Inawezekana vipi video za Millard Ayo ziko clear kuliko TBC?

wapo wanaofanya live video streaming kupitia youtube
je itahitaji vifaa extra?

na wanao charge watu kupata hizo live video streaming wanatumia teknolojiaa ipi?
unaweza charge watu kutumia youtube?
kufanya live streaming, hauhitaji kitu chochote zaidi ya kamera na computer, tena kuna baadhi ya kamera zina connectivity kabisa na kurusha direct bila kupitia kwenye compyuta.

Ila kurusha kitu kizuri, unahitaji production equipment's na sio kamera tuu, unahitaji kamera zaidi ya moja, angalau 3, mixer, taa, tripods, mic nzuri, etc. Full simple production sets cost around $ 10,000-100,000 kwa ma studio ya ukweli.

Kupitia simu tuu mtu unaweza kufanya streaming.

U tube bado ni bure.

P.[/QUOTE]


Zipo Channel za youtube unalipia
ndo maana nikajiuliza
mtu akitaka iwe hivyo anafanyaje?
 
Kuanzia fundi mitambo hadi watangazaji ccm what do you expect
 
Sidhani kama Millard Ayo tv ana record matukio yake na camera ya simu, ile ni camera yenye pixel kubwa kubwa na new technology ,
 
Nimecheka sana nilipokuwa nafuatinia SUPER BRAND kwenye michuano ya SPORT PESA hapo kwenye kuonyesha live ndio utagundua tofautti ya vituo
 
Unashangaa video mkuu
Angalia hospital za watu binafsi zina dawa na huduma nzuri kuliko hospitali za serikali.

Angalia shule za serikali zinafaulisha kuliko shule za serikali.

Angalia wafanyakazi wa serikali wanaishi kwa shida kweli kweli kuliko wafanyakazi wa private sectors.

Serikali yoyote inapokua serikali ya wapiga dili mambo lazima yawe hovyo.

TBC haivutii hata kutazama, muonekano wake ni hovyo utadhani ndo tunaangalia zama za vita ya Idd Amin na Nyerere.
 
Na kwa kuongezea TBC ni FTA wakati Azam ni Cable. Kutangaza FTA ni more expensive. Kutangaza Cable ni cheap.

Tunakokwenda kila mchungaji, Gwajima, Mzee wa Upako, Kakobe,Rwakatare etc watakuwa na channel zao kama Mwingira, Agape na TB Joshua. Kila kanisa litakuwa na TV yake, na sisi Watangazaji tutakuwa na channel zetu, AYO TV, PPR TV, Joyce Kiria TV, Albert Kilala TV, Salama Jabir TV, Zamaradi Mketema TV, etc.

P.[/QUOTE]

Pascal Mayalla,
Kuna ombwe kubwa sana YouTube la documentary na habari za kina (10 minutes) kuhusu masuala ya kiuchumi, usafiri, utalii, biashara, vyuo vya elimu ya juu, sayansi & technolojia n.k katika lugha ya Kiingereza Tanzania.

Nakupa changamoto la kuziba uhaba za suala hilo ktk lugha ya Kiingereza hasa katika dokumentari na habari za kina fupi za waandishi freelance kama wewe. Usibweteke kukaa kusubiri uitwe kwa ''bahasha ya kaki'' na taasisi, kampuni, shirika, chuo n.k nenda wavamie waeleze umuhimu wa habari zao kufahamika ulimwenguni achana na ''ukongwe''.

Jitume kama Millard Ayo aliyebobea ktk habari za Kiswahili ila wewe lenga Kiingereza, usiwe na wasiwasi waachie jamaa wajieleze kwa Kiingereza fasaha rahisi (Plain English) na matunda yake utayaona, utakuwa unaitwa na dau watapandisha wenyewe baada ya ''kujitoa'' kwanza kuonesha umuhimu ya habari ktk Kiingereza. Na pia si ajabu mashirika na wadau wa nje wataanza kukufukuzia kwa vile umeonesha umahiri wa kuitangaza Tanzania kupitia jicho la Mtanzania ktk Lugha ya Kiingereza. Na utaanza kuwa kama 'Reuters'' ya Tanzania kuhusu habari mbalimbali toka Tanzania ktk ''lugha ya kwanza ya media ktk dunia'' na kujiongezea kipato.
 
Na kwa kuongezea TBC ni FTA wakati Azam ni Cable. Kutangaza FTA ni more expensive. Kutangaza Cable ni cheap.

Tunakokwenda kila mchungaji, Gwajima, Mzee wa Upako, Kakobe,Rwakatare etc watakuwa na channel zao kama Mwingira, Agape na TB Joshua. Kila kanisa litakuwa na TV yake, na sisi Watangazaji tutakuwa na channel zetu, AYO TV, PPR TV, Joyce Kiria TV, Albert Kilala TV, Salama Jabir TV, Zamaradi Mketema TV, etc.

P.[/QUOTE]

BILA KUSAHAU JAMIIFORUMS TV:)
 
Na kwa kuongezea TBC ni FTA wakati Azam ni Cable. Kutangaza FTA ni more expensive. Kutangaza Cable ni cheap.

Tunakokwenda kila mchungaji, Gwajima, Mzee wa Upako, Kakobe,Rwakatare etc watakuwa na channel zao kama Mwingira, Agape na TB Joshua. Kila kanisa litakuwa na TV yake, na sisi Watangazaji tutakuwa na channel zetu, AYO TV, PPR TV, Joyce Kiria TV, Albert Kilala TV, Salama Jabir TV, Zamaradi Mketema TV, etc.

P.

BILA KUSAHAU JAMIIFORUMS TV:)[/QUOTE]
Mkuu Madukwappa, umenikumbusha, tena kuna wakati tulianza, sijui imepotelea wapi, ila kwa upande wa vifaa, JF wako kamili sana.

Kuna wakati nilitoa ushauri huu jf,
Vipindi Maalum vya JF kwenye TV: Naomba Maoni Yako! | Page 2 ...

P
 
Inaingia vipi akilini kuwa Television ya Taifa/TBC ambayo ina unlimited budget na resources za video zake zina kiza na mwingu lakini video zinazotolewa na huyu kijana Millard Ayo ambaye videos zake ni za Simu ya mkononi ni High Definition (HD) na ni ziko clear.

Mfano tazameni video ya TBC za bunge kwenye Youtube. Utadhani bado tuko kwenye miaka ya 1950's

Naomba waziri husika alifanyie kazi hili. Haya mambo ya sub standards na kuzugazuga hayana nafasi kwenye zama hizi
Jibu lako ni rahisi sana
Namajibu yako ni mawili tu hapa

1: millad ayo anatumia cameras ambazo tunaziita DSLR cameras ambazo tunaiata Digital Single Lens Reflex camera hizi zinapiga HD kwamana frame ya 1920 x 1080 au zaidi ya HD kwamaana ya 2k au 4k au 6k nakuendelea, sasa milad anapoedit kipindi chake huwa anakipandisha youtube kwa quality ile ile ya HD maana yy ni online Tv na si kama TBC wao wanaingia kwenye Multplex kuja kwenye vingamuzi vya star times ambavyo sasa sio HD bali Ni SD kwamaana ya STANDARD DIMANTION ambayo ni 720 x 576 frame. Kwahyo basi tukija kwene camera za wenzetu TBC wao wanatumia camera ambazo sio full HD na sio Full Frame kwamaana zinapiga may b 1080 x 720 50i frame ambayo sio full HD sasa wanapo edit nakupeleka kwenye play out hata kama itakuwa kwa quality hiyo bado itashuka maana multplex ya star times ni SD na sio HD kwahyo itakuwa encoded kwenda kwenye 720 x 576 frame so quality inashuka inapofika kwa mtumiaji mwenye king, amuzi cha SD cha star time .ndio maana Azam wao wana HD ving, amuzi wao picha zao zinapungua kiasi sana quality ila wao ving, amuzi vyao ni HD hata multplez yao inauwezo wa kurusha HD.

Pili ni je unapewa MBPS ngapi katika Space yao hao star times nayo ina mata kwenye quality .ila pia wao TBC wanaweza ku shut Kwa quality yao ile wakaweka youtube na wakawa na quality nzuri .

NOTE. : Quality inapotelea hapo kwenye Multplex
 
Mkuu Post Truth, uko right, TBC ndio TV ya kwanza nchini Tanzania kutumia technolojia ya DV, (Digital Video), wakati TV nyingine zote zikitumia VHS. Japo TBC ilikuwa ikitumia DV Signal, ila transmiter yake ilikuwa Analog.

Baadae vituo vingine vikaingia kwenye DV kwa kununua TX za DV lakini TBC nayo ikanunua TX ya DV. Technology ikachange kwenda kwenye HDV, TV zote zikahamia kwenye HDV lakini TX ya TBC, ITV na Star TV bado ni DV, Clouds na EA TV ndio HDV. Azam TV ndio ameingia na Full HDV na TX yake ni Full HD

Kwa sasa technology ni 4K kwa kutumia UHDV, Bara la Afrika sisi bado, the Best signals za TV kwa Tanzania zinaongozwa na Full HD za DSTV channels za Super Sport, zikifuatia na Azam, ambayo ni HD, Clouds na Eatv ni HDV, ITV, TBC, Star TV na Channel Ten bado wanatumia DV tx.

Dogo Millard AYO anatumia Full HD!.

NB. Mimi ni Broadcast Journalist, taarifa hizi ni kwa mujibu wa reception yangu na sio specification toka vituo vyenyewe!.

Paskali.
Soma uzi wangu apo juu utaelewa .bado ujawapa maana halisi KWANINI QUALITY YAO MBOVU? KUNA SABABU KUBWA AMBAYO NIMEELEZA. HII ULIYOSEMA NI JIBU ZURI JAPO SI KWA SWALI HILI NADHANI KWA TECHNICAL MTU NI NGUMU KUKUELEWA. ILA UMEFAFANUA VYEMA PASCAL
 
Kuna kipindi nilikuwa nchi fulan hivi. Na iyo nchi ilikuwa inacheza na Taifa stars pale uwanja wa Taifa. TBC ilikuwa inarusha Match live.
Niliambulia matusi sana kwa kuwa tupo under technology. Nadhani sababu ni hii
 
Back
Top Bottom