. Vyama vya upinzani ndio vilivyomuibua mtu kama Mhe. MAGUFULI.
 
Nimesiliza mada star TV nakusoma huu uzi. Nakubaliana na Kitila kwamba ni Upinzani makini ndio utakao survive kwenye siasa zetu hasa ukichukulia mambo ya JPM. Pia ni sawa kuwa upinzani UCHWARA hauna nafasi kwa sasa. Tunapopishana ni pale anapo-imply kuwa chama au vyama fulani ndio upinzani UCHAWARA apart from ACT. Ukichukua siasa na kuibuka kwa JPM utaona zina msukumo mkubwa wa upinzani alitumia neno MABADILIKO, M4C etc. Kwa agenda anayotimiza JPM inabidi vyama VYOTE vya upinzani vijitathmini. Na hapo ndipo tutaona vipi ni vyama makini. CCM au JPM ameshinda (katiba yetu inatoa msimamo huo) lakini kuna ideology na sera mbadala-ACT wanazao na CDM, CUF, NCCR wanazao. Na ideologies zinaweza kufanyiwa ukarabati kutokana na mahitaji ya wakati. Hata CCM inahitajikujitathmini na JPM aliomba achaguluwe na moja ya ahadi zake ni kuleta mabadiliko ndani ya CCM.
 
Mwisho wa siasa za Majitaka

zilizoasisiwa Na Magamba zaidi ya miaka kumi

iliyopita zimefikia ukingoni mwaka huh Na upinzani Yaani ni ukawa utastawi !!

Aina ya siasa hizo ni unafiki udini Na ukabila
 
ili ujue.upinzani.wa Tanzania unavyokabiliwa na changamoto lazima ushiriki kwenye field kama kugombea nafasi.sio kufanya siasa za kwenye media kama za huyo.prof.wa commedy.
UPINZANI Nchini unakabiliwa na kuminywa kwa kiasi kikubwa na chama tawala kupitia vyombo vya dola na mapungufu yaliyopo kwenye katiba.
Huyo ni Prof.Jina tu kwani maprof.waliomfundisha hawaongei ujinga kama huo.
Magufuli mpaka hapo hajatoa timeflame ya kutengeneza.katiba mpya wala hajasema kama atachukua maoni ya wananchi kama yalivyo.sasa utafuteje upinzani.kama UKAWA ambao ndio agenda yao?! pia kazi za magufuli hata zikiwa nzuri.kupita lulu bila kuingizwa kwenye katiba ni buree akija raisi mwenye utashi tofauti na yeye.
pia naamini kama kuna maprofesa wasio tumia tafiti katika kubwabwaja ni huyo Baba.nahisi alipewa huo.uprofesa kama zawadi.kwa kuwa pandikizi la chama tawala.kichwani.anazidiwa na hata machinga asiyesoma.
profesario adui yake ni upinzani kila.anapotoa maoni lakini haelewi namna upinzani unavyohujumiwa na kukosa equal praying ground na chama tawala.bado ana kisasi cha kufurushwa chadema
RiP ACT na prof.Anayeota ujamaa uliomshinda Nyerere na CCM.

Mkuu democracy sio kugawana wala sio kupendelewa. Ukishapewa haki ya kuwepo na ku practice democracy ni juu yako kutafuta sbb ya kuwepo na kukubalika na Wananchi. Na ukishaanza kufanya vizuri serikali inakutambua na unaanza kupewa ruzuku. Ukianza kupewa ruzuku lazima uelewe kuwa kwenye uchaguzi ujao kuna chama au vyama vitapambana ili vipate ruzuku au ili viongeze kiwango cha ruzuku. Ukiwa na siasa uchwara utaishia kusema nimeibiwa. Na mwisho wa siku chama kitakufa kama inavokufa nccr na tlp na may be Cdm. Its not about uwanja sawa. Its about mikakati na political agenda ambayo Wananchi walio wengi wataikubali. Mbona kuna nchi kama zambia malawi kenya nk vyama tawala vilishindwa. Inamaana watawala wake hawakuweza kutumia dola au walichoka kuwa madarakani walihitaji kupumzika.. Ukiwa na siasa uchwara lazima utaishia kulalamika kuwa unaonewa. Na mwisho wa siku chama kinapotea. Ukipata mbunge mmoja wa ziada ujue kuna chama kimepoteza mbunge mmoja then inabidi ujiandae kupambana next election as kitataka kurudisha kiti chake cha ubunge. Ukishindwa utadai umeibiwa mara uwanja wa ushindan sio sawa.
 
Wanabodi,

Leo asubuhi nimepata fursa ya kufuatilia mjadala live wa Star TV kuhusu kasi ya Magufuli kwenye kupambana na Rushwa na Ufisadi ambapo wageni waalikwa ni Renatus Mkinga na Prof. Kitila Mkumbo wa Chuo Kikuu cha DSM.

Prof. Kitila ameuta upinzani wa Tanzania ni upinzani uchwala, umekuwa ukiendeshwa na siasa za matukio rkwa kupigia kelele rushwa, na ufisadi, kwa vyama vya upinzani kuishitaki CCM kwa wananchi kuwa haijafanya hili, au haijafanya lile. Upinzani wa namna hii ni upinzani uchwala!, hivyo kasi hii ya Magufuli kupambana na ushwa na ufisadi, kutapelekea wapinzani uchwala kujikuwa wamekuwa pre-emptied na kukosa cha kusema kama Magufuli atafanikiwa kukomesha rushwa na ufisadi!.

Amesema katika hii kasi ya Magufuli kupambana na rushwa na ufisadi, bado hajasikia sera zozote katika vita hii, hivyo upinzani makini anaotoka na sera makini ndio pekee utakaoweza ku survive kwa sababu hata serikali ya Magufuli ilete mabadiliko makubwa kiasi gani, kama haya mabadiliko haya sera, dira wala dhima, upinzani makini wenye sera, dira na dhima, utaendelea kuipinga CCM na kusurvive!.

Kwa muktadha huu, jee Tanzania tuna upinzani makini au huu uliopo ni upinzani uchwala tuu?!. Na kama tuna upinzani makini, upinzani huo ni upi?!.

Nitashukuru kama tutaweza kumpata Prof. Kitila humu akatuendeshee hili somo la upinzani uchwala na upinzani makini, na kifo cha upinzani uchwala na kuibuka kwa upinzani makini nchi Tanzania!.

Nawatakia Jumapili Njema.

Pasco

CC. Kitila Mkumbo

UPINZANI uchwara ni.ule wa mbowe na timu yake, wanategemea matukio na makosa ya uzembe wa serikali bila ya kutoa clear alternative solutions or policies.

Chama tawala kikiwa makini na serikali ikiwa makini uzaa, kulazimisha, uibua upinzani makini
 
Nimesiliza mada star TV nakusoma huu uzi. Nakubaliana na Kitila kwamba ni Upinzani makini ndio utakao survive kwenye siasa zetu hasa ukichukulia mambo ya JPM. Pia ni sawa kuwa upinzani UCHWARA hauna nafasi kwa sasa. Tunapopishana ni pale anapo-imply kuwa chama au vyama fulani ndio upinzani UCHAWARA apart from ACT. Ukichukua siasa na kuibuka kwa JPM utaona zina msukumo mkubwa wa upinzani alitumia neno MABADILIKO, M4C etc. Kwa agenda anayotimiza JPM inabidi vyama VYOTE vya upinzani vijitathmini. Na hapo ndipo tutaona vipi ni vyama makini. CCM au JPM ameshinda (katiba yetu inatoa msimamo huo) lakini kuna ideology na sera mbadala-ACT wanazao na CDM, CUF, NCCR wanazao. Na ideologies zinaweza kufanyiwa ukarabati kutokana na mahitaji ya wakati. Hata CCM inahitajikujitathmini na JPM aliomba achaguluwe na moja ya ahadi zake ni kuleta mabadiliko ndani ya CCM.

Nina kubaliana na wewe Masiya kuwa kwa siasa za JPM ni chama cha upinzani makini kitakachosurvive. Huu ni kweli mtupu kwa sababu Mhe Magufuli namuona kama mwanaCCM mpinzani aliyeishi ndani ya CCM huku akiumizwa na matendo ya CCM na bila kutarajia wanaCCM wakamkabithi kijiti cha uraisi bila kutarajia, sasa CCM waisoma namba wenyewe! Ndugu yangu Masiya pamoja na elimu aliyonayo Prof Kitilaa na wasomi wengine kwa sababu wanazozijua kushindwa kujua mazingira magumu ya siasa wanayokabiliwa nayo vyama vya upinzani dhidi ya chama dola CCM, hata hivyo comments nyingi za watu wa ACT ni mtazamo hasi walionao dhidi ya upinzani hasa CDM. Kwa tanzania mpaka hapa tulipo na mazingira ya siasa za upinzani hatuna budi kuvipongeza vyama vya upinzani kwa vuguvugu la haya MAGEUZI yanayotokea kwa sasa kwa ni juhudi za UKAWA
 
Wapinzani uchwala wanadandia tu matukio kupata point za umaarufu na huruma! Prof. Yuko sawa kabisa, mfano kifo cha marehemu Alfonce Mawazo.
 
Mkuu democracy sio kugawana wala sio kupendelewa. Ukishapewa haki ya kuwepo na ku practice democracy ni juu yako kutafuta sbb ya kuwepo na kukubalika na Wananchi. Na ukishaanza kufanya vizuri serikali inakutambua na unaanza kupewa ruzuku. Ukianza kupewa ruzuku lazima uelewe kuwa kwenye uchaguzi ujao kuna chama au vyama vitapambana ili vipate ruzuku au ili viongeze kiwango cha ruzuku. Ukiwa na siasa uchwara utaishia kusema nimeibiwa. Na mwisho wa siku chama kitakufa kama inavokufa nccr na tlp na may be Cdm. Its not about uwanja sawa. Its about mikakati na political agenda ambayo Wananchi walio wengi wataikubali. Mbona kuna nchi kama zambia malawi kenya nk vyama tawala vilishindwa. Inamaana watawala wake hawakuweza kutumia dola au walichoka kuwa madarakani walihitaji kupumzika.. Ukiwa na siasa uchwara lazima utaishia kulalamika kuwa unaonewa. Na mwisho wa siku chama kinapotea. Ukipata mbunge mmoja wa ziada ujue kuna chama kimepoteza mbunge mmoja then inabidi ujiandae kupambana next election as kitataka kurudisha kiti chake cha ubunge. Ukishindwa utadai umeibiwa mara uwanja wa ushindan sio sawa.

Sidhani.kama unaishi Tanzania.labda kama upo basi umulikiwe tochi ili uelewe! kwa utaratibu wa uendeshaji wa uchaguzi unaona kuna nafasi ya chama cha upinzani kukabidhiwa nchi? ya ZANZIBAR yametokea mara ngapi? unaweza kupinga matokeo ya Urais hapa Tz hata kama una vielelezo? wakina kafulila,silinde etc.wanavyokwamishwa kwa maelekezo wanauopewa wakurugenzi.unaona ni sawa? Matokeo ya uchaguzi mpaka wananchi wapoteze.uvumilivu na kutaka kuvunja amani DSM unaona ni weredi wa tume na dola? Jecha kufuta uchaguzi wakati hana mamlaka na watawala wakasimamia unaona ni siasa.usitete hoja dhaifu za kuongea vijiweni huku Jf.refa anateuliwa na.mpinzani wako na kumlipa mafao yake kuna refa hapo.Walipo fika mpaka hapo oppositions parties zote nawapa pongezi.they.opperate under very hostile environment.mikutano/maandamano yanazuia na polisi na kuzuia ustawi wa democracy.
 
Huelewi unachoongea. Umefungwa. Nenda zambia wapinzani wamezuiwa hata kufanya mikutano ya hadhara but stil uchaguzi ukija ni ngumu chama kilicho madarakani kushinda. Nenda malawi utaelewa ninachokiongea. Fuatilia political history ya kenya jinsi akina kibaki walivostruggle kuiondoa kanu madarakani pamoja Na kuwa Wananchi walikuwa tayari. Uliza walifanya nn mpaka wakafanikiwa. Juzi wakati odinga anashindwa alikuwa ni waziri Mkuu lakini aliishia kuwa kaibiwa na uhuru.. Huelewi tu unachokiongea unafuata mkumbo. Siasa ni majority. Kama huna. Majority hata upendwe Vip huwezi kushinda.
Obama kwenye term yake ya Pili alishinda Kwa sbb alikuwa na Majority ingawa masenator na wabunge chama chake kilishindwa vibaya. Ingekuwa bongo tungesema kaiba vile alikuwa bado raisi. Chambua ww mwenyewe uone varidity ya hizo sentence. Sio kufuata mkumbo tu. Jaribu ku reason ukitumia ubongo wako vizuri.
 
Mkuu Pasco,

Hongera kwa andiko lako kuhusu kauli ya Prof. Dr. Kitila Mkumbo.

1. Hakika Kitila anadhani Upinzani imara utatoka ACT, Amekosea. ACT kwa sasa wanakosa pa kusimamia/kutokea (lack of Identity). Hawajui wawe wapinzani au waendelee kuichekelea CCM na kupokea ufadhili wao. Na ndio maana kuna taarifa zipo kuwa Kiongozi wao Mkuu anahaha kumsifia Magufuli na Spika Ndugai ili apate Uenyekiti wa PAC na kuendelea kufanya Parliamentary Politics.

2. Sera mbadala zipo za kutosha tatizo ni jamii yetu ambayo ina nakisi ya watu wanaojua kusoma nyaraka vizuri na kuzifanyia uchambuzi.

3. Kuna propaganda kuwa CDM inajijenga kupitia misiba hebu jiulizeni, aina kifo cha mawazo, wadhfa wa Mawazo ndani ya Chama, Propaganda za Polisi Mkoa wa Mwanza na hukumu ya Mahakama. Ni ukosefu wa fikra kutaka Mawazo azikwe kama mfu aliyefariki kifo cha kawaida.

4. Kitila ni mtu wa maslahi na siasa za Makundi toka akiwa CDM wala sishangai kuwa alikuwa mtu wa karibu wa Edward Lowassa kabla ya kuhamia CDM. Na ninawahakikishia kuwa Kitila ataendeleza siasa zilezile za Makundi ndani ya ACT, kuna taarifa kuwa kwa sasa wanaona kuwa Samson Mwigamba hana uwezo wa kuendesha chama wakati walikuwa na alliance kubwa sana toka wakiwa CDM. Huenda Mwigamba ameshindwa kulinda maslahi yao huko ACT na sasa wanaanza kumuandama, sitashangaa chochote kutokea hapo baadae.

Wasaalam.
 
Huelewi unachoongea. Umefungwa. Nenda zambia wapinzani wamezuiwa hata kufanya mikutano ya hadhara but stil uchaguzi ukija ni ngumu chama kilicho madarakani kushinda. Nenda malawi utaelewa ninachokiongea. Fuatilia political history ya kenya jinsi akina kibaki walivostruggle kuiondoa kanu madarakani pamoja Na kuwa Wananchi walikuwa tayari. Uliza walifanya nn mpaka wakafanikiwa. Juzi wakati odinga anashindwa alikuwa ni waziri Mkuu lakini aliishia kuwa kaibiwa na uhuru.. Huelewi tu unachokiongea unafuata mkumbo. Siasa ni majority. Kama huna. Majority hata upendwe Vip huwezi kushinda.
Obama kwenye term yake ya Pili alishinda Kwa sbb alikuwa na Majority ingawa masenator na wabunge chama chake kilishindwa vibaya. Ingekuwa bongo tungesema kaiba vile alikuwa bado raisi. Chambua ww mwenyewe uone varidity ya hizo sentence. Sio kufuata mkumbo tu. Jaribu ku reason ukitumia ubongo wako vizuri.

Naona ZANZIBAR hutaki kuongelea ulivyobiased! kenya wanatume huru baada ya ile ya KUVUITI-Marehemu kuvuruga uchaguzi wa kenya ukapelekea vita ya wenyewe kwa wenyewe.pia huelezi kama mfumo wa utendaji kazi wa tume upo kwaajiri ya ustawi democracy Tanzania au kulinda maslahi ya mtawala.
 
Back
Top Bottom