Japan yaanza kutumia treni ya kasi zaidi kupita chini ya bahari

Shida hatujapata viongozi wenye dira ndio maana hakuna ubunifu. Wanaendekeza siasa na wataalamu wametelekezwa. Tunasindwa hata kujenga nja ya chini ya bahari kuvuka Kigamboni sehemu ambayo haifiki hata 300m. So painfull
juzi waliambiwa hawana dira wakaanza kufura kama chura na jana nimeweka uzi unaoonyesha dira ya rwanda wamekua mbogo sijui lini taifa hili litaelimika
 
treni za kawaida tuu manjanga si reli ya kati wala TAZARA zote zipo chini ya standard gauge. Sasa ndiyo tutaweza kuwa na treni zinazo pita chini ya bahari? au treni za umeme na umeme wetu huu wa kukatika katika..?

Mkuu sio mbaya kufahamu hiyo ballet train huwenda siku moja ukaenda huko sasa mora kupata info mapema sana sio unafika unaambiwa nenda metro station usafiri unajikuta unashangaa tuu hujui hiyo underground station ya kusafiri kwenye tunnels . Kwahiyo isikupe stress bali jifunze kitu hapa
Dah Mkuu wewe ni mwalimu ?? Unajua kutumia saikolojia kumfariji mtu kweli huenda nikasafiri siku moja asante kwa kunitia moyo
 
Sisi umeya wa jiji tu ni shida,huko Zenji ndo usiseme.Reli zetu zote ni kwa hisani ya WAGENI.
 
Wakati si tukizungusha mikono wenzetu wanazungusha ubongo, na hiyo ndiyo tofauti yetu na wao basi.
Go @Magufuli go,ulipo tupo.
 

Attachments

  • OTH_4628.jpg
    OTH_4628.jpg
    14 KB · Views: 40
DNA ya Tiffah lazima ijulikane, hayo matrain kwa Afrika sahau labda tuwe re colonised. Kwa hizi chaguzi za akina Jecha, nimeishiwa nguvu.
Huu niujinga kama sio upofu wakati tunaongea maswala yanayohusu maendeleo unachanganya habari.
 
Japan wamefungua mradi wao mpya wa treni ya kasi zaidi (Bullet train) unaopita chini ya bahari (Seikan Tunnel) na kuunganisha sehemu kaskazini ya kisiwa chake cha Hokkaido. Kwa hivi sasa kisiwa hicho kimeunganiswa na jiji la Tokyo na treni ya kasi zaidi. Mradi huo umegharibu takribani dola za kimarekani bilioni tano ($5 billion).

Kutoka Tokyo hadi Hokkaido kwa treni hii inachukua dakika 53 ikiwa inachukua dakika 90 kusafiri kutoka Tokyo hadi mji wa Shin-Hakodate ulioko Hokkaido inachukua dakika 90, ukijumla muda wa ukaguzi wa kiusalama yaweza chukua zaidi ya masaa 3. kwasasa kuna ushindani kati ya usafiri huo na ndege.

Seikan Tunnel ni njia kubwa kuliko zote za chini ya bahari inaurefu wa mile 33.4 (53.8 km).


0,,19143580_303,00.jpg

Japan Bullet Train, picha kwa hisani ya Reuters

OJ-AH785_JTRAIN_16U_20160325024215.jpg

Ramani kwa hisani ya WSJ

Tazama video hapa

Source:
Japan opens high-speed rail link to northern island of Hokkaido | News | DW.COM | 26.03.2016

Japan Opens First Bullet-Train Service to Island of Hokkaido

kubuni new technology kwao kumekua kama utamaduni aisee...pamoja n nchi kuharibiwa vibaya wakati wa WW2 lakini japan ni moja kati ya nchi zlilizoendelea zaidi duniani kiuchumi ikiachwa na marekani na china pekee..inastahili pongezi
 
Nchi nyingi za kiafrika viongozi sio committed ktk maendeleo they are just overwhelmed na political goals it is just being elected and re-elected. Nchi inatakiwa iendeshe like a business entity lazma tujue faida na hasara.. ukiona wamarekani wanaingia vitani ni for their nationa economic interest na wellbeing ya watu wao.

Sisi wa africa ni siasa tu mwanzo mwisho, bado tunahangaika na those three basic needs na i hope 300 years later bado tutakua tunazungumzia madawati ya wanafunzi
 
tukiweka malengo na mikakati imara tunaweza kufanya kitu fulani. upande wa teknolojia kwetu bado haujawa bayana. tunapanga kuongeza wanadayansi lakini wale wachache waliopo hutaanga nini hasa tufanye.
mbaya zaidi tunawabeba wanasayansi na kuwapa majukumu ya kisiasa badala kuwapa pesa waendeleze utafiti.
tunawapa fursa ya kusema uongo na kuiba
 
Back
Top Bottom