BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,812
Jaji amesema nchi haitapungukiwa chochote ikiwa itaruhusu watu binafsi na wagombea kupinga matokeo ya Urais Mahakamani.
Ameongeza kuwa "ukishasema kwenye Katiba kwamba Mahakama ndiyo Mamlaka ya mwisho ya Kisheria, basi mzozo wowote unapaswa kufika kwenye Mamlaka hiyo ya mwisho ya kisheria".
Kwa mujibu wake, kwasababu Tanzania ni nchi ya Demokrasia ya vyama vingi ambapo kunakuwa na Chaguzi za ushindani, hivyo Tume ya Uchaguzi haiwezi kujihukumu yenyewe kwa sababu ndiyo inayotangaza matokeo.
Kuhusu Mabadiliko ya Katiba Juu ya Uchaguzi Mkuu
Amezitaja nchi za Kenya, Afrika Kusini, Malawi na Uganda pamoja na baadhi kutoka Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kuwa zilifanya mabadiliko ya Katiba yanayoruhusu uwasilishaji wa Pingamizi la matokeo ya Uchaguzi wa Urais Mahakamani.
Aidha ameongeza kuwa "Tunatakiwa kukubaliana kwamba tunahitaji Tume yenye nguvu, pia tukubali kuweka viwango kama wenzetu wa Kenya. Katiba lazima iwe wazi, Teknolojia iwe rahisi na inayowajibika na vile vile uwazi. Nadhani tukishakuwa na masharti haya yote, tunaweza kuchukua hatua zaidi,”.
Kwa mujibu wa Jaji Chande, kutoruhusu matokeo ya Uchaguzi wa Urais kupingwa Mahakamani kunakuwa na pengo, pia Katiba inapaswa kusema nani anaruhusiwa kupinga, sababu za kupingwa na muda unaohitajika kwa Mahakama kutupilia mbali Pingamizi.
BBC Swahili