Raphael Alloyce
Senior Member
- Nov 15, 2020
- 169
- 389
TOLEO MAALUM – APRILI 2025
JE, KUNA DALILI ZA MAKUSUDI ZA KUHUJUMU UTHABITI WA TAIFA LETU?
Katika kipindi ambacho Tanzania inapiga hatua kubwa za kimkakati katika ujenzi wa miundombinu, uendelezaji wa sekta binafsi, na kuimarisha mapato ya ndani kupitia mageuzi ya kiuchumi na utawala bora, kumeibuka hali ya wasiwasi kuhusu uwepo wa baadhi ya watu wanaotaka kuvuruga uthabiti huu. Ni wazi kuwa mafanikio haya hayawafurahishi wote hasa wale ambao maslahi yao binafsi hayajafanikishwa kupitia njia halali na za kizalendo.
Lakini je, Serikali inaweza kuendelea kukaa kimya wakati baadhi ya watu wanashabikia propaganda, uchochezi na upotoshaji, kwa kisingizio cha uhuru wa kidemokrasia?
KWANINI WENGINE HUDHANI TANZANIA INAWEZA KUCHEZEWA?
Tanzania ni nchi iliyojijengea heshima kimataifa kupitia sera thabiti, diplomasia ya uchumi, na utulivu wa kisiasa. Hata hivyo, kuna dalili kuwa baadhi ya watu, wakiwemo wanasiasa na wanaharakati wachache, wanadhani wanaweza kuitumia nchi hii kama uwanja wa majaribio ya ajenda zao binafsi. Wanajificha nyuma ya neno "uhuru wa kujieleza" na kuibua hoja zenye harufu ya uasi, ilimradi tu wapate umaarufu au uungwaji mkono wa kisiasa.
Hili ni kosa la kimkakati. Tanzania si nchi ya majaribio ni taifa lenye misingi imara, linalosimamia nidhamu, sheria, na uzalendo.
MSTARI MWEMBAMBA KATI YA DEMOKRASIA NA HUJUMA NI UPI?
Katika mfumo wowote wa kidemokrasia, uhuru huambatana na wajibu. Lakini kwa baadhi ya watu, uhuru huo unaelekea kugeuzwa kuwa silaha ya kisiasa inayolenga kuvuruga amani na mshikamano wa kitaifa. Wanafanya hivyo kwa kueneza taarifa potofu, mashambulizi dhidi ya taasisi za dola, na kushambulia uongozi wa juu wa nchi kwa maneno ya kejeli na dharau, na kutumia viongozi wa dini kama silaha ya shinikizo.
UTEKELEZAJI UNATAKIWA LEO, SIO KESHO
Wananchi tunalojukumu la kuhakikisha utulivu wa taifa kabla hata ya vyombo vya ulinzi na usalama, waathirika wakubwa wa machafuko ni sisi wananchi. Ukiambiwa jambo kaa lichuje kabla hujachukua hatua ya kufanya uovu.
Taifa tuwe wenye kubishana kwa hoja sio kupata mihemko ya kuleta machafuko. Wote inabidi tulindwe na sheria sio kauli za watu fulani ambao wakishapata umaarufu wao hujiona wanaweza kufanya lolote na wakapata watetezi kwa haraka.
Kijana mtanzania ukweli mchungu ni kwamba, maisha yako yapo mikononi mwako, Serikali kazi yake kubwa ni kuweka mazingira wezeshi kukuwezesha kufikia malengo yako na kuijenga Tanzania imara. Sivyo, kama wale wanavyo wahubirieni kwenye majukwaa. Kama unaona kuna jambo haliko sawa jenga hoja sio kutukana, na kutisha watu, kufanya hivyo haitabadilisha hatima yako.
Wale wanaotumia mwanya wa kufahamika kimataifa kuleta uchochezi hatua madhubuti zichukuliwe kwa mujibu wa sheria. Wanaopaswa kuwajibika waonywe na, ikibidi, wachukuliwe hatua bila kuogopa kelele za watu wachache wanaotaka kuvuruga amani kwa kisingizio cha demokrasia.
TAIFA HILI LINA HISTORIA. LINA DIRA. LINA DHAMIRA.
Tanzania haiko sokoni. Sidhani kama wenye dhamana (viongozi na wananchi) watakubali kuchokozwa na maneno ya kejeli na misukumo ya watu wenye ajenda za kisiasa zisizo na maslahi kwa Watanzania.
"YA KUAMBIWA CHANGANYA NA YA KWAKO". LINDA AMANI POPOTE ULIPO.