Mtoto Wabibi
JF-Expert Member
- Apr 29, 2016
- 451
- 294
- Thread starter
- #21
Kikwete ni Charismatic leader, Mwalimu alilijua hili, Lowasa alilitambua hili, Mkapa aliliona hili.
Ubovu wa Kikwete ni Usimamizi lakini ilipokuwa linakuja suala la kuonyesha Leadership, huyu mtu ni Kiongozi.
Halafu huyu mtu ni mwanajeshi, Kafundisha siasa jeshini. hawezi kubabaishwa na vi crisis vidogovidogo vya kisiasa.
Huyu mtu aliongoza Unification ya TANU na ASP zanzibar kutengeneza CCM upande wa Zanzibar, utambabaisha kwamba hajui siasa za nchi hii na CCM?
Huyu mtu alikuwa ana enlist watu kwenda vitani Uganda, anajua maana ya mapambano, uvumilivu na kusimamia unachokiamini.
Kikwete ana roho ya utu, ni binadamu kwelikweli, tumeona akifariji watu misibani, kwa vigogo hata watu wa kawaida, tumeona akiwatoa akina Diamond Platinumz na kuwapa platform ( Diamond alipata audience nchi nzima mwaka 2010 pale JK alipomuintegrate ktk timu ya waimbaji kwenye kampeni zake, before that Diamond alikuwa hajapata jina sana), Kuna kina Ray C wamesaidiwa na mzee ktk ishu ya madawa ya kulevya.
Bob Marley aliimba
" You can't miss the water, until your well runs dry.
No matter how you treat them, Men will never be satisfied"
naunga mkono hoja..! washikaji tutamisi sana huyu tozi