Siku chache kabla ya uchaguzi mkuu wa 2015 Dr Wilbroad Slaa wakati huo akiwa GS wa CHADEMA na akiwa mchezaji tegemeo ktk safu ya ushambuliaji aliwatosa wenzake dakika chache kabla ya mchezo kuanza...
Kila mtu (nikiwemo mimi) alipigwa na butwaa na mioyo ya matumaini ya ushindi dhidi ya CCM ikayeyuka kabisa wakati huo..
CHADEMA wakalipokea hilo. Wakasimama kiume, likapita na wakafanikiwa kuvuka salama...
Uchaguzi mkuu wa mwaka huo ukanyika. Hayati John P. Magufuli [CCM]akatangazwa mshindi dhidi ya mpinzani wake wa karibu Mzee Edward Ngoyai Lowassa [CHADEMA]...
John P. Magufuli akaapishwa na kukalia kiti cha Urais wa JMT.
Akaanza kutawala kwa mkono wa chuma. Na mwezi Februari, 2016 katika maadhimisho ya "birthday" ya CCM huko Singida, akatangaza vita ya kuangamiza vyama vya siasa vyote vya upinzani akikilenga zaidi CHADEMA..
Na kwa kuanzia akaanza kwa kupiga marufuku harakati zote za vyama vya siasa vya upinzani dhidi ya CCM kinyume cha sheria na katiba kufanya aina yoyote ya shughuli za kisiasa kama mikutano na maandamano pengine kwa fikra zake ili vidhoofike na kujifia vyenyewe..
Hilo likadumu na likazoeleka. Vilivyodhoofika na kufa vilipitia hiyo dhahama. Lakini CHADEMA iliendelea kuimarika ktk mazingira hayo hayo. Jiwe alishangaa na kustaajabu sana...
Akaja na biashara ya kununua wanasiasa wenye ushawishi fulani wapenda pesa kuliko utu toka upinzani wabunge, madiwani na yeyote aliyekuwa na nguvu fulani ya ushawishi kwa propaganda maarufu za "kuunga juhudi".
Hilo likapita, CHADEMA haikufa badala yake iliimarika zaidi na zaidi kwa kimo, kina, urefu na mapana. CCM wakapigwa na mshangao sana. Bila shaka akawa hajapata risasi sahihi ya kuulia...
Tukiwa hatuna hili wala lile, Rais John P. Magufuli akaleta mshangao mwingine tena kwa kumpa ubalozi nchini Sweden Dr Wilbroad Slaa. Yakasema yaliyosemwa kwa staili zote..
Lakini hilo nalo likapita, maisha yakaendelea, CHADEMA haikufa badala yake ikazidi kuimarika tena na tena na tena...
Mwaka 2017 mwezi Septemba ktk mazingira tata bila shaka baada ya mbinu ya kumnunua kwa fedha kushindikana, mwanasiasa na mwanaharakati maarufu zaidi kwa sasa ndugu Tundu Lissu na Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA alishambuliwa na kupigwa risasi ktk jaribio la kumuua saa 7 ya mchana kweupe katika eneo la makazi ya viongozi wa serikali Area D huko Dodoma..
Za ndani kabisa zinasema, mpango wa kumuua ndugu Tundu Lissu kwa staili hiyo ilikuwa ni maagizo ya Rais John P magufuli mwenyewe. Bila shaka hii inaeleweka maana ushahidi wa kimazingira unathibitisha madai haya...
Na baadaye (iwapo angekufa) script ya filamu hiyo ilikuwa ni kum - frame Freeman Mbowe (Mwenyekiti Taifa - CHADEMA) na baadhi ya viongozi wakuu wa chama, kuwa ndiyo wamepanga mpango wa kumuua mwenzao...
Isingeishia hapo. Freeman Mbowe na wenzake wangeshitakiwa kwa kesi ya mauaji na mahakama ingethibitisha na kugonga muhuri na hukumu isingekuwa kunyongwa hadi afe, bali kifungo cha maisha jela..!
Ingetokea hivyo, obvious huo ndio ungekuwa mwisho wa CHADEMA kwa kufutiwa usajili kwa kigezo kuwa hicho ni chama cha kigaidi na lengo la Magufuli lingetimia 100%..!
Asante Yesu Kristo kwani Mungu baba wa mbinguni alitenda muujiza wa kuzuia kifo cha mwamba Tundu Lissu. Filamu ikawa imeungulia huko huko studio...
Hilo likapita, CHADEMA ipo na ikaendelea kukua kwa kasi kwa kimo, kina, mapana na marefu...
Muhula wa kwanza wa Urais wa Magufuli ukapita. Ikaja 2020 tukafanya uchaguzi mkuu mwingine. Magufuli akitambua kuwa hawezi kumshinda Tundu Lissu, akaanza kwa kuvuruga mchakato na uchaguzi wenyewe wote. Na mwishoni alijitangaza mshindi...
Miezi michache baada ya Magufuli kuanza kutawala kwa muhula wa pili (2020 - 2025), ktk mazingira ya kutatanisha Rais John P Magufuli akaugua na kufariki mwezi March, 2021 Yaani aliyetaka kuua wenzake, akafa yeye...
It was a shock lakini ndivyo ilivyokuwa..!
Makamu wake Bi. Samia Suluhu Hassan akapokea kijiti kama sheria ya nchi (katiba) inavyoelekeza. Akaapishwa na akawa Rais kamili wa JMT..
Hakukaa sana na ktk mazingira tatanishi akatengua ubalozi wa Dr Wilbroad Slaa na kumrudisha nchini. Hakumpa kazi nyingine rasmi yoyote..
Katika mazingira tatanishi pia, ghafla ikazuka skendo ya mkataba tata na wa kiwiziwizi na kifisadi wa kuuza bandari zote za bahari na maziwa makuu za Tanganyika kwa anayedaiwa ni mwekezaji wa kiarabu kupitia kampuni ya DP World toka Dubai..
Dr Wilbroad Slaa akawa ni miongoni wakosoaji wakubwa wa makubaliano/mkataba huu na mwenye lugha kali za kuikera serikali na viongozi wake hasa Rais Samia Suluhu Hassan..
Kwa namna ya ukosoaji wake, akajikuta ameshitakiwa kwa kosa la uhaini. Alikaa ndani kwa muda mfupi na baada kosa kubadilika na kuwa ni la uchochezi na hivyo kutoka kwa dhamana...
Alipotoka tu kifungoni, Rais Samia Suluhu Hassan akamvua hadhi ya ubalozi...
Cha kushangaza bado ameendelea kukosoa na sasa lugha anayotumia kukosoa ni kali zaidi na yenye ukakasi wa kukera kuliko hata ilivyokuwa kabla ya kuwekwa ndani kwa kosa la uhaini...
Haya yakiwa yanaendelea, kumbe wameanzisha taasisi? Chama Cha siasa? kinachoitwa Sauti ya Watanzania.
Sina hakika ni rasmi imesajliwa au la. Humo ndani wako wengi akiwemo Wakili aliyejitokeza hivi majuzi na kujipatia umaarifu ghafla Adv. Boniface Mwambukusi toka Mbeya..
Sauti ya Watanzania wameandaa mikutano na maandamano yatakayokuwa hayana ukomo unless tu serikali itamke kuwa imeachana na mkataba wa kutoa bandari za Tanganyika kwa waarabu wa Dubai kupitia kampuni yao ya DP World..
Mikutano na maandamano kwa maelezo yao yatafanyika kwa kuanzia Mbeya, DSM, Arusha na Mwanza...
Hawa Sauti ya Watanzania wameingia kwenye mzozo na malumbano yasiyotarajiwa na chama kikuu Cha upinzani Tanzania - CHADEMA kwa wanachosema CHADEMA kukataa kushirikiana nao ku - push agenda zao za katiba mpya na kupinga mkataba wa uuzaji bandari ambazo wanadai ni agenda za CHADEMA pia..
Na CHADEMA japo kweli wanapigania kitu kimoja wameshindwa kushirikiana na hawa wanaojiita Sauti ya Watanzania kwa sababu wanazozieleza kuwa ni kutoshirikishwa mapema ktk hatua za maandalizi ili waone kama ushiriki wao hautaingiliana na mipango na programu za chama chao..
Bila shaka, mpaka hapo CHADEMA wana sababu za msingi sana. Na mimi nasema kumbe wana akili na ufahamu wa kuona mbali..
Hili limewaudhi Sauti ya Watanzania na wengine wasijiuliza na kuchuja mambo..
Kwa mtiririko wa matukio jinsi ulivyo, inanileta kwenye hoja juu ya kujiuliza huyu Dr Wilbroad Slaa ni nani na amesahau nini CHADEMA kiasi cha kutumia njia za kificho kurudi huko? Je, Kwamba alisahau kitu? Hakukamilisha kazi aliyopewa kuifanya na CCM...?
Kwa wasioelewa ni kuwa, kwa ngazi na cheo alichofikia serikalini, Dr Wilbroad Slaa bado ni afisa wa serikali na sehemu ya TISS ambayo currently inafanya kazi kujilinda CCM zaidi badala ya nchi..
Usishangae kabisa ukiambiwa hawa kina Dr Slaa, Mwambukusi, Mdude Nyangali ni wakala wa TISS ya CCM kwa staili hii ili kuwaingiza mkenge CHADEMA wanaotakiwa kufutwa na kupotezwa..
Hii ndiyo maana ya kauli mbiu maarufu ya huyu mwanamama Bi Samia Suluhu Hassan ya "KAZI UENDELEE". Maana yake ni kuendeleza alichokiacha Magufuli ikiwemo kuua na kutesa na kupoteza..
Sauti ya Watanzania ni mpango mzima wa TISS ya CCM kama ndoano ya kuwanasa CHADEMA wajae wenyewe kisha wajimalize. Hongera Freeman Mbowe na chama chenu kwa kutumia macho yeu ya ndani kuuona mtego huo..!