SoC04 Nini kifanyike, kama sio kuondoa basi kupunguza mikopo kufadhili bajeti ya nchi kufikia miaka 5 hadi 25 ijayo

Tanzania Tuitakayo competition threads

Rajieh01

New Member
Apr 18, 2024
2
1
Utangulizi
Tanzania kama nchi nyingine yingi zinazo endelea inakabiliwa na ukopaji wa fedha kutoka Kwa wafadhili mbalimbali wa ndani na nje ya nchi kufadhili bajeti ya Taifa. Utatuzi wa changamoto hii unahitaji maoni si ya wataalamu na viongozi wa kisiasa pekee, bali kuwapa nafasi wananchi kushiriki katika utoaji wa maoni Kwa serikali yao ili kuchocheo ujio wa mawazo mbadala. Yafwatayo ni maoni ya Nini kifanyike ili kupunguza ukopaji wa fedha kufadhili bajeti ya taifa kufikia miaka 5 hadi 25 ijayo.

Maoni
1. Kufuatia uwepo wa ukopaji fedha kama taifa kufadhili bajeti ya nchi na wakati mwingine mikopo iyo kutumika kulipa deni la taifa na hati fungani zinazoiva, kama taifa Kuna haja ya kutafuta njia mbadala za kupunguza ama kuondoa mikopo ya aina hii, kwani inaweza changia kuongezeka Kwa deni la taifa, kuongeza utegemezi wa taifa na hata wakati mwingine kuingiza uhuru wa taifa matatani ikiwa mikopo iyo Ina masharti magumu. Kwa mfano bajeti ya mwaka 2023/24, "misada na mikopo ya masharti nafuu kutoka Kwa washirika wa maendeleo inakadiriwa kufikia TZS 5.47 trillion, aidha serikali inatarajia kukopa TZS 5.44 trillion kutoka soko la ndani, ambapo TZS 3.54 trillion zitakuwa Kwa ajili ya kulipia hati fungani zinazoIva na TZS 1.90 Kwa ajili ya kugharamia miradi ya maendeleo, pia 2.10 trillion kutoka vyanzo visivyo na masharti nafuu Kwa madhumuni ya kuongeza Kasi ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo" (Tanzaniainvest.com). Ivo basi, kufwatia maelezo na mfano uo Kuna uhitaji wa juhudi za makusudi kupunguza kama si kuondoa ukopaji fedha kufadhili bajeti.

Nini kifanyike
Ianzishwe harambee ya kitaifa itakayo simamiwa na wizara ya fedha. Dhumuni la harambee hii itakua si nyingine Bali kufadhili bajeti ili kupunguza kama si kuondoa ukopaji wa fedha kufadhili bajeti ya nchi. Harambee iyo ifanywe miezi miwili au mmoja kabla ya bajeti ya wizara ya fedha kusomwa na waziri mwenye dhamana. wananchi watangaziwe siku ya kufunguliwa harambee iyo miezi mitatu au zaidi kuelekea kuwasilisha bajeti bungeni ili mara baada ya bajeti ya jumla kupitishwa na bunge basi pesa izo ziwe tayari zimekusanywa kwaajili ya kuongeza mapato kufadhili bajeti ya nchi. Lakini harambee iyo itakua si ya lazima na haitalenga kuongeza mlundikano wa Kodi Kwa wananchi bali itakuwa hiara. Wazo la harambee hii ni matokeo ya mafanikio ya harambee kadhaa zilizo fanyika kuichangia timu ya taifa, ivo ni imani yangu ya kwamba wananchi na wadau mbalimbali wakiandaliwa Kwa kupewa elimu yakutosha harambee hii inaweza kua na mafanikio na shauku kubwa Kwa wananchi Kwani matumizi yake ni Kwa manufaa na ustawi wa wananchi wenyewe, ivo mapato yatakayo kusanywa yataweza kufadhili bajeti kulingana kadri itakavyo kusanywa.

2. Kufuatia kuepo Kwa mataifa mengi ya yanayoendelea kama Tanzania kua na uwezo wa kukopesha fedha Kwa mataifa mengine na hatimaye kuwa wanufaika wa riba kutoka Kwa wakopeshwaji wao kumekua na tija kwani ni chanzo mbadala Cha mapato Kwa taifa. ivo basi ni shauku yangu kuona ya kwamba baada ya miaka 20 hadi 25 ijayo, Tanzania iwe na uwezo wa kukopesha mataifa mengine ili kujiongezea vyanzo vya mapato kama Taifa.

Nini kifanyike
Ianzishwe akaunti ya serikali itakayo simamiwa na serikali kupitia wizara ya fedha kwamba kuanzia miaka 5 hadi 20 ijayo serikali kupitia vyanzo vyake vya mapato viwe na utaratibu Kwa kuweka kiasi fulani Cha pesa Kila mwaka wa bajeti ili kuweka fedha kama mtaji lakini vile vile kutenga kiasi fulani Cha fedha za misaada Kwa ajili ya akaunti hii ili kuweka kuanzia miaka 5 ijayo, ivo kufikia miaka 20 ijayo kama nchi tuwe na uwezo wa kuanza kukopesha mataifa mengine Kwa vile itakavyo wezekana kufadhili bajeti Kwa siku za usoni, lakini ikishindikana itaweza tumuka kama akiba Kwa kutengenezewa Sheria maalumu ama utaratibu maalumu. Sambamba na malengo ya akounti iyo kua ni kujiongezea vyanzo vya mapato Kama taifa, itakua ni ishara pia ya maono kama Taifa Kwa kizazi kijacho.

3. Kufuatia mafanikio ya nchi mbalimbali Africa na hata njee ya Africa kuweza kunufaika na uwepo wa wananchi wao nje ya nchi zao wakifanya kazi mbalimbali nje ya mataifa Yao na kuwa Moja ya chanzo kikubwa Cha mapato na kuchangia Pato la taifa Kwa mataifa wanayo Toka. Mfano mzuri china wamefanikiwa kuwatumia wananchi wao nje ya mipaka ya nchi yao kua chanzo Cha mapato na hata kua na mchango wa Moja Kwa Moja katika ujenzi wa taifa lao, ivo ni shauku yangu ya kwamba Tanzania baada ya miaka 5 hadi 25 ijayo tutakua katika nafasi nzuri zaidi Kwa kua na ongezeko kubwa la wananchi njee ya mipaka yetu watakao ongeza mchango
katika Pato la taifa na kusaidia kuongeza ufadhili wa bajeti na kupunguza ukopaji wa pesa kufadhili bajeti.

Nini kifanyike
Serikali kupitia Mabalozi wake kila taifa wawajibike kutafuta ajira au fulsa mbalimbali katika mataifa waliko pangiwa kizazi, kwani Kwa kufanya ivo watasaidia kuongeza Pato Kwa taifa kupitia wananchi wake. Aidha kuwe na ushirikiani wa karibu kati ya Mabalozi na Wizara inayo jihusisha na ajira ili kutafuta fulsa nyingi zaidi Kwa watanzania nje ya mipaka ya nchi yao. Kuongeza uwajibikaji kunapaswa kuwe na ushirika baina ya Mabalozi na wizara ya ajira, Wizara ya fedha na ofisi ya Raisi utumishi na utawala bora ziwe zinapokea ripoti kutoka Kwa Mabalozi na sekretarieti ya ajila juu ya muenendo wa utafutaji ajira Kwaajili ya wananchi wenye ujuzi mbalimbali ili mwishowe mchango wao katika Pato la taifa uongezeka na ili iwe rahisi kupunguza kukopa pesa Kwa ajili ya ufadhili wa bajeti. Kufikia hatua hii Kuna hitaji uboreshwaji wa sekta ya elimu Kwa kuifanya iwe ni yenye ushindani. Lakini serikali yapaswa vile vile kuongeza utoaji wa elimu na hamasa Kwa wananchi kuwajengea shauku na utayari wa kwenda kufanya kazi nje ya mipaka yako.

Hitimisho
Hivyo basi, uanzishwaji wa harambee ya kitaifa, uanzishwaji wa akaunti ya uwekaji akiba Kwa ajili ya kujiandaa kuanza kukopesha fedha Kwa mataifa mengine yanayo endelea sambamba na kuongeza juhudi za kushirikiana na wananchi kutafuta fulsa nyingine nje ya nchi kutasaidia kuongeza pesa au mapato, ambayo Kwa namna Moja ama nyingine yatasaidia ufadhili wa bajeti ya nchi na hatimaye kuweza kupunguza utegemezi wa mikopo kama sio kuondoa katika ufadhili wa bajeti nchini kuelekea miaka 5 hadi 25 ijayo.
 
Harambee iyo ifanywe miezi miwili au mmoja kabla ya bajeti ya wizara ya fedha kusomwa na waziri mwenye dhamana. wananchi watangaziwe siku ya kufunguliwa harambee iyo miezi mitatu au zaidi kuelekea kuwasilisha bajeti bungeni ili mara baada ya bajeti ya jumla kupitishwa na bunge basi pesa izo ziwe tayari zimekusanywa kwaajili ya kuongeza mapato kufadhili bajeti ya nchi.
Hahahaaaah, ama kweli mnafikiria nje ya box. Mleta mada una imani kuu sana kwa watanzania asee. Wacha niisome zaidi hii Harambee ya kitaifa

Kweli taifa liko na think tank. Unajua kipimo cha kwamba unayemsikiliza anafikiria sana ni pale anapoleta wazo ambalo hujawahi kuliwaza, na hata uwezekano wa kuwazwa haukuwepo. Insha hii ni original idea 100% hakuna cha plagiarism wala AI hapa tunao uhakika. Tanzania tuitakayo ni motooo👌🏽
 
Hahahaaaah, ama kweli mnafikiria nje ya box. Mleta mada una imani kuu sana kwa watanzania asee. Wacha niisome zaidi hii Harambee ya kitaifa

Kweli taifa liko na think tank. Unajua kipimo cha kwamba unayemsikiriza anafikiria sana ni pale anapoleta wazo ambalo hujawahi kuliwaza, na hata uwezekano wa kuwazwa haukuwepo. Insha hii ni original idea 100% hakuna cha plagiarism wala AI hapa tunao uhakika. Tanzania tuitakayo ni motooo👌🏽
Asante kiongozi, ebu tuendelee kuandika maoni pengine yanaweza leta chachu ya maendeleo atleast kufikia miaka 5 hadi 25 ijayo kama Taifa tukawa tumeongeza kitu kutolea hapa tulipo 🙏🙏🙏.
 
Back
Top Bottom