SoC04 Inawezekana Tukawa Taifa Lenye Kujitegemea miaka 30 ijayo

Tanzania Tuitakayo competition threads

Economist Jay

Member
Feb 18, 2016
41
50
Leo nitachangia kidogo sana kupitia mpango wa maendeleo ambao watu wengi wanaweza kuuona kuwa ni wa ajabu sana.

Nianze kwa kuuliza swali, inatufaidia nini kuwa na mbuga nyingi zinazoingiza kidogo sana kwenye pato la taifa ikiwa watu wake wana shida ya maji, afya na barabara huko vijijini?

Tufanye hivi, tukodishe mbuga za wanyama mbili tupate trilioni 100, kwa maelekezo kuwa baada ya wao kutulipa gharama za kukodisha, tutakuwa tunawakata kodi kwa miaka 15 katika mbuga hizo maana watakuwa wanafanya biashara ya utalii na uwindaji. Kisha wanarudisha hizo mbuga baada ya miaka hiyo kuisha.

Pesa hii trillion 100 tunaitumia ku invest katika viwanda hapa nchini pamoja na kurekebisha maisha ya watu wa vijijini kwa kuwajengea barabara za kiwango cha rami.

Inatufaidia nini kuwa na mbuga ambazo hatuli nyama pori na wala hatuingizi pesa nyingi kulingana na uthamani wa mbuga hizo.

Tumepewa kazi ya kuzilinda kwa faida ya watalii tu? Kwa nini tusiwakodishie kwa mkwanja mrefu kisha tukate kodi kwenye biashara yao ya utalii na uwindaji?
 
Kumbe lengo la kukodisha ni ili biashara ifanyike ya nyamapori, uwindaji na utalii?

Kuna utofauti gani na sasa ambapo watu hulipia kwa serikali mojakwamoja kufanya huo utalii, wanalipia vibali na vitalu vya kuwinda nyamapori?

Je unarudi kwenye akili inayotutafuna ya kuamini kwamba nchi haiwezi kuzitumia rasilimali zake yenyewe chini ya serikali hadi aje muwekezaji tokea nje?

Hilo linaweza kufaa zaidi katika uwekezaji mkubwa wa mitambo mikubwa mfano mafuta na gesi (japo naamini kama nchi bado inaweza kujikusanya kwa muda na ikaifanya anyway). Lakini hadi mambo ya kawaida kama kuwinda na kuongoza utalii kweli ujuzi wetu haujatosha? Tunaweza nini sasa mleta mada?
 
Maana imeonekana hatuwezi kuzitumia mbuga vizuri😂😂😂 ni bora kuamua kufanya yale yasiyowezekana
 
Back
Top Bottom