Jambo gani ulikuwa ukikatazwa utotoni na mzazi/mlezi ukahisi sio sawa ila huku ukubwani unashukuru sana kuwa yale makatazo yamekusaidia kuwa mtu bora?

Matongee

JF-Expert Member
Jun 17, 2023
614
1,492
Nilipokuwa mtoto kuna wakati nilikuwa naona wazazi hasa baba kama wamezidisha unoko ila kwa sasa ndo nimekuja kuelewa nilikuwa najengwa kuwa mtu bora. Haya hapa makatazo ambayo nilidhani ni ya kinoko kumbe yalikuwa mema sana.

1. Giza likiingia halafu usiwepo nyumbani balaa lake lilikuwa zito mno. Baba alikuwa ana utaratibu wa kula chakula jioni nyumbani hivyo mida ya saa moja moja huwa tuko nyumbani. Ikawa rahisi kwake kujua nani hayupo home.

2. Kanisa letu lina kambi za vijana na picnic za hapa na pale. Mzazi wangu alikuwa ni mgumu mno kuruhusu kuhudhuria hizo kambi. Nakumbuka kuna kambi ya vijana kanda ya kaskazini ilikuwa inafanyikia Mlima Shengena, Same ila ilikuwa ngumu sana mzee kukubali mimi na dada yangu kwenda. Ukubwani ndo nimekuja kwenye zile kambi watu hupigana miti kinyama bila kujali kama ni kambi ya kidini.

3. Kabla ya ujio wa simu zamani tulikuwa tunajiburudisha na magazeti ya Sani, Bongo na mengine. Ila kuna majarida yalikuwa yamejaa stori za ngono. Mzee akapiga marufuku majarida yote nyumbani kwake. Tuliishia kumaind kimoyomoyo.

4. Urafiki wa wazazi wangu na wale waalimu wanoko shuleni ulikuwa unanikera sana. Kuna siku nilifanya kosa shule nikamchenga mwalimu. Ile jioni tunatoka kuchunga namkuta yule ticha mnoko yuko na baba nje wanasikiliza DIRA YA DUNIA huku wakipata chai. Wote wawili walinipa kibano. Ila ndo miaka kadhaa baadae niligundua yule mwalimu alinipenda sana na aliona nitafika mbali.

5. Kwenda kanisani ilikuwa ni lazima na kutokwenda ni kosa lisilosameheka. Yaani yule mzee hata kama hajaenda lazima apate ripoti ya walioenda na ambao hawakwenda. Hadi leo hii nikiendaga home ikifika siku ya ibada najikuta tu naenda. Ile sheria ingawa kwa sasa sio lazima sana ila ndo hivyo ukiwa home unajikuta unaifuata.

6. Kipindi cha likizo huwa ni kazi tu hakuna mambo za kwenda tuition. Likizo zangu zote za O - level nilikuwa nakutana na programs mbalimbali zilizoandaliwa kitaalam na kuniweka bize likizo nzima. Nakumbuka likizo ya mwezi wa 6 nikiwa form four nilipelekwa Karatu kwenye shamba la ngano kupambana na ndege waitwao kwelea kwelea. Na baada ya form four ule muda wote wa kusubiria matokeo hadi kwenda form five nilifanya kazi kwenye mashamba ya vitunguu. Yaani mzee alihakikisha kuanzia kupanda hadi kupeleka kitunguu sokoni Kilombero nashiriki. Ndo kipindi nilijua kilimo cha Tanzania ni kama kamari tu.
 
Nilipokuwa mtoto kuna wakati nilikuwa naona wazazi hasa baba kama wamezidisha unoko ila kwa sasa ndo nimekuja kuelewa nilikuwa najengwa kuwa mtu bora. Haya hapa makatazo ambayo nilidhani ni ya kinoko kumbe yalikuwa mema sana.

1. Giza likiingia halafu usiwepo nyumbani balaa lake lilikuwa zito mno. Baba alikuwa ana utaratibu wa kula chakula jioni nyumbani hivyo mida ya saa moja moja huwa tuko nyumbani. Ikawa rahisi kwake kujua nani hayupo home.

2. Kanisa letu lina kambi za vijana na picnic za hapa na pale. Mzazi wangu alikuwa ni mgumu mno kuruhusu kuhudhuria hizo kambi. Nakumbuka kuna kambi ya vijana kanda ya kaskazini ilikuwa inafanyikia Mlima Shengena, Same ila ilikuwa ngumu sana mzee kukubali mimi na dada yangu kwenda. Ukubwani ndo nimekuja kwenye zile kambi watu hupigana miti kinyama bila kujali kama ni kambi ya kidini.

3. Kabla ya ujio wa simu zamani tulikuwa tunajiburudisha na magazeti ya Sani, Bongo na mengine. Ila kuna majarida yalikuwa yamejaa stori za ngono. Mzee akapiga marufuku majarida yote nyumbani kwake. Tuliishia kumaind kimoyomoyo.

4. Urafiki wa wazazi wangu na wale waalimu wanoko shuleni ulikuwa unanikera sana. Kuna siku nilifanya kosa shule nikamchenga mwalimu. Ile jioni tunatoka kuchunga namkuta yule ticha mnoko yuko na baba nje wanasikiliza DIRA YA DUNIA huku wakipata chai. Wote wawili walinipa kibano. Ila ndo miaka kadhaa baadae niligundua yule mwalimu alinipenda sana na aliona nitafika mbali.

5. Kwenda kanisani ilikuwa ni lazima na kutokwenda ni kosa lisilosameheka. Yaani yule mzee hata kama hajaenda lazima apate ripoti ya walioenda na ambao hawakwenda. Hadi leo hii nikiendaga home ikifika siku ya ibada najikuta tu naenda. Ile sheria ingawa kwa sasa sio lazima sana ila ndo hivyo ukiwa home unajikuta unaifuata.
Tufupishe story,

Kama asingekua baba sijuh ingekuaje 😁😁
 
Wazee wamenifanyia mengi nawashukuru ila kuna mambo mengine walikuwa wanazingua

Baba alikuwa hataki tuingize marafiki zetu ndani hata sebleni, hii ilikuwa inaniumiza sana kijamii

Mzee kuna kipindi TV iliharibika tulikaa miaka mitatu bila tv sebleni, kwake chumbani full dstv

Ila yote kwa yote kwenye msosi tume enjoy wali kila usiku, elimu alitukazania, Kuanzia Chekechea mpaka form 6 ni private, Chuoni sikupata mkopo ila sikuwahi kukwama kiuchumi, nilipomaliza chuo nikapewa gari.

Kwa sasa nami nimekuwa baba napambania watoto wasiishi chini ya maisha niliyoishi
 
Nilipokuwa mtoto kuna wakati nilikuwa naona wazazi hasa baba kama wamezidisha unoko ila kwa sasa ndo nimekuja kuelewa nilikuwa najengwa kuwa mtu bora. Haya hapa makatazo ambayo nilidhani ni ya kinoko kumbe yalikuwa mema sana.

1. Giza likiingia halafu usiwepo nyumbani balaa lake lilikuwa zito mno. Baba alikuwa ana utaratibu wa kula chakula jioni nyumbani hivyo mida ya saa moja moja huwa tuko nyumbani. Ikawa rahisi kwake kujua nani hayupo home.

2. Kanisa letu lina kambi za vijana na picnic za hapa na pale. Mzazi wangu alikuwa ni mgumu mno kuruhusu kuhudhuria hizo kambi. Nakumbuka kuna kambi ya vijana kanda ya kaskazini ilikuwa inafanyikia Mlima Shengena, Same ila ilikuwa ngumu sana mzee kukubali mimi na dada yangu kwenda. Ukubwani ndo nimekuja kwenye zile kambi watu hupigana miti kinyama bila kujali kama ni kambi ya kidini.

3. Kabla ya ujio wa simu zamani tulikuwa tunajiburudisha na magazeti ya Sani, Bongo na mengine. Ila kuna majarida yalikuwa yamejaa stori za ngono. Mzee akapiga marufuku majarida yote nyumbani kwake. Tuliishia kumaind kimoyomoyo.

4. Urafiki wa wazazi wangu na wale waalimu wanoko shuleni ulikuwa unanikera sana. Kuna siku nilifanya kosa shule nikamchenga mwalimu. Ile jioni tunatoka kuchunga namkuta yule ticha mnoko yuko na baba nje wanasikiliza DIRA YA DUNIA huku wakipata chai. Wote wawili walinipa kibano. Ila ndo miaka kadhaa baadae niligundua yule mwalimu alinipenda sana na aliona nitafika mbali.

5. Kwenda kanisani ilikuwa ni lazima na kutokwenda ni kosa lisilosameheka. Yaani yule mzee hata kama hajaenda lazima apate ripoti ya walioenda na ambao hawakwenda. Hadi leo hii nikiendaga home ikifika siku ya ibada najikuta tu naenda. Ile sheria ingawa kwa sasa sio lazima sana ila ndo hivyo ukiwa home unajikuta unaifuata.
1.kuamshwa alfajiri ya saa 11:00 na kulala kabla ya 4:00... Nilikuwa naona mateso sana ila baadae mwili ukazoea sasa naona faida yake....

2. Kufanya kazi nyumbani ni lazima... Hata kama mwanaume utachota maji, utapiga deki ndani na chooni, utapika, utaosha vyombo... Na zamu imewekwa kabisa... Maana shule sio tiketi ya uvivu wa kufanya kazi za mikono
 
Nilikuwa ninakatazwa kwenda disco vumbi,sherehe sherehe sijui za harusi,mikusanyiko mbalimbali kwangu ilikuwa ngumu kunikuta na ikitokea labda nyumba jirani kuna harusi basi mimi ni majukumu tu labda jioni saaana nahudhuria dakika 15 jua likitua nyumbani.

Mpaka leo hii matukio yanayonitoa nyumbani ni soccer. Habari sijui kaja msanii gani,lipigwe disco la kupasua miamba jirani na nyumbani kwangu hapo mimi watakuwa wananipigia kelele tu.
 
Jua likiwa linazama nawewe uzame nalo ndani, hakuna kutoka bila ruhusa na ukitoka lazima uage.

Kumiliki Simu na matumizi yake kwa ujumla, katika kitu nilikuwa nachukia ni kuambiwa habari za simu ila sasa nawashukuru wazazi waliniepushia mengi.

Mapenzi, mama alikuwa akiniimbia kila siku kuhusu kujihusisha na mahusiano, alikuwa akiniambia soma mwanangu hayo mambo utayakuta mpaka utayakimbia. Nilikuwa namind lakini nmekuwa nimeyaona.

Hakuna mazoea ndugu wakike, mama alikuwa hataki kabisa nizoeane na ndugu wa kike(mabinamu) pindi watutembeleapo nyumbani kipindi cha likizo. Hakutaka ukaribu uliopitiliza alikuwa ananiambia we ni mwanaume na hawa ni dada zako usijethubutu kufanya ujinga wowote. Nadhani alikuwa akinihusia hayo kutokana na tabia za hao mabinamu. Nilikuwa naona kama anaongea mambo ambayo hayapo kabisa ila kadri nilivyozidi kukuwa nilimuelewa sana.
 
Kupokea vitu kutoka kwa watu yaani ukipewa kitu na ukaenda nacho home hata kama cha kawaida unapigwa maswali sometimes na kichapo juu. Nilikuwa nakasirika sana ila hivi sasa naelewa kwanini wazazi walikuwa wanamind hicho kitu
 
1. Saa 06 - 07 PM niwe ndani nyumbani, halafu kwa nje bado unasikia washkaji bado wanakimbizana

2. Kuchota maji, hasa kipindi cha shida ya maji mnaamka saa 10 usiku

3. Siku mzee akishinda nyumbani hakuna kutoka nje, ila nilichokuwa nampendea mzee, sometime akienda bar kujichangamsha na marafiki zake, alikuwa ananichukua naenda kununuliwa chipsi Yai na soda

4. Kula kwa watu, lakini wao kuja kula kwetu freshi wanakaribishwa

5. Wakiume kucheza na wakiume wenzao, na wakike kucheza na wakike wenzao
 
Back
Top Bottom