jebs2002
JF-Expert Member
- Sep 3, 2008
- 9,397
- 8,582
Mzee kichwa sana sana huyuWaziri Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Sinde Warioba, amewataka wanajeshi kuepuka kuingilia siasa, akisisitiza kuwa kazi yao ni kulinda usalama wa nchi. Akizungumza na wanahabari Disemba 4, 2024, Warioba alikumbusha historia ya machafuko kutoka nchi jirani na kusema jeshi lilifanikiwa kudhibiti mikoa ya mipakani kama Katavi, Kigoma, na Kagera. Alionya kuwa kuingiza jeshi katika siasa kunaweza kuhatarisha usalama, akitoa mfano wa ufanisi wa jeshi katika vita ya Uganda.
"Tangu Uhuru watu wa Kongo, Burundi, Rwanda wamekuwa na machafuko, wananchi wa huko walikuwa wakikimbilia huku na wengine wakitaka kuendeleza harakati zao kutoka ndani ya nchi yetu, jeshi letu lilidhibiti mikoa mbalimbali hasa ile ya mipakani kuanzia Katavi, Kigoma, Kagera kukawa salama kabisa."
"Mnajua chokochoko iliyotokea Uganda, na mnajua kazi iliyofanywa na jeshi, tulipoteza vijana wengi sana, wale wameapa kuifia nchi na waliifia nchi, tusije tukawaingiza kwenye haya matatizo ya kisiasa, wananchi wakaanza kuwaona nao wanapendelea upande mmoja. Mimi ninaomba kabisa jeshi la ulinzi lisije likaingizwa kwenye mambo ya siasa, siyo kazi yake, kazi yake ni kulinda usalama wa nchi".